Waziri wa 'Vijana' atazunguka nchi nzima kusikiliza kero za Vijana?

and 998 others

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
28,477
Reaction score
40,278
Waziri Nanauka anaonekana na msafara wake anazunguka vijiweni, Stendi kusikiliza kero za Vijana. Je huu utaratibu utachukua muda gani ili kupata maoni ya vijana kwa nchi nzima?
 
Attachments

  • images (71).jpeg
    images (71).jpeg
    70.2 KB · Views: 25
Amenikumbusha enzi Hayati Ali Hassan Mwinyi alipokuwa kila jumamosi anakutana na wananchi pale Ofisi za CCM Lumumba.

Lakini aliacha na utaratibu ule baad ya kuona hauna tija wala malengo yaliyokusudiwa hayafikiwi.

Mfumo ndiyo unaotakiwa kurekebishwa na wala siyo kujifanya mtu wa vijiwe vya vijana wakati haiba hiyo hauna.
 
Waziri Nanauka anaonekana na msafara wake anazunguka vijiweni, Stendi kusikiliza kero za Vijana. Je huu utaratibu unachukua muda gani ili kupata maoni ya vijana kwa nchi nzima?

Pamoja na nia yake njema angetengeneza pia online platform kuwezesha Vijana kuwasiliana naye
Njia aliyochagua ni nzuri ila bila kuchanganya na Online platform atakuwa ameliacha kundi moja muhimu sana nje kwani kuna vijana wengi ambao hawahudhurii mikutano ya hadhara
 
unateua motivational speaker kuwa mbunge na waziri..sijui awalete vijana pamoja, mbona huteui wale ambao wamefanikiwa kibiashara na wameanzia chini kabisa na sasa wamekwenda hadi nje ya mipaka ya Tanzania kibiashara..? Hao ndio mfano wa kuigwa na vijana wakisema na vijana wanawaelewa! kina Nyambari yule mtunzi wa vitabu..motivational speaker..? hicho anachoandika au kusema yeye mwenyewe hajawahi kujaribu..! mambo ya motivational speakers afrika hayana impact!
 
Nchi ina vituko kila mtu anazurula tu atakavyo

Kero zipo kibao kwa zaidi ya miaka 64
Leo ndo hivi viazi vinazurula na misafara kujua kero??!

Pimbi hizi zenyewe tu ni KERO.
 
Mimi ni CCM ila siungi mkono anachokifanya NANAUKA. Ni maigizo kama maigizo mengine. Kero za vijana zinajulikana hakuna haja ya kupoteza muda kuzunguka vijiweni. Na hizi kero haziwezi isha kama sheria hazitabadilishwa. Kuna mambo mengi mno ya kipuuzi yangeachwa kufanywa yangeleta mabadiliko ya haraka kwenye maisha ya vijana. Kwa mfano miradi kama ile ya BBT ingepigwa chini na pesa kupewa vijana walime wenyewe. Pia mikopo kwa vikundi ni kupiga chini na kukopesha vijana mmojammoja wanaojitambua. Serikali haishindwi kukopesha Tsh 20m kwa vijana 100 kila mkoa ambao tayari wapo kwenye biashara ili wazikuze zaidi. 20m kwa vijana 100 ni bilioni 2 tu. Kwa mikoa 30 ni bilioni 600 kitu ambacho inaweza bila kufikiria mara 2.
 
Hawawezi kufanya hivo mkuu.
 
Waziri Nanauka anaonekana na msafara wake anazunguka vijiweni, Stendi kusikiliza kero za Vijana. Je huu utaratibu unachukua muda gani ili kupata maoni ya vijana kwa nchi nzima?
Watanzania mbona mnakuwa warahisi sana kutapeliwa? CCM imekuwepo kwenye madaraka kwa muda gani? Samia amekuwepo kwa muda gani? Ina maana muda wote hawajui ni nini ''kero'' za vijana mpaka wapite vijiweni? Walipokuwa wanaomba kura walikuwa hawajui vijana wana shida gani na walikuwa wanasubiri waibe kura ndiyo waanze kuuliza? Unaweza kuomba kuongoza wananchi ambao hujui shida yao?
 
Mimi ni CCM ila siungi mkono anachokifanya NANAUKA. Ni maigizo kama maigizo mengine. Kero za vijana zinajulikana hakuna haja ya kupoteza muda kuzunguka vijiweni. Na hizi kero haziwezi isha kama sheria hazitabadilishwa. Kuna mambo mengi mno ya kipuuzi yangeachwa kufanywa yangeleta mabadiliko ya haraka kwenye maisha ya vijana. Kwa mfano miradi kama ile ya BBT ingepigwa chini na pesa kupewa vijana walime wenyewe. Pia mikopo kwa vikundi ni kupiga chini na kukopesha vijana mmojammoja wanaojitambua. Serikali haishindwi kukopesha Tsh 20m kwa vijana 100 kila mkoa ambao tayari wapo kwenye biashara ili wazikuze zaidi. 20m kwa vijana 100 ni bilioni 2 tu. Kwa mikoa 30 ni bilioni 600 kitu ambacho inaweza bila kufikiria mara 2.
Anafaa awe mtangazaji wa clouds 360. Yule bwana. Mfupi mnene hivi sijuiam. Anaitwa nani
 
Back
Top Bottom