Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Nikushukuru sana Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri, wakati nakuja Watu waliniuliza utavaa nguo zako za mitumba au utavaa kitu kipya, lakini leo nimetia suti mpya, maana hata hiyo mitumba ni sehemu ya mazingira na ni sehemu ambayo inachafua hadhi ya Nchi yetu.

Rais Magufuli umefanikiwa sana kupiga vita mifuko ya Plastic, lakini sasa mifuko hiyo inarudi kwa njia za pembeni, vifungashio (packages) sasa vinaboreshwa na Watu wanabebea vitu na kuharibu mazingira, watu wa NEMC tuulize kwanini vitu hivi viko mitaani, nitalifanyia kazi.

Kwa Watu wa Wizarani (Muungano na Mazingira) urafiki upo lakini kwenye kazi za Umma hatutofanya urafiki, tukikutana nje ya kazi za Umma tutaendelea na Urafiki wetu.

Amakweli mwenye shibe kamwe hamjui mwenye njaaa sasa tusubiri mapya ya kupiga marufuku mitumba.



Sent using Jamii Forums mobile app
Duu bloo angu [emoji12]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebu tutolee huo upotoshaji usiyo na tija kwa taifa, unataka kutwambia kuwa nyie ndiyo mliyomsikiliza pekee yenu? Tazama michango ya watu wote mnataka kusema hawana akili?
Wacheni ujjnga wenu wa kuficha pembe la ng'ombe
Exactly, alichosema ni kuwa mitumba ni sehemu ya mazingira sema tu inashusha hadhi (kuna mahala hupaswi kuvaa mitumba kama alivyokuwepo yeye leo).
Kwa lugha rahisi ametetea wauzaji wa mitumba waliompa kura (soko la Karume/Ilala) yeye kiasi ya kuaminiwa na leo kuvaa suti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tijifunze kuvaa vipya tutakuwa na mawazo mapya.

Mimi namuunga mkono. Mitumba imepitwa na wakati.
 
Ebu tutolee huo upotoshaji usiyo na tija kwa taifa, unataka kutwambia kuwa nyie ndiyo mliyomsikiliza pekee yenu? Tazama michango ya watu wote mnataka kusema hawana akili?
Wacheni ujjnga wenu wa kuficha pembe la ng'ombe

Sent using Jamii Forums mobile app
Umejitahidi kuniqoute kila mara lakini sioni logic yeyote ya quotations zako.
Please be specific,what is wrong?
Is he right or wrong? na kama hayuko sawa nini suluhisho?
Maoni yako yamesimamia wapi ili tujadili kwa kina.?
JF ni sehemu huru ya kujadili ilimradi tusivunje sheria za nchi na wengine wapate kujifunza sio busara kufumbafumba facts.
 
Leo 27/01/2020 baada ya kuapishwa Waziri Mpya wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Hassan Zungu alisema yafuatayo, "Nikushukuru Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri. Wakati nakuja watu waliniuliza utavaa nguo zako za mitumba au utavaa kitu kipya, lakini leo nimetia suti mpya, maana hata hiyo mitumba ni sehemu ya mazingira na ni sehemu ambayo inachafua hadhi ya nchi yetu.

Mavazi ya mtumba husaidia Watanzania wenye maisha ya kati na duni kujisitiri, si hivyo tu baadhi yake hukaribia ubora wa yale mavazi mapya.Je Waziri alikuwa sahihi? Ama itakuwa sahihi kuzuia nguo hizi?Tuchukue hatua zipi?

Karibuni wana JF.
Naona historia ya mitumba huijui.

Ni hivi juzi juzi tu, mwaka jana au juzi mwishoni walitishiwa nyau tu kwa kuzuiwa kwenye mpango wa AGOA wote kasoro Rwanda wakaukunja mkia. Huyo waziri mpya bado hajaelezwa uhalisia wa mambo.

Hizo 'jeans' zinazotengenezwa hapo kwa Mkapa Economic zone watawauzia akina nani?
 
Yaani viongozi wanataka kuendesha wizara na nchi mithili wanavyoendesha nyumba ndogo...!!
Hivi unateuliwa tu hivi unakuja na matamko na vitisho...
Are all these based on a researched information??
Unataka kuzuia mitumba sawa je, una mbinu mbadala za kusitiri utu na biashara za common wananchi?
Shame on you id 1oTs!
 
Back
Top Bottom