TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

Aliefariki ni Balozi Bakari Harith Mwapachu

Picha imewekwa kimakosa, Bakari alikuwa na style yake ya miaka yote ya kuchana nywele kwa mtindo wa kulalia nyuma, wakati Juma ana style ya kuficha mvi

Aliwahi kuwa Waziri wa Sheria wakati wa Utawala wa Bw.Benjamin Mkapa, akahudumu kama Waziri wa Usalama wa Raia kwny Cabinet ya Kwanza ya Bw.Jakaya Kikwete

Juma ni mdogo wake ambae aliwahi kuwa Tanzania one kwny matokeo ya kidato cha sita miaka ya kati kati ya 1960s, pia akawa Katibu wa Jumuia ya Afrika Mashariki


Hii ni familia kubwa na yenye historia kubwa sana kwny history ya kuanzia harakati za uhuru Baba yako akiwa Mwamba katika miamba ya wakati huo

Allah ampe kauli thaabet Balozi Bakari bin Harith bin Mwapachu
Apumzike kwa amani,hivi huyo ni Juma Mwapachu au ni Bakari Mwapachu...?
 
inna lillah wainna ilayh raajiun


Retired njoo tumzike jirani mwenzetu yan ndio mana lile beach bonaza la kila jumapili la wiki iliyopita halikuepo kumbe ndio alikua mgonjwa
 
Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu, amesema Andrew Nkuzi msemaji wa familia ya Mwapachu.

View attachment 1700461
============

Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu ameieleza Mwananchi Digital kuwa mwili wa mbunge huyo wa zamani utawasili Tanga leo jioni na utahifadhiwa nyumbani kwake Mchukuuni kata ya Tangasisi.

Amesema mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika kesho Jumamosi Februari 12, 2021 kijiji cha Pande Wilaya ya Tanga.

Mwapachu alikuwa Mbunge wa Tanga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 alipomwachia kijiti Omar Nundu (marehemu) na amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini katika vipindi tofauti.

Soma pia - The History of Mwapachu family in relation to uhuru struggle
RIP Mwapachu.
Alikuwa mnyakyusa?
Kwa nini azikwe Tanga.
 
Back
Top Bottom