TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

TANZIA Waziri wa zamani, Bakari Mwapachu afariki dunia

Mtoa mada, nadhani iko haja uweke sawa; aliefariki hakuwa kuwa Balozi.

Harrith Bakari Mwapachu aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ndani na sio balozi.

Aliewahi kuwa Balozi Ufaransa na baadae katibu mkuu wa East African Communuty ni mdogo wake ambae ni Balozi Juma Mwapachu.
Upo sahihi, jina lake kamili ni Harith Bakari Mwapachu. Amewahi kuwa waziri wa iliyokuwa wizara mpya ya usalama wa raia 2005-2008. Pia waziri wa katiba 1995-2005. Wakati wa Mkapa, mzee Mwapachu na JK ndio mawaziri pekee waliohudumu wizara zao kwa miaka 10 mfululizo. Mdogo wake ndio amewahi kuwa balozi France.
 
Apumzike kwa amani,hivi huyo ni Juma Mwapachu au ni Bakari Mwapachu...?
 
Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu, amesema Andrew Nkuzi msemaji wa familia ya Mwapachu.
View attachment 1700461
============

Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Balozi Bakari Mwapachu amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu ameieleza Mwananchi Digital kuwa mwili wa mbunge huyo wa zamani utawasili Tanga leo jioni na utahifadhiwa nyumbani kwake Mchukuuni kata ya Tangasisi.

Amesema mazishi ya kiongozi huyo yatafanyika kesho Jumamosi Februari 12, 2021 kijiji cha Pande Wilaya ya Tanga.

Mwapachu alikuwa Mbunge wa Tanga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 alipomwachia kijiti Omar Nundu (marehemu) na amewahi kushika nafasi za mbalimbali za uongozi serikalini katika vipindi tofauti.
Chanzo cha mauti tafadhali
 
Back
Top Bottom