Waziri wa Usalama wa Israel afanya sala katika eneo takatifu la al-Aqsa. Awaudhi Wapalestina

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Waziri wa Usalama wa Israel, Itamar Ben-Gvir ametembelea eneo la Msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem na kusali huko, na kukiuka mpango wa miongo kadhaa unaohusu mojawapo ya maeneo nyeti zaidi katika Mashariki ya Kati.

Picha na video za ziara yake zinaonyesha Ben-Gvir akiongoza maombi ya Kiyahudi katika boma hilo, ambalo linajulikana na Wayahudi kama Mlima wa Hekalu.

Kufanya ibada kwenye eneo hilo ni kuvunja mpango wa muda mrefu unaoruhusu Wayahudi kutembelea sehemu hiyo lakini sio kwa maombi. Sera ya Israel ni ya kudumisha makubaliano ya hali ya sasa ambayo yanaruhusu ibada ya Waislamu pekee katika eneo hilo.

Jordan, moja ya mataifa yaliyoingia katika makubaliano hayo, ilitaja ziara hiyo ya Ben-Gvir kuwa ni "uchochezi usiokubalika." Wapalestina wanaishutumu Israel kwa kuhujumu makubaliano hayo na wanalalamika kwamba wageni wa Kiyahudi mara nyingi wameonekana wakisali katika eneo hilo bila kuzuiwa na polisi wa Israel.

Hamas nayo imeiita ziara hiyo kuwa ni "uchokozi unaoendelea dhidi ya Wapalestina." Na msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amesema kwamba ziara hiyo "imevuka mipaka yote."

Wayahudi wanadai kwamba eneo lililojengwa msikiti wa al-Aqsa ni mahali patakatifu zaidi kwa Wayahudi, kwa sababu palikuwa na mahekalu mawili makubwa yanayotajwa katika Biblia.

Kwa Waislamu, eneo hilo ni sehemu ya tatu takatifu, kwa sababu wanaamini kuwa pale ndipo Mtume Muhammad alipopaa mbinguni.

Hivi majuzi, Ben-Gvir, alipendekeza ujenzi wa sinagogi katika eneo hilohilo lenye msikiti wa al-Aqsa. Hii inathibitisha habari zinazovuma kwamba Wayahudi wanafanya maandalizi ya kuuvunja msikiti huo na kujenga hekalu kubwa la tatu hapo hapo, ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Masihi. Je, hilo litawezekana? Time will tell.
Source: BBC News
 
Hii inathibitisha habari zinazovuma kwamba Wayahudi wanafanya maandalizi ya kuuvunja msikiti huo na kujenga hekalu kubwa la tatu hapo hapo, ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Masihi.
Wakiuvunja watapona mabomu ya Iran?
 
Maajabu! Eti ndipo Muhammad alipopaa mbinguni! Uwongo mkubwa! Muhammad alipaa?

Muhammad died in Medina on June 8, 632 CE, after a brief illness.

Prophet Muhammad's body is buried at the Al-Masjid an-Nabawi Mosque.
 
Hadithi za Mohammad ni vichekesho kama futuhi tu hizo story za kupaa kwenye Quran haisemi alipaa bali alichukuliwa hadi msikiti wa Mbali kichekesho hakukuwa na misikiti kipindi hicho and aya za mbele zinasema alioteshwa hahaha
 
Makafiri bado hua mpo juu juu sana,ndo mana mmeitwa ni wagalatia na hazimo
 
Maajabu! Eti ndipo Muhammad alipopaa mbinguni! Uwongo mkubwa! Muhammad alipaa?

Muhammad died in Medina on June 8, 632 CE, after a brief illness.

Prophet Muhammad's body is buried at the Al-Masjid an-Nabawi Mosque.
Na Enoch ilikuwaje
 
Na Enoch ilikuwaje
Mtume alipaa!Sasa kule Madina lile kaburi ni la nani?Mnatuambia mtume Muhammad kazaliwa Maka kafia Madina na kaburi lake liko pale,waislamu maelfu kwa maelfu hulitembelea kaburi lake mwaka kwa mwaka.Sasa iweje tena alipaa!!Aliyepaa ni nani na aliyezikwa pale Madina ni nani?
 
Maajabu! Eti ndipo Muhammad alipopaa mbinguni! Uwongo mkubwa! Muhammad alipaa?

Muhammad died in Medina on June 8, 632 CE, after a brief illness.

Prophet Muhammad's body is buried at the Al-Masjid an-Nabawi Mosque.
Si ndo nawashangaa hawa watu!
 
Waziri wa Usalama wa Israel, Itamar Ben-Gvir ametembelea eneo la Msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem na kusali huko, na kukiuka mpango wa miongo kadhaa unaohusu mojawapo ya maeneo nyeti zaidi katika Mashariki ya Kati.

Picha na video za ziara yake zinaonyesha Ben-Gvir akiongoza maombi ya Kiyahudi katika boma hilo, ambalo linajulikana na Wayahudi kama Mlima wa Hekalu.

Kufanya ibada kwenye eneo hilo ni kuvunja mpango wa muda mrefu unaoruhusu Wayahudi kutembelea sehemu hiyo lakini sio kwa maombi. Sera ya Israel ni ya kudumisha makubaliano ya hali ya sasa ambayo yanaruhusu ibada ya Waislamu pekee katika eneo hilo.

Jordan, moja ya mataifa yaliyoingia katika makubaliano hayo, ilitaja ziara hiyo ya Ben-Gvir kuwa ni "uchochezi usiokubalika." Wapalestina wanaishutumu Israel kwa kuhujumu makubaliano hayo na wanalalamika kwamba wageni wa Kiyahudi mara nyingi wameonekana wakisali katika eneo hilo bila kuzuiwa na polisi wa Israel.

