Wazo Fyatu: Jaribio la Kumkinga Samia Linaendelea - Tutarudi Tulikotoka?

Wazo Fyatu: Jaribio la Kumkinga Samia Linaendelea - Tutarudi Tulikotoka?

Na waliovunja maduka, kuchoma Mali Za watu na kupora karma Yao ni nini?
We mzee punguza wenge na kuwashwa washwa, thamani ya mali haifikii hata theluthi ya maisha au uhai wa mtu.

Watoto wachanga, vilema, omba omba, wanawake wakiwa ndani, wanaume wakiwa wana angalia mpira wali uliwa without a question or any interrogation.
 
Ewe mwananchi kujilinda dhidi ya policcm ni jukumu lako binafsi.

Iwe kwa bunduki,panga,shoka,mkumi au mshale kujilinda ni jukumu lako.
Nimekuwa nikiwaambia watu humu kuwa waache kuwa wanyonge.

Waanze kujilinda kwa namna yoyote ile wawezayo.

Tunadili na mijitu ambayo haina ubinadamu.

Yakikukamata hata ujieleze vipi, yatakupiga na kukuua.

Nimesikiliza clip moja nadhani ilikuwa sijui maeneo ya Tabata yale…..

Wamembananisha mshikaji wa bodaboda. Jamaa kajaribu kwa kila namna kujielezea lakini wapi! Yakampiga risasi na kumuua.

Katika hali kama hiyo hakuna jinsi tena. Kuwa mnyonge siyo option.

Heri wakuue ukiwa unapambana nao kuliko wakuue ukiwa unawabembeleza wakunusuru maisha yako.

Wamekosa akili na busara za kutambua kwamba wananchi wakianza kujihami na kujilinda, hiyo ni vita ambayo hao askari hawawezi kushinda hata kidogo.

Hakuna polisi wala jeshi la kuwazuia Watanzania zaidi ya milioni 60!

Na kiukweli hatuna polisi wala jeshi linaloweza kukabiliana hata na watu milioni moja tu.

Hakuna tena kurudi nyuma. Ni kusonga mbele tu sasa.
 
Udini unakusumbua!! Ile siku 29/11 ulikua na shauku na ghamu yakutaka kuona mnafanikiwa baada ya kile kichapo mmegeuza shingo!! Mpumbavu sana wewe tulishakubaini kitambo kuwa ni mdini uliyepindukia!
Wale wauaji walikuwa wanauliza dini yako kwanza ndio wakushoot?

DINI NI ULEVI MMOJA MBAYA SANA.

Unaacha kufuata amri za Mungu uko bize kutetea dini.
 
Kwa siasa za kimataifa hii miaka ya karibuni za kihafidhina , tusitegemee msaada wowote kutoka nje kukabiliana na huyu mwanamke muuaji....
Maana Sudan wameuwa zaidi ya 3000 kwa siku moja na bado yanaendelea, lakini wazungu wameziba masikio....
Maana kwa mauaji yaliyotokea nchini, na anakaa kimya kama hayakutokea, basi ni kuanza kuelewa wale wazee wa Kibiti baada ya vijiji vyao kunyanyaswa na na watu kuuwawa na kupotea, waliona mbali.....
Hamadi, wakafikia mpaka huku



 
MY TAKE;
  • Wito wangu ni kuwa kuanzia sasa Watanzania mjihami wenyewe. Nyumba yako ndio himaya yako. Usipoweza kujilinda na kuwalinda watu wa nyumbani mwako unaweza kulinda nini kingine? Msipoweza kulinda Watoto wenu kutoka kwenye “illegal search and seizure” mtaweza kulinda nini. Mtu anweza kuja hana waranti, hana amri yoyote ya mahakama anakuja nyumbani au dukani kwa mtu na watu wanamuacha tu. Toka lini bunduki imekuwa ni kitambulisho cha uaskari? Watanzania lindeni mitaa yen una nyumba zenu, lindeni mabinti zenu na Watoto wenu wa kiume, lindeni wenyewe! Msiache mtu aje na kufanya atako juu yenu!
sasa mtu kaja na bunduki, wako wawili watatu halafu we huna bunduki utakabiliana vipi na hao wenye bunduki? Wito wa kujilinda umeeleweka! Kwa hali iliyotokea wananchi watajilinda the way they can
 
Na waliovunja maduka, kuchoma Mali Za watu na kupora karma Yao ni nini?
Karma is the law of cause and effects, and it acts both sides kwa mtenda na mtendewa.

