Wazo duni? Rais Samia atayaweza mengine, Muungano mtihani kwake

Wazo duni? Rais Samia atayaweza mengine, Muungano mtihani kwake

mavumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
596
Reaction score
328
Nimebahatika kufuatilia na kushiriki mikutano na mijadala maeneo mbalimbali kuhusu Muungano wa Tanzania hii.

Mitazamo ya baadhi ya watu inaashiria muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar unaendelea kuwa moja ya mambo yenye udonda sugu. Kila inapotokeza fursa ama tukio la kuujadili muungano, mambo yanayoibuliwa kadiri siku zinavyoenda yana mwelekeo wa kuibuka kwa hoja za nguvu na zinazokinzana kuhusu huu muungano wa Tz na Zanzibari. Ingawa wapo wanaosema kuwa wenye mitazamo fulani ama wana uchu, wana ubaguzi, hawajui wasemalo na kadhalika, ipo haja ya kutazama yafuatayo.

Mwalimu Nyerere (RIP) alitumia ushawishi wenye upeo mkubwa kuwaondoa watu kwenye haja ya kuunda upya muungano. Kwa kuona mbali, alishawishi kuundwa Chama kimoja kwa pande zote mbili, kama kete himili na hii ndio turufu ya muungano. Mambo yalipoonekana kufikia hali tete aliwahi kuwaambia WaTz "Dhambi ya ubaguzi ni sawa na kosa la kuonja nyama ya mtu" (sijui ukweli kuhusu hili aliupata wapi). Hata hivyo, Ushawishi wake ulikuwa nguvu ya aina yake katika kuustawisha muungano

Alhaji Ali Hassan Mwinyi alitumia ushawishi wa kuwasukuma WaZanzibari kuzichangamkia fursa za kimamlaka (kuteua watendaji waandamizi kwenye nafasi za muungano) na hamasa kwa zile za kiuchumi zilizokuwepo bara, na wakati huo WaTz Bara wakiwa na upeo mdogo wa ujasiriamali, waZenj walizitumia. Mzee Mwinyi alifanikiwa kwa namna hii kuweka mustakabali wenye utulivu kwa kipindi chake. Sante Mzee Ruksa!

Mhe Uncle Ben Mkapa (RIP) alifanikiwa kurekebisha mifumo ya kiuchumi lakini kwenye la muungano alionekana kukubali Zanzibar ichukue nafasi yake katika mambo ya kujiendesha baada ya kipindi kigumu ilichopitia kutokana na mivutanio ya kisiasa Visiwani. Mtihani alioupata ni pale alipolazimika kutumia vikosi vya jeshi kutuliza mihemko yenye kuashiria kuyumba kwa dola Zanzibar.

Mhe Bro J M Kikwete alionyesha nia njema ya kuwashawishi WaZanzibari waondoe kwanza tofauti zao (Unguja vs Pemba), lakini katika kipindi chake ndipo hali ilionekana kushamiri kwa madai ya fursa sawa zaidi katika masuala ya kiuchumi. Ndiye aliyetamka rasmi kuwa Gesi na Mafuta vilivyopo ndani ya eneo la mipaka ya Zanzibar ni vya Zanzibari (hili liliibua hoja kali na mijadala mikubwa lakini mwenzetu aliitumia hii kama kete mojawapo ya kuwapooza WaZanzibari)

Marehemu JPM (RIP), yeye alipeleka ujumbe wa moja kwa moja kwamba pamoja na yoote yaliyopo na yaliyopita, Dola ni moja tuu. Alisema Mwaka 2020 kwenye mkutano wa Kampeni viwaja vya Mnazi Mmoja, "Mimi ndiye Rais...Mkuu wa Mkoa yupo hapa? Chukua jina na namba ya simu ya huyo mama" (Sijui alisahau kwamba Wakuu wa Mikoa wa Zanzibar huteuliwa na Rais wa Zanzibar na huwajibika kwa anayewateua?)

Mwenendo wa mijadala na maamuzi ya mambo ya Muungano vinaashiria ujasiri na ushawishi wa aliyepo madarakani. Uwezo wa kukabiliana na nguvu zinazokinzana , na kuchukua maamuzi yenye misimamo ni kipaji cha mtu na pale ambapo hofu itaingia kwa sababu za kitamaduni ama kuogopa lawma, mambo yanaweza kubadilika vizuri kabisa.

Mlio karibu naye mtieni moyo wa ujasiri
 
Angeitumia hii fursa vizuri kuumaliza huu msuguano kupitia njia sahihi; ikiwemo ile ya kuendesha kura ya maoni kwa wananchi wa pande zote, iwapo bado wanauhitaji huu Muungano, au la! Na kama bado wanauhitaji, basi waeleze bayana wanata Muungano wa aina gani/wa muundo upi!

Kinyume na hapo, huu mvurugano utaendelea mpaka mwisho. Wazanzibari wengi hawataki Muungano, na Watanganyika wengi pia hawaoni faida yoyote ile ya huo Muungano!

Kwangu mimi mpaka sasa, naamini ni CCM pekee ndiyo inayotaka Mungano.
 
Rais wa JMT akitokea Zanzibar anakuwa na tabia ya upendeleo uliopitiliza.
 
Wameshindwa maraisi waliopita hata hayati Julius muungano ulimshinda kutatua matatizo na masahibu yake . Tusimuonee mama hatoweza sababu ilani ya ccm haitaki kugusa muungano
 
alisemaje nzee
Marehemu JPM (RIP), yeye alipeleka ujumbe wa moja kwa moja kwamba pamoja na yoote yaliyopo na yaliyopita, Dola ni moja tuu. Alisema Mwaka 2020 kwenye mkutano wa Kampeni viwaja vya Mnazi Mmoja, "Mimi ndiye Rais...Mkuu wa Mkoa yupo hapa? Chukua jina na namba ya simu ya huyo mama" (Sijui alisahau kwamba Wakuu wa Mikoa wa Zanzibar huteuliwa na Rais wa Zanzibar na huwajibika kwa anayewateua?)
 
Back
Top Bottom