Wazo lako usione watu wanalipinga ukafikiri wana mihemko ila huo mwanya wa kuandamana hawatoi hicho kibali as long as sababu ya kuandamana inawavua nguo watawala Mfano maandamano ya TLS yalivyonyimwa vibali nchi nzima ila Yale maandamano ya kina Jokate yaliruhusiwaNimekuelewa sana na point zako zina mashiko ya chanzo cha matatizo lakini ninacho kataa ni njia iliyotumika kwa pande zote mbili waandamanaji na upande wa kuzuia maandanano na hili haielezewi sana sijui kwanini
Unapodai haki yako usivunje haki za wengine mwisho wake inakua ni uwehu na mihemko tu
Huo utekaji au ukandamizaji una mahusiano gani na kupora duka au Bar au mali ya mtu binafsi na ndo tulivyoona kwa sehemu kubwa
Toeni elimu sahihi ya watu kuandamana na kutoa maoni yao bila kuumiza wasio husika mnatuumiza sie ambao tupo neutral na ma ujinga yenu wote wa chama tawala na hao wana harakati
Wale jamaa walipofikia hakuna chembe ya diplomasia watayotumia maana tayari wameshakuwa na sifa za uhalifu sio viongozi tena
Swali ni je wadai haki watumie njia gani kudai haki zao kwa mazingira haya?