Mfano Chadema waliwahi kumtenda vibaya huyu kada wao, nikawashauri Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"

Fuatilia all the main players, kila mmoja yamemkuta ya kumkuta, one after the other!

Kwa hiyo kwenye baadhi ya hizo mali zilizoharibiwa, some of them could be zilipatikana kwa ill gotten money, hivyo kushambuliwa kule ndio karma yake.

P
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tanzania tuliyoijua kabla ya Oktoba 29, 2025 haipo tena, haiwezi kuwepo tena, na hata tukiitaka kwa machozi hatuwezi kuipata tena. Tanzania iliyojivunia “umoja na mshikamano” na “amani na utulivu” imetoweka kama ukungu wa alfajiri na kama umande wa asubuhi imeyeyuka. Siyo Samia, wala wasaidizi wake wanaoweza kuirudisha Tanzania ile. Mwiko umevunjwa, laana imetenguliwa, mtego waliotegwa Watanzania kwa miaka sitini ya utawala ulioshindwa wa CCM umeteguliwa na kizazi kipya cha wajukuu na vitukuu wa mababu! Kwaheri CCM, kwaheri Tanzania ile!

Toka matukio ya siku ile ya giza na usiku ule wa damu wa Oktoba 29, ambapo Watanzania walishuhudia Uchafuzi Mkuu wa 2025 (uliojiigiza kama Uchaguzi Mkuu) nimetatufa maneno mengi ya kusema lakini nimejikuta nashindwa kuyapata kwa usahihi na nikikosa uthubutu wa kuyatamka yaliyonijia kichwani. Nimeona picha na video nyingi, nimesikiliza wengi kwenye mitandao, na nimesubiria kwa hamu nione kama kuna yeyote ndani ya hawa watawala mwenye utulivu wa akili ambaye angeweza kuliambia Taifa ni nini hasa kimetokea. Kwa vile wamekosekana wa kusema na kwa vile yale tuliyoyaona bado yanatoa harufu ya miili ya Watoto wetu na machozi ya mama zetu nimejikuta nimepata nguvu kidogo ya mimi kusema kitu. Nina mambo matano ya kusema.

  • Laana ya Mjerumani kwenye Akili za Watanganyika Imevunjwa: Baada ya kujua kuwa Wajerumani kufuatia kumalizika kwa Kongamano la Berlin 1884-1885 wamechukua Tanganyika rasmi na kuifanya sehemu ya himaya yao mababu waliamua kuasi kiakili na kivitendo. Mababu waliokuwa na tofauti mbalimbali za kihistoria na kikabila walijikuta wanaunganisha nguvu zao kumpinga Mjerumani a.k.a Mdachi. Mababu walianza harakati za kufanya vita vya msituni na kushambulia kambi mbalimbali za Mjerumani.

  • Karl Peters alijulikana kama mikono ya damu kwa jinsi alivyomwaga damu ya mababu zetu. Mababu walipoamua kuunganisha makabila karibu ya ishirini kumpinga Mjerumani ndipo ugomvi na watawala ulipoiva moto. Matokeo yake ni vita vya MajiMaji. Mjerumani akaamua kuja na hatua kali Zaidi za kuzima mababu ikiwemo kunyonga viongozi wa wananchi, kusababisha baa la njaa kwa kuchoma mazao na vyanzo va maji. Wajerumani kama CCM na serikali yake miaka 125 baadaye walileta mamlumki kuwaua mababu. Leo kusikia kuna watu kutoka nje wamekuja kuua ndugu zetu ni kuwa historia imejirudia tu!

