TANZIA Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia

TANZIA Waziri William Lukuvi (na Mbunge wa Isimani) afariki Dunia

Afu ujue kuna uzi aliandika ndgu yetu ngara23 kuhusu matukio ya kufa wabunge toka MO29 mods naomba muunganishe tafadhari..
Kulikua na huu pia.


Ni nature ilivyo popote kwenye uonevu basi lazima namna itajitokeza kupambana na uonevu ni nature hiyo.

Kundi lolote linaweza kuonewa mwanzo ila mwisho wa kuna siku watapata namna kufanya retaliation hata kama haitakuwa kubwa basi kuna wakati napo itawaumiza kundi onevu.
 
Ving'ang'a huyu na mwenzake Jenista. Wote Mpaka kifo ndo kimewatenganisha na Cabinet, na wote wamepita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Sera,Bunge, Utaratibu na nini )
Gridi ya taifa haibagui Rais, waziri, mbunge na raia wa kawaida. Hata ukipanua wigo mpana kwa kutafuna njugu itakuondoa tu na presha.

King Kong III Erythrocyte
 
Ile siku bungeni wanamtamgaza waziri wao mkuu Mwigulu walipangwa wabunge wazoefu ndiyo waongee kwanza. Ambao ni pamoja na Lukuvi na Mhagama. Na wote wa wamekata moto
 


Rais Samia, amesikitika kutangaza kifo cha William Vangimembe Lukuvi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Isimani.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Lukuvi amefariki dunia leo tarehe 25 Machi, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu kufuatia ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Rais Samia ametoa salamu za pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia msiba huo.
View attachment 3562430


Historia ya William Lukuvi​

William Vangimembe Lukuvi ni mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Tanzania ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya ardhi, maendeleo ya makazi, na siasa za kitaifa. Akiwa Mbunge wa Jimbo la Ismani kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1995 mpaka kufariki mwaka 2026, Lukuvi ameshikilia nyadhifa mbalimbali za uwaziri.

Maisha ya Awali na Elimu
William Lukuvi alizaliwa tarehe 15 Agosti 1955 katika kijiji cha Mapogoro, Wilaya ya Iringa Vijijini, Tanganyika. Alipata mafunzo yake ya awali katika Tabora Teachers College (TTC) na baadaye kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Huria cha Tanzania.

Safari ya Kisiasa
Lukuvi alianza safari yake ya kisiasa kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ismani mnamo mwaka 1995 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), nafasi ambayo ameendelea kushikilia hadi amefariki Dunia March 25, 2026.

Aidha, amehudumu kama Waziri katika nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge.

Mnamo Juni 2023, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mshauri wa Rais kuhusu Mahusiano ya Kisiasa na Kijamii na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Rais Samia alimteua William Lukuvi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) nafasi ambayo ameishikilia mpaka kufariki kwakwe.

Zaidi, Soma=> CV ya William Lukuvi
R.I.P mh. william
 
Back
Top Bottom