Wazo Fyatu: Jaribio la Kumkinga Samia Linaendelea - Tutarudi Tulikotoka?

Wazo lako usione watu wanalipinga ukafikiri wana mihemko ila huo mwanya wa kuandamana hawatoi hicho kibali as long as sababu ya kuandamana inawavua nguo watawala Mfano maandamano ya TLS yalivyonyimwa vibali nchi nzima ila Yale maandamano ya kina Jokate yaliruhusiwa
Wale jamaa walipofikia hakuna chembe ya diplomasia watayotumia maana tayari wameshakuwa na sifa za uhalifu sio viongozi tena

Swali ni je wadai haki watumie njia gani kudai haki zao kwa mazingira haya?
 
Wewe ni mpuuzi. Uhai wa mtu huwezi kuulinganisha na mali. Isitoshe tusingefika hapa kama maccm yangeheshimu haki za wananchi. Acha kufocuss na matokeo, focuss na chanzo. Maccm ndio yametufikisha hapa.
Hakuna sehemu nimefurahia uhai wa mtu yoyote kuondolewa na kwa sababu zozote

Kama ambavyo umesema haya yaneletwa kutokana na chanzo na ni sahihi kabisa lakini hata haya maafa kwa maana ya vifo, uporaji na uharibifu bado navyo ni sababu hizo hizo ya chanzo cha kuwapa watu hamasa kengeufu bila utaratibu mzuri na kama kuna uwajibikaji uwe wa pende zote kwa maana zote zimehusika , wenye dola na washawishi wa maandamano

Wapi ilitoka elimu sahihi namna ya kuandamana kwa amani na utulivu? Je kusema kuna uungwaji mkono wa hii movement na watu watoke kwa uhuru lkn imekuja kinyume chake na damu nyingi kumwagika na mali nyingi kuharibiwa

Mie napinga uonevu wote kwa upande wa dola na pia nakataa kuwapa haki wengine kuhalalisha uporaji na machafuko maana muumiaji mkuu ni sie wananchi wa kawaida

Tutafute namna bora kutatua mzozo huu bila kuumiza watu zaidi na kumwaga damu zaidi na hasa kwa sie ambao tupo neutral tunapambania familia zetu tunaona tupo trapped kwa huu mzozo

Kwa walio ndani ya mfumo na wanaopambania kuingia ndani ya mfumo ni wale wale tu ni zao la jamii hii ya ubadhirifu, rushwa na ufisadi
 
Kiukweli nimeumia sana na hakuna kipindi nikechukia polisi na CCM kama kipindi hiki
 
Ni swali zuri na fikirishi ndo tukae kama jamii tuone hii changamoto tuna ipatia ufumbuzi upi na pia mie sijakataa maandamano lkn vitendo vya ku trigger hao wanaopinga maandamano visingekuwepo sidhani kama silaha za moto zingetumika

Watu walipoanza kupora na kuvunja miundo mbinu na mali za watu binafsi ndo hasa ilianza shida mpaka tumepoteza vijana wetu wengi, sijapinga maandamano yawe yana kibali au vinginevyo , nacho kataa namna ya kuandamana na ndo yanafanya watu kama sie ambao tupo neutral tuone hayana tija zaidi ya uharibifu tu na umwagaji damu usio na sababu za maana
Hao organizers wote wa hayo maandamano kama ndo kwa namna ile ilivyokuwa nao wanahusika na vifo vya ndugu na jamaa zetu
 
Unawaza kwa ufupi na uduni mno...!!!

Tatizo halitatuliwi kwa kuangalia matokeo. Tatizo hutatuliwa kwa kuangalia chanzo chake!!

Wewe bila shaka ni mmoja wa washauri na watendaji wa serikali hii mlio wajinga na wapumbavu ktk kufanya maamuzi...!

Jiulize chanzo cha maafa haya ni nini kilichopelekea watu kukatwa vidole, mali kuharibiwa, watu kuuwawa na uharibifu mwingine..!!

Tatizo limeanzia wapi kiasi cha kusababisha hayo...?

Hilo👆🏻👆🏻 ndilo swali la msingi kwa watu wenye akili, ufahamu, hekima na busara watajiuliza. Watu kufa, kukatwa vidole, mali kuharibiwa na maafa mengine ni matokeo ya tatizo...!!

Hatutatui tatizo kwa kuangalia matokeo bali tatizo hutatuliwa kwa kuangalia kisababishi i.e chanzo..!!

Maana watawala hawa na CCM yao kama zilivyo akili zako na mawazo yako ya kuwaza vidole vilivyokatwa na mali zilizipotea tayari wanafikiri kuwa chanzo cha uovu huu uliotendeka ni waandamanaji, wakemea uovu mitandaoni kina Maria Sarungi, Mange Kimambi, Viongozi wa CHADEMA, Askofu Josephat Gwajima na wengine..

Huo ndio ujinga wenyewe wa watawala unaosemwa na Mzee Mwanakijiji. Wanaangalia matokeo badala ya chanzo.