  • Hata kabla ya vita ya MajiMaji (1905-1907) Mjerumani alishaanza kunyonga viongozi wa makabila mbalimbali ikiwa ni njia yake ya kutoa onyo kwa yeyote atakayewakataa Wajerumani. Nitataja wachache waliouawa kabla ya vita ya Majimaji na baadaye wakati wa vita hivyo:
  • Ma-Mangi 19 walionyongwa hadharani pale Old Moshi Machi 2, 1900 kwa kumpinga Mjerumani. Miongoni mwao ni Mangi Ngalami wa Siha, Mangi Molelia wa Kibosho, Mangi Lebolu wa Meru, Mangi Lebanga wa Arusha, na Mangi Meli wa Moshi. Wengine kama kina Abushiri nao walinyongwa sehemu mbalimbali za Tanganyika kabla ya vita vya Majimaji.
  • Huko Songea Machi 2, 1906 Nduna Songea alikubali kunyongwa kuliko kuishi chini ya Mjerumani; ilikuwa siku tatu baada ya wenzake 66 kunyongwa.
Alichokifanya Mjerumani kiliumiza akili na hisia za Watanganyika kiasi kwamba wazo la kutokumpinga mtawala lilitushika kichwani kwa miaka. Matokeo yake TANU ilipoanza harakati za uhuru haikuweza kuhamasisha matumizi ya nguvu. Tulijengewa woga na mjerumani kiasi kwamba CCM ilipokuja kushika madaraka ilikuwa inatuimbia wimbo wa “amani na utulivu” kama “code” ya kutuambia msije kusahau kilichotokea kwa mjerumani; na mara zote wananchi wanarudi wanaufyata kimya.

Walichokifanya vijana hawa juzi ni kuvunja hofu hiyo na yeyote anafikiria Watanzania watawaogopa tena watawala wakati wana mifano sasa hai kabisa ya kuwa nchi yao ni kubwa Zaidi kuliko uhai wao, na kuwa katika ulimwengu huu hakuna mtu ambaye anaweza kuwatendea Watanzania bila kuulizwa au kupingwa! Laana ya Mjerumani imevunjwa!! Watanzania wanaweza kuwa wameshuhudia mtu mwingine akiitwa ‘Mikono ya Damu’.

  • Kuua Mamia na kushtaki Waliobakia Hakutazima Roho ya Kuwapinga Watawala. Hili ni somo la kihistoria. Katika kujaribu kupuuzia kilichotokea watawala wetu wanajaribu kuwalaumu waliokufa na wanakwepa kabisa kujiangalia kwenye kioo na kujiuliza ni kwa jinsi gani wao walisababisha yaliyotokea Oktoba 29. Nimesema wanajaribu kumkinga Samia. Kiukweli ni kuwa wanajaribu kuwalaumu waliouawa na kuwanyoshea kidole; kwamba waliouawa kwa sababu waliwapinga watawala.

  • Hadi hivi sasa wanataka tuamini kuwa tuliyoyaona kuamkia Alhamisi ile hadi tarehe 3 Novemba ni vitu tulivyovitengeneza vichwani mwetu tu. Kwamba, hakukuwa na mauaji, na kama yalikuwepo basi yalifanywa na wageni na wa kulaumiwa ni kina Mange na Maria Sarungi! Hii ni alama ya juu kabisa ya mtu mwoga na asiyetaka kuwajibikwa makosa yake mwenyewe. Yaani, wale waliokuwa wanapiga wananchi wetu risasi mitaani, barabarani, kwenye nyumba zetu, kwenye vibanda vya kuangalia filamu walifanya hivyo wakiongozwa na Mange na Sarungi! Yaani, wale jamaa tuliowaoana wanatembea na silaha na kumwaga risasi hovyo barabarani walifanya vile kwa sababu Maria Sarungi na Mange waliwaagiza! Huu ni wendawazimu wa watu waliolewa madaraka na kulewa bwii!!

  • Hivyo, tunavyomsikia AG Johari ati anaapa kuwatafuta kina Mange na Sarungi badala ya kutafuta mamluki walioua Watoto wetu inaudhi na inakera! Yaani, amekereka na ukali wa maneno ya kina Sarungi na Mange na watu wa mitandaoni badala ya ukali wa risasi za wenye visasi kwenye mitaa yetu! Leo wanawafungulia mashtaka ya uhaini Watoto wetu, vijana wetu, mbwa, sisimizi, na kuku ilimradi tu wasiwafungulia mashtaka wauaji wa Watoto wetu! Ni ufyatu per excellence!

