TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu, amesema Andrew Nkuzi msemaji wa familia ya Mwapachu.

1613111446729.png

============

Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu ameieleza Mwananchi Digital kuwa mwili wa mbunge huyo wa zamani utawasili Tanga leo jioni na utahifadhiwa nyumbani kwake Mchukuuni kata ya Tangasisi.

Amesema mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika kesho Jumamosi Februari 12, 2021 kijiji cha Pande Wilaya ya Tanga.

Mwapachu alikuwa Mbunge wa Tanga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 alipomwachia kijiti Omar Nundu (marehemu) na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini katika vipindi tofauti.

Soma pia - The History of Mwapachu family in relation to uhuru struggle
 
Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Bakari Mwapachu, amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa February 12, 2021 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa Matibabu

Amesema Andrew Nkuzi msemaji wa familia ya Mwapachu.

Chanzo: Mwananchi
 
Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu, amesema Andrew Nkuzi msemaji wa familia ya Mwapachu. #MwananchiUpdates
Mtoa mada, nadhani iko haja uweke sawa; aliefariki hakuwa kuwa Balozi.

Harrith Bakari Mwapachu aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ndani na sio balozi.

Aliewahi kuwa Balozi Ufaransa na baadae katibu mkuu wa East African Communuty ni mdogo wake ambae ni Balozi Juma Mwapachu.
Poleni sana Watanzania, wana Tanga na familia yote wa Mwapachu kwa msiba huu.
 
Duh! Namkumbuka mzee Mwapachu.

Pole sana wanafamilia, na sote tulioguswa na msiba huu. Nyakati ngumu sana hizi! Mungu mwenyezi azidi kutujaza neema za kuyapokea mapenzi yake japo ni yenye kuumizwa katika ubinadamu.
 
Back
Top Bottom