👉🏻Wanahangaika na walioonya juu ya hatari iliyo mbele yetu, kushauri: Gwajima, Polepole, CHADEMA/Tundu Lissu na wengine

👉🏻Wanahangaika na waliopiga kelele mitandaoni kina Mange, Maria Sarungi nk

##Wanaacha kushughulika na chanzo. Na kama hujui, ni kuwa, chanzo cha maafa yote haya yaliyotokea: Maandamano ya kuipinga serikali, watu kupigwa risasi na kuuwawa kwa maelfu, mali kuharibiwa ni KIBURI, JEURI NA DHARAU YA SERIKALI NA RAIS SAMIA DHIDI YA WANANCHI kwa kutufanyia dhuluma dhidi ya haki zetu za msingi za kushiriki uchaguzi huru, wa haki na wa wazi na kuaminika ili kuchagua viongozi tuwatakao..!

Chezeni makida makida yote mtakayo, lakini kusema ukweli kabisa, Samia na wenzake CCM ndilo tatizo letu. Likiondoka hili, tunaweza kuwa salama..!
 
Mkuu hao milioni 60 sio wote wana mtizamo kama wako au huo ?

Kama sikosei ww unatoka huko usukumani hivi unajua sehemu kubwa ya maeneo huko Shinyanga na Tabora hata watu hawajajua hasa shida ilikuwa nini ukitoa Mwanza na Kahama na Mara kwa ukanda huo

Tuendelee kuhamasishana kuhusu amani na maridhiano na kama nyie mpo nje afu ndo mna trigger hii sijui watu wauwane mtatuingiza chaka na mbaya itafika hatua sio mtu na polisi itakuwa sisi kwa sisi wananchi mkuu .
Sitetei uonevu kwa wenye dola dhidi ya Raia wake lkn siwezi intertain vurugu na kumwaga damu kwa sababu zozote nina imani hata kwenye giza kali bado kuna njia ya matumaini mkuu na amani itatawala kwa wote

Hivi alieporwa mali zake na kuharibiwa sehemu yake ya biashara anaona kama unavyoona wewe nae akitaka kujihami na sio kwa sababu ya polisi ila kuhami uporaji na uharibifu wa mali yake hapo si mzozo wa sisi kwa sisi?
 
Mkubwa mie najua chanzo lkn kusema aina ya kuadamana ile imeleta pia maafa na hizi pande zote zinatakiwa kuwajibika

Na kwa taarifa yako mie sijawahi na sina unufaika wowote kwa walio ndani ya utawala na sana ni muhanga wa utawala na sijawahi kuamini ktk utatuzi wa changamoto zangu eti nipate upendeleo kwa wenye mamlaka
Na deep down nina chuki na baadhi yao kwa wizi,rushwa na ubadhilifu wao lkn njia ya vurugu na kupora na kupoka haki ya wengine na hasa sie tulio kati neutral ni kutuumiza kwa maslahi ya pande hizi mbili kwa faida zao
 
Mwamba umeongea point kubwa sana na ndio ilitakiwa iwe Uzi kabisa
 
Hata Kama CCM imetufikisha hapa tulipo inahusiana vipi uharibifu wa Mali za watu wengine?
 
Unapoleta ishu mali na uhai wa watu nakuona kama mpuuzi TU

Unalinganishaje mali miundombinu na uhai wa watu.
Nyie ndo wale bus linapata ajali mnasikitikia bus kuliko uhai wa walikuwa kwenye bus

Mali zinatafutwa hata kulipwa fidia , uhai wa raia wako unaweza kulipia fidia ???
 
Hongera mkuu uchambuzi wa kisomi kabisa
Msaidie Mzee mwenzako Pascal Mayalla
 
Mkuu kuhamasisha amani upande wa wananchi tu sidhani kama inasaidia na ndio imetufikisha hapa, ndio maana watu wanazungumzia chanzo kwa maana kuna namna serikali kwa upande wao wanaubiri amani ila wanafanya mambo ambayo hayaendani na amani.
 
Hata Kama CCM imetufikisha hapa tulipo inahusiana vipi uharibifu wa Mali za watu wengine?
Ndipo ilipotufikisha ccm kwamba tumefikia hatua hadi kunapatikana watu wanaamua kuharibu miundombinu na mali binafsi za watu, ndio maana tunarudi kulekule tu cha muhimu kuangalia chanzo.
 
Ndipo ilipotufikisha ccm kwamba tumefikia hatua hadi kunapatikana watu wanaamua kuharibu miundombinu na mali binafsi za watu, ndio maana tunarudi kulekule tu cha muhimu kuangalia chanzo.
Huwezi ku enjoying uharibifu wa Mali za watu ambao ni raia wa kawaida kwa kuona ni Jambo la kawaida eti kisa hasira zako na CCM huo ni uhalifu
 
Huwezi ku enjoying uharibifu wa Mali za watu ambao ni raia wa kawaida kwa kuona ni Jambo la kawaida eti kisa hasira zako na CCM huo ni uhalifu
Kwa hiyo ccm sio wahalifu waliotufikisha hapa? Natamani kukuuliza umeishia darasa la ngapi ila naogopa utaigeuza kuwa ndio hoja
 
Ni suala la muda tu Samia atamfuata Jean Bosco Ntaganda mahali panapostahili watu wa aina yake.
 
Kwa hiyo ccm sio wahalifu waliotufikisha hapa? Natamani kukuuliza umeishia darasa la ngapi ila naogopa utaigeuza kuwa ndio hoja
Sipingi maandamano ila ninachopinga ni matumizi mabaya ya maandamano kupitia hayo maandamano vitu vingi vya watu vimeibiwa, Mali za watu zimevunjwa na miundombinu imeharibiwa hivi unachoma vituo vya mwendokasi wakati nawe una upanda hiyo mwendokasi wewe unadhani hii imekaa sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…