  • Kutokana na Mauaji Haya Hawatatoka Madarakani kwa Kura Kirahisi: Kuanzia kurejea kwa mfumo wa vyama vingi tumekuwa na Imani kuwa kuna namna ya kuweza kuiondoa CCM madarakani kupitia sanduku la kura. Toka 1995 hadi hivi sasa watu walikuwa wanaenda kupiga kura wakitegemea kuwa wanaweza kuitikisa nchi na kuing’oa CCM. Tulikuwa tunapata wabunge wengi tu wa upinzani na tulijiaminisha kuwa tunaweza kupiga kura nyingi na kuweza kumkataa mgombea wa Urais toka CCM.

  • Uchaguzi huu a.k.a Uchafuzi Mkuu wa 2025 umetuonesha jambo moja wazi toka mwanzo kabisa. CCM ilikuwa katika udhaifu mkubwa kuliko wakati mwingine wowote ule. Woga wao ndio uliowafanya wachukue hatua kali Zaidi kwa upinzani. Kufunga na kuwasweka wale wote waliowaona kuwa ni tishio lao na hakuna aliyewatishia kwenye Urais kama Tundu Lissu. Kama Lissu aliweza kukampeni wakati wa Magufuli na kupata kura karibu milioni 2 za mizengwe ni wazi kuwa mwaka huu kama wangethubutu kidogo tu CCM siyo tu ingeanguka lakini ingeanguka kwa kishindo kikuu! Ni kwa sababu hiyo waliamua kutumia nguvu yote kubakia madarakani.

  • Kwa sasa kuwatoa kwa kutumia kura inaonekana ni ngumu lakini naamini inawezekena. Lakini haitokuwa rahisi hasa kwa sababu ya damu hii iliyototesha ardhi ya mababu zetu tena, kuamsha mizimu na kuwaamsha mahoka!


  • Kwa Mashujaa Huenda Kilio kwa Waoga Kicheko. Sikuwahi kuufikiria sana msemo huu hadi matukio haya ya juzi. Leo kuna nyumba na familia zina misiba. Kuna wamama wanalia (namfikiria mama Niffa mfano mmoja tu). Watu wanalia kwa kupoteza Watoto wao, waume zao, wadogo zao n.k Kama mababu walivyolia kupotezwa kwa ndugu zao wakati wa vita va MajiMaji. Vita ile ilichukua Maisha Zaidi ya watu 75,000 katika Tanganyika! Wanaodhania Watanzania ni waoga hawajui historia!

  • Watawala wetu wanakumbatiana na kuchekeana, wanapigiana saluti na kutiana moyo. Wanaamini wamezima jaribio la kuwakataa madarakani. Ndugu zangu, historia ni mwalimu mzuri sana. Tuliyoyaona Oktoba 29 yatajirudia tena na labda kwa hasira Zaidi. Kama risasi zingeweza kuzuia fikra za watu leo hii Gaza kungekuwa kumetulia! Ukraine kungekaa kimya! Mtu akishavuka mpaka wa woga hana cha kuogopa tena. Hawa vijana na wengine watoka tena kwa hasira Zaidi kuwapinga watawala. Siamini kama kuna risasi za kutosha kuzuia fikra za wananchi! Wamekataa kuleta mabadiliko ya kweli sasa mabadiliko yanaletwa hata wakikataa!

  • Bahati mbaya sana kwao sasa hivi ni kuwa umwagikaji mkubwa wa samu uliotokea umetengeneza mtego. Samia na wenzake watatakiwa kujibu swali iliwezekana vipi mamia ya Watanzania kuuliwa wao wakiwa madarakani. Hawawezi hata kidogo kusingizia “wageni kutoka nje”. Kwa vile hawawezi kukwepa kuwajibika na hili kinachotokea sasa ni kuwa lazima walindane maana nje ya hapo licha ya kuendelea kupigiana saluti hatima yao ni moja! Nakuwa wa kwanza kusema kuwa si miezi mingi mashtaka yataletwa dhidi ya Samia na baadhi ya wakuu wa vyombo vya usalama na hati za kukamatwa kwao zitatolewa ili wajibu mashtaka ya mauaji ya Watanzania. Kuwalaumu Mange, Sarungi na mitandao hakutawasaidia!