Hamas nayo imeiita ziara hiyo kuwa ni "uchokozi unaoendelea dhidi ya Wapalestina." Na msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amesema kwamba ziara hiyo "imevuka mipaka yote."

Wayahudi wanadai kwamba eneo lililojengwa msikiti wa al-Aqsa ni mahali patakatifu zaidi kwa Wayahudi, kwa sababu palikuwa na mahekalu mawili makubwa yanayotajwa katika Biblia.

Kwa Waislamu, eneo hilo ni sehemu ya tatu takatifu, kwa sababu wanaamini kuwa pale ndipo Mtume Muhammad alipopaa mbinguni.

Hivi majuzi, Ben-Gvir, alipendekeza ujenzi wa sinagogi katika eneo hilohilo lenye msikiti wa al-Aqsa. Hii inathibitisha habari zinazovuma kwamba Wayahudi wanafanya maandalizi ya kuuvunja msikiti huo na kujenga hekalu kubwa la tatu hapo hapo, ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Masihi. Je, hilo litawezekana? Time will tell.
Source: BBC News
Hiv hapo Israel Kuna kanisa lenye hadhi kama huo msikiti
 
Mtume alipaa!Sasa kule Madina lile kaburi ni la nani?Mnatuambia mtume Muhammad kazaliwa Maka kafia Madina na kaburi lake liko pale,waislamu maelfu kwa maelfu hulitembelea kaburi lake mwaka kwa mwaka.Sasa iweje tena alipaa!!Aliyepaa ni nani na aliyezikwa pale Madina ni nani?
Safari ya kwenda mbinguni ilianzia "baytu Al-muqaddas" kwenda mbinguni huko ndiko alipozungumza na Allah moja kwa moja na kupewa amri ya Swala 5

Ilikuwa safali ya kwenda na kurudi na Uislamu unafundisha kuwa Yesu nae atarudi na ndiyo dalili kubwa za (kiyama)siku ya mwisho

na atapambana na (Masih dajjal)Masih wa uwongo ndiyo maana huwa nawashangaa waislam wanaomtukana "Yesu" kwa kigiriki "Lesous" na kwa Kiarabu "Isa" wanafanya hayo kwa ujinga.
 
Waziri wa Usalama wa Israel, Itamar Ben-Gvir ametembelea eneo la Msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem na kusali huko, na kukiuka mpango wa miongo kadhaa unaohusu mojawapo ya maeneo nyeti zaidi katika Mashariki ya Kati.

Picha na video za ziara yake zinaonyesha Ben-Gvir akiongoza maombi ya Kiyahudi katika boma hilo, ambalo linajulikana na Wayahudi kama Mlima wa Hekalu.

Kufanya ibada kwenye eneo hilo ni kuvunja mpango wa muda mrefu unaoruhusu Wayahudi kutembelea sehemu hiyo lakini sio kwa maombi. Sera ya Israel ni ya kudumisha makubaliano ya hali ya sasa ambayo yanaruhusu ibada ya Waislamu pekee katika eneo hilo.

Jordan, moja ya mataifa yaliyoingia katika makubaliano hayo, ilitaja ziara hiyo ya Ben-Gvir kuwa ni "uchochezi usiokubalika." Wapalestina wanaishutumu Israel kwa kuhujumu makubaliano hayo na wanalalamika kwamba wageni wa Kiyahudi mara nyingi wameonekana wakisali katika eneo hilo bila kuzuiwa na polisi wa Israel.

Hamas nayo imeiita ziara hiyo kuwa ni "uchokozi unaoendelea dhidi ya Wapalestina." Na msemaji wa Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amesema kwamba ziara hiyo "imevuka mipaka yote."

Wayahudi wanadai kwamba eneo lililojengwa msikiti wa al-Aqsa ni mahali patakatifu zaidi kwa Wayahudi, kwa sababu palikuwa na mahekalu mawili makubwa yanayotajwa katika Biblia.

Kwa Waislamu, eneo hilo ni sehemu ya tatu takatifu, kwa sababu wanaamini kuwa pale ndipo Mtume Muhammad alipopaa mbinguni.

Hivi majuzi, Ben-Gvir, alipendekeza ujenzi wa sinagogi katika eneo hilohilo lenye msikiti wa al-Aqsa. Hii inathibitisha habari zinazovuma kwamba Wayahudi wanafanya maandalizi ya kuuvunja msikiti huo na kujenga hekalu kubwa la tatu hapo hapo, ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Masihi. Je, hilo litawezekana? Time will tell.
Source: BBC News
Kama kule uturuki jumba la kikiristo lilichukuliwa na serikali na kufanywa msikiti, hakuna aliyesema chichote, unadhani hilo la kuvunja huo msikiti inashindikana?
Mbona inawezekana tu.
Historia inaonyesha kabla ya msikiti huo hapo palikuwa na Hekalu. Kama Hekalu lilivunjwa pakajengwa msikiti, hata msikiti utavunjwa pakengwe Hekalu. Ni swala la wakati tu
 
Sisi wasabato hayatuhusu.
Ila mada hii inawahusu
 
Makafiri bado hua mpo juu juu sana,ndo mana mmeitwa ni wagalatia na hazimo
I think ulitakiwa kuweka aya inayopingana na alicho kisema huyu "kafiri" laa hufanyi hivo, wasomaji wenu tutamtafsiri msemaji kwamba alikua sahihi au wewe ndio hukijui kitabu chako
 
Back
Top Bottom