Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 11,612
- 16,189
GTs,
Samia tangu amteue Nanauka kuwa waziri wa vijana sijaona alichofanya zaidi ya kucheza bao na wahuni aliowakodisha.
Yaani badala ya kuamrisha yafuatayo;
1. Kuhakikisha vijana hawatekwi tena
2. Kuhakikisha vijana wote waliofariki maiti zao zinapatikana
3. Kuhakikisha vijana wote waliokamatwa wanaachiwa huru,
4. Kuhakikisha vijana wote walioumizwa na Polisi wanatibiwa bure
5. Kuhakikisha vijana wote waliouawa wanapata kumbukumbu siku maalumu na yeye kama Waziri anasimamia
6. Kutembelea familia zilizofiwa na zenye majeruhi ili kuwafariji
Katika yote hayo wizara hii haijafanya hata moja zaidi ya kunenepesha mashavu kujifanya anazurura na gari.
Sijaona hata sehemu moja maslahi ya vijana kayagusia.
Iwapo vijana wakiandamana D09 huyu kibarua chake kiote nyasi, hajui mahitaji ya vijana.