  • Ushauri wangu kwa hasa maaskari wa chini na watendaji wa chini tunzeni Ushahidi wa mawasiliano yenu na wakubwa wenu!! Tunawaangalia wanavyocheka sasa, tunawaangalia wanavyoenda kugawiana vyeo. Tukumbuke kuwa wote wanaopokea vyeo hivi sasa hivi ni sehemu ya watawala walioleta ile Oktoba 29. Tutawakumbuka hawa, hatutawasahau!

  • Rais Samia anawajibika moja kwa moja kwa yote yaliyotokea Oktoba 29 hadi hivi sasa. Siyo Abdul, siyo Wazanzibari, siyo Waganda, siyo Maria Sarungi, siyo Mange Kimambi, siyo watu wa Clubhouse, siyo kina MMM, siyo wengine wote. Ni lazima yeye ajibu na kuwajibika kwa yaliyotokea na kutokea yeye kuna msururu wa viongozi waliochini yake ambao watasimamishwa pamoja kujibu. Inaweza isiwe kesho, au keshokutwa, lakini watasimama kujibu. Ikumbukwe, kesi za mauaji hazina ukomo wa kuletwa mahakamani. Sasa hivi waendelee kufurahia magari yenye viyoyozi na bendera zinasopepea kwa raha, kwa sasa waendelee kufurahia kupigiana saluti na kupeana mikono ya pongezi, kwa sasa waendelee kuimbiana nyimbo za shangwe lakini tumeshaona yanayotokea kwa Rais wa Zambia, hawa hawataweza tena kutembea kwa starehe kujifanya hawajui kilichotokea. Kwa sasa wajue kuwa isipokuwa wasimame na kukiri makossa yao, wasimame na kuwajibishana wenyewe kwanza kabla hawajawajibishwa na Watanzania au jumuiya za kimataifa.

  • Kuendelea kujificha vichwa vyao chini kama mbuni na kupuuzia kilichotokea ni kujidanganya; watawajibika tu; mmoja mmoja au kwa pamoja.

  • Watanzania Wanapaswa Kuanza Kujilinda Wenyewe. Nimeona video moja ya vijana wakichapwa viboko hadharani huko Mwanza (nafikiri). Yaani, polisi wanakuja na kuwala watu kifudi fudi na kuwapiga kama Watoto wadogo. Tumesikia matukio ya watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi wakipita nyumba kwa nyumba na kuchukua vijana na kupiga watu. Tumeona milango na kuta zilizopigwa risasi na watu ambao wakiaminiwa kuwa ni ‘askari’.

  • Wito wangu ni kuwa kuanzia sasa Watanzania mjihami wenyewe. Nyumba yako ndio himaya yako. Usipoweza kujilinda na kuwalinda watu wa nyumbani mwako unaweza kulinda nini kingine? Msipoweza kulinda Watoto wenu kutoka kwenye “illegal search and seizure” mtaweza kulinda nini. Mtu anweza kuja hana waranti, hana amri yoyote ya mahakama anakuja nyumbani au dukani kwa mtu na watu wanamuacha tu. Toka lini bunduki imekuwa ni kitambulisho cha uaskari? Watanzania lindeni mitaa yen una nyumba zenu, lindeni mabinti zenu na Watoto wenu wa kiume, lindeni wenyewe! Msiache mtu aje na kufanya atako juu yenu!

