Waziri ya Ardhi yashiriki uzinduzi wa michezo ya Mei Mosi 2025

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
Michezo ya wafanyakazi kuelekea kilele cha Mei Mosi 2025 imefunguliwa rasmi tarehe 22 Aprili 2025, katika Uwanja wa CCM LITI mkoani Singida. Uzinduzi huo umehudhuriwa na mamia ya watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali za serikali, mgeni rasmi akiwa ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Pascal Katambi.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, Mhe. Katambi amesisitiza umuhimu wa michezo hiyo kwa ajili ya kuimarisha afya, mshikamano na kuongeza morali kazini miongoni mwa wafanyakazi.

“Natoa wito kwa wakuu wa idara na taasisi kuhakikisha wanawapa nafasi watumishi wao kushiriki michezo hii kikamilifu, kwani michezo huongeza weledi, hamasa na kuimarisha mahusiano kazini,” alisema Mhe. Katambi. Aidha, Mgeni Rasmi alikemea vikali Idara na Taasisi za Serikali ambazo hazikushiriki Michezo hii kuwa atawachongea kwa Mamlaka ya Uteuzi kwakuwa wanarejesha nyuma juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendeleza michezo na kuwajengea Afya njema Watumishi wa Umma.

Wizara ya Ardhi ni miongoni mwa taasisi zilizojitokeza kushiriki kikamilifu katika mashindano hayo, ikiungana na taasisi nyingine.
IMG_2289.jpg

Michezo ya Mei Mosi imekuwa chachu ya mshikamano na umoja miongoni mwa watumishi wa umma, na ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayotarajiwa kufanyika rasmi tarehe 1 Mei 2025.

Siku hii ni muhimu kwa wafanyakazi kote duniani kupaza sauti zao, kuonesha mshikamano wao na kusherehekea mafanikio ya utumishi wao kwa taifa.
 
View attachment 3312983

vipi wakuu na nyinyi ni "no reforms no election" au nyinyi ni "ubaya ubwela" tu
 
Back
Top Bottom