TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

mtoa uzi umesema amefariki leo alfajiri tarehe 12feb ilikuwa ijumaa halafu umesema atazikwa kesho jumamosi tarehe 12 feb.Kuna utata hapo ila nadhani ni makosa ya bahati mbaya rekebisha basi
jumaWaziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu, amesema Andrew Nkuzi msemaji wa familia ya Mwapachu.

View attachment 1700461
============

Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu ameieleza Mwananchi Digital kuwa mwili wa mbunge huyo wa zamani utawasili Tanga leo jioni na utahifadhiwa nyumbani kwake Mchukuuni kata ya Tangasisi.

Amesema mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika kesho Jumamosi Februari 12, 2021 kijiji cha Pande Wilaya ya Tanga.

Mwapachu alikuwa Mbunge wa Tanga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 alipomwachia kijiti Omar Nundu (marehemu) na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini katika vipindi tofauti.

Soma pia - The History of Mwapachu family in relation to uhuru struggle
 
Sasa mnategemea raisi awaambie kila siku mvae barakoa ? Mwanzoni huko aliwaonya na kutoa tahadhari,unategemea kila siku awambieni vaeni barakowa na kunawa kwa maji tiririka,
ameshatoa tamko ni wewe na nwele zako nikimaanisha akili. Msitegemee atarudi tena awaambie mvae barakowa.
 
Back
Top Bottom