Kwa sababu, Tanzania ile ya kabla ya Oktoba 29 haipo tena. Tanzania tuliyoijua kabla ya Oktoba 29, 2025 haipo tena, haiwezi kuwepo tena, na hata tukiitaka kwa machozi hatuwezi kuipata tena. Tanzania iliyojivunia “umoja na mshikamano” na “amani na utulivu” imetoweka kama ukungu wa alfajiri na kama umande wa asubuhi imeyeyuka. Siyo Samia, wala wasaidizi wake wanaoweza kuirudisha Tanzania ile. Mwiko umevunjwa, laana imetenguliwa, mtego waliotegwa Watanzania kwa miaka sitini ya utawala ulioshindwa wa CCM umeteguliwa na kizazi kipya cha wajukuu na vitukuu wa mababu! Kwaheri CCM, kwaheri Tanzania ile!
Shida ni akili ndogo kufunika akili kubwa , na akili kubwa kukubali kufunikwa, na akili ndogo. Na
Kuna waandishi wa habari , chawa na wengine viongozi wanafurahia, lakini Hali hii, bila hawaelewi kwamba mafanikio yao, misingi yake sio yazege Bali mchanga, hivyo muendelezo wake ni mfupi
 
Udini unakusumbua!! Ile siku 29/11 ulikua na shauku na ghamu yakutaka kuona mnafanikiwa baada ya kile kichapo mmegeuza shingo!! Mpumbavu sana wewe tulishakubaini kitambo kuwa ni mdini uliyepindukia!
Wewe ni zaidi ya mjinga!
Samuya anapingwa kwa ukilaza wake, haya Lipumba kamuambia 'unapwaya, unapwaya'...unasemaje hapo kuhusu udini?!.
 
Duh this time hakuna atakayetoka kinyonge, ule ujasiri ni cha mtoto. Nasikia this time watadili na individuals (askari, makada, familia zao na mali zao) hapa ndio patamu. Yaani unarudi nyumbani huna bunduki unakua man to man. Lazima wakufanye kama walivyomfanya Sabela kwenye movie ya Sarafina
 
Wito wangu ni kuwa kuanzia sasa Watanzania mjihami wenyewe. Nyumba yako ndio himaya yako. Usipoweza kujilinda na kuwalinda watu wa nyumbani mwako unaweza kulinda nini kingine? Msipoweza kulinda Watoto wenu kutoka kwenye “illegal search and seizure” mtaweza kulinda nini. Mtu anweza kuja hana waranti, hana amri yoyote ya mahakama anakuja nyumbani au dukani kwa mtu na watu wanamuacha tu. Toka lini bunduki imekuwa ni kitambulisho cha uaskari? Watanzania lindeni mitaa yen una nyumba zenu, lindeni mabinti zenu na Watoto wenu wa kiume, lindeni wenyewe! Msiache mtu aje na kufanya atako juu yenu!
Point kubwa sana
 
Umeandika mengi na mengi yana maana lkn nakuuliza swali moja tu wale waliokuwa wanaiba na kuchoma mali za hao Watanzania wenzao, na nasikia wengine wamekatwa vidole kwa sababu ya kuwa na wino wa kupigia kura nao kosa lao lipi ? kama tunaimba hiyo demokrasia na tunakandamiza pia uhuru wa watu wengine hiyo si sawa

Shida yetu bado ni ile ile ujinga na umasikini ndo vina zaa chuki, rushwa, kuoneana tamaa, wivu na ma uchafu yote haya
Demokrasia mnayo iimba kwa jicho la ulaya ni tofauti na mazingira yetu haya ya umasikini na elimu duni kule uelewa wao na elimu zao ni tofauti na sie

Mfano watu wangeandamana kwa kupeleka ujumbe kwa bango na mazingira ya kutokuleta fujo na uporaji
Nafikiri wasingewapa hata nafasi ya wanaotumia udhaifu huo kuona ilikuwa ni kuleta machafuko na vurugu tu

Sio hao Chadema wala CCM wote wale walewale tu kwa kizazi hiki maana ni zao la jamii hii hata nani aje rushwa na kukandamizana hauwezi kumalizika mara moja

kubwa tuanze kubadili mitazamo yetu kama jamii kuanzia ktk ngazi ya familia, tuheshimu utu na uwajibikaji na kuheshimiana
Umeleta point ambayo ni dhaifu sana, acheni kutafuta visingizio. Kipi kilianza kwanza? Kwa kila kitu kitokeacho kuna chanzo. Usipoziba ufa utajenga ukuta. Sasa hapa ndiyo inabidi CCM na Serikali wajenge ukuta. Kwani wewe ulitegemea nini kwenye maandamano ya watu walioteseka kwa kutekwa, kuuliwa ndugu zao, njaa, na joblessness, corruption nk nk iliyosababishwa na hii serikali na CCM? Hizo ndiyo gharama ya udhalimu. Haya mambo yalianza muda mrefu na sasa ndiyo yamechemka, na kuzima itakua kazi kwa sababu watu ule utu wao waliokuwa nao umetoka.

Achane majibu na maswali rahisi kwa matatizo magumu kama haya, wenye uwezo acha waongee.
 
Asha Rose Migiro katibu mkuu wa chechemaa, katibu mkuu (naibu) wa UN mstaafu, balozi mstaafu, lecturer mstaafu, hivi huu uchaguzi wa 29/10 aliuona uko powa kabisa?
What went wrong?
Amekubali kabisa kua mmoja wa viongozi wa chechemaa hata baada ya watoto wasio na hatia kupoteza maisha?
Wasomi wetu Tanzania akipata ulaji tu basi anabweteka, hata akili zinawatoka.
 
Nimekuelewa sana na point zako zina mashiko ya chanzo cha matatizo lakini ninacho kataa ni njia iliyotumika kwa pande zote mbili waandamanaji na upande wa kuzuia maandanano na hili haielezewi sana sijui kwanini
Unapodai haki yako usivunje haki za wengine mwisho wake inakua ni uwehu na mihemko tu
Huo utekaji au ukandamizaji una mahusiano gani na kupora duka au Bar au mali ya mtu binafsi na ndo tulivyoona kwa sehemu kubwa
Toeni elimu sahihi ya watu kuandamana na kutoa maoni yao bila kuumiza wasio husika mnatuumiza sie ambao tupo neutral na ma ujinga yenu wote wa chama tawala na hao wana harakati
 
Umeandika mengi na mengi yana maana lkn nakuuliza swali moja tu wale waliokuwa wanaiba na kuchoma mali za hao Watanzania wenzao, na nasikia wengine wamekatwa vidole kwa sababu ya kuwa na wino wa kupigia kura nao kosa lao lipi ? kama tunaimba hiyo demokrasia na tunakandamiza pia uhuru wa watu wengine hiyo si sawa

Shida yetu bado ni ile ile ujinga na umasikini ndo vina zaa chuki, rushwa, kuoneana tamaa, wivu na ma uchafu yote haya
Demokrasia mnayo iimba kwa jicho la ulaya ni tofauti na mazingira yetu haya ya umasikini na elimu duni kule uelewa wao na elimu zao ni tofauti na sie

Mfano watu wangeandamana kwa kupeleka ujumbe kwa bango na mazingira ya kutokuleta fujo na uporaji
Nafikiri wasingewapa hata nafasi ya wanaotumia udhaifu huo kuona ilikuwa ni kuleta machafuko na vurugu tu

Sio hao Chadema wala CCM wote wale walewale tu kwa kizazi hiki maana ni zao la jamii hii hata nani aje rushwa na kukandamizana hauwezi kumalizika mara moja

kubwa tuanze kubadili mitazamo yetu kama jamii kuanzia ktk ngazi ya familia, tuheshimu utu na uwajibikaji na kuheshimiana
Wewe ni mpuuzi. Uhai wa mtu huwezi kuulinganisha na mali. Isitoshe tusingefika hapa kama maccm yangeheshimu haki za wananchi. Acha kufocuss na matokeo, focuss na chanzo. Maccm ndio yametufikisha hapa.
 
Na waliovunja maduka, kuchoma Mali Za watu na kupora karma Yao ni nini?
Halafu watu ni wajinga eeh? Kwani tungefika hapa kama maccm yangeheshimu haki za raia? Maccm yameteka watu, yanapoteza watu, yanahongana rasilimali za taifa, yanauza bandari na rasilimali za watanzania. Maccm yametufikisha hapa kwa sababu ya ulafi wa madaraka na mali. So acheni upuuzi wa kufocuss na matokeo badala ya chanzo
 
Back
Top Bottom