Wazo Gomvi: Kabla ya Kujitoa CHADEMA Ingeeleza Hili Kwanza...

..Why not?

..kama ni jambo jema na litakaloleta heri na amani kwa nchi yetu kwanini lisifanyike?

..Je, tunatoa wapi uhalali wa kujiita WAZALENDO?
Mkuu , anachosema Kalamu1 ni kukoksekana uwezekano wa CCM kukaa na vyama vingine kuangalia mustakabali wa amani.

Tatizo ni CCM ambayo inaoenakana kama organiziarion lakini ukweli ni kuwa imekufa kuliko vyama vya upinzani . Sasa wapinzani watakaa mezani na nani?

CCM ya sasa si chama ni CCM ya mtu. Hata CCM wenyewe hawapendezwi na yanayoendelea lakini hakuna anayethubutu kwasababu si chama kile cha wanachama ni'one man show''

CCM unayoiona inasimamishwa na Polisi na vyombo vingine si ile unayoiujua ya wanachama
Ukiona mtu anaimba si kwasababu anaipenda, hapana! ndipo mkono unapoanzia kuelekea kinywani.

Kususia uchaguzi ni ku draw public attention na kupitia hilo vyama vianze kuhamasisha na kuwaelemisha wananchi kuporwa haki zao za kirai, kugeuzwa misukule n.k.
Hakuna mabadiliko ya maana bila nguvu ya umma ambayo haijawahi kushindwa duniani
 
Inasikitisha sana kuona kuna watu ni kama vile hawajuwi kinachoendelea.Lakini ni ukweli usiopingika aliyeratibu hii hujuma ana akili ndogo mno.Alichoambulia ni kuiabisha serikali na ameiabisha CCM yake.Miaka minne wapinzani hawafanyi siasa,viongozi wao wamehamishia ofisi zao Kisutu, lakini bado mnaogopa kushindana nao?.Awamu ya tano imejiwekea historia ya ajabu sana.
 

Hivi unafikiria nilichoandika hapa nimekiandika mara ya kwanza? Tatizo ni kuwa watu wananisoma kwa kufikiria "baada ya 2015". Tatizo langu na mikakati ya upinzani kuiondoa CCM siyo suala la leo. Ni tatizo la muda mrefu na matokeo yake ndiyo haya sasa.
 
''Nione umamtangaza mpinzani''! halafu leo tunadhani kuna matatizo ya ufundi!

Mzee Mwenzangu usije ukawa umeingia huu mtego mbaya sana uliowanasa upinzani wa Tanzania. Unataka tuamini kuwa CCM ina jukumu na wajibu wa kuwatengenezea wapinzani mazingira safi ya kufanya siasa ili wapinzani hao hatimaye waje kuiondoa CCM madarakani? Kwamba, walegeze kila mahali, wawasaidie wapinzani ili "upinzani ukomae"? Kwamba, CCM wasijitahidi "kuua" upinzani ili waendelee kutawala kwa miaka mingi? Ni mtego mbaya sana huo. Ukinasa ni vigumu kunasuka.
 
We kunywa Bia...mambo ya Jafo yamekorogeka...Chadema ni mpango wa Mungu.......CCM wanatakiwa wajifunze jambo kupitia uchaguzi huu.....
 
Achaneni na huyo Mwanakijiji. Nadhani ameamua kujivika ujinga.
 
Hivi CCM waleenguliwa wangapi ? vilena kama wote wamepita inaingia akilini?. Mi nijuavyo mazingira waliko wagombea yanafanana mfn elimu waliyopata , vijiji, vitongoji na mitaa e
walipo iweje CCM wao wawe smart 100%?.

Wala hawahitaji kuwa smart; wenzenu wanawazidi kwenye ujanja. Na ujanja mmojawapo ni labda kila mtu anapojaza fomu zinapitiwa na mtu mwingine au kiongozi wake na kuhakikishwa hazina makosa ya kawaida. Binafsi ningependa kweli kuona baadhi ya hizi fomu zilizokataliwa.
 

..nadhani kauli au mitizamo kama hii ina-discourage siasa za haki na kistaarabu.

..ccm ikiendelea namna hii kwa kukandamiza wengine mwisho wa nchi ni nini?

..hivi mnafikiri ccm wakishavisambaratisha vyama vya upinzani, wataishia hapo hawatashughulika na wengine?
 
Mwombe Polepole. Ana nakala zote.

Mwanakijiji ujisikitikie maana hakuna unachokijua. Wagombea wengi walioenguliwa hawakufanya kosa lolote. Sehemu nyingine yalitolewa maelekezo, kateni wote. Wakikatwa wote wapo watakaokata rufaa tutawarudisha lakini watakuwepo watakaokata tamaa. Tutakuwa tumepungiza.

Mzee Mwanakijiji sasa hivi umekuwa kama debe tupu. Unaandika bila ya kuwa na taarifa kamili wala kujua uhalisia wa mambo. Kwa hili la uchaguzi wa serikali za mitaa ni aheri ungenyamaza, usiandike chochote kwa sababu hujui chochote. Unapotaka kuonekana una uelewa wakati watu wanaojua wanafahamu kuwa wewe hujui chochote, wanakudhatau sana, kama wanavyofanya sasa. Ushabiki wako umekufanya ukose weledi na utashi.
 
Mkubwa, ninakuelewa vizuri sana ! kwamba lazima Wapinzani watafute njia mbadala

Kwa kuanzia waachane na ''insanity'' ya kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile wakitegemea matokeo tofauti. nakuelewa.

Ninachokiona ni hatari inayotengenezwa na CCM wenyewe ambayo haitakuwa nzuri kwa kila mmoja wetu. Nyerere aliporidhia vyama vingi alielewa mabadiliko yanayotokea.

Leo kuna idadi kubwa ya kizazi ambacho hakikuona mazishi ya Nyerere

Nyerere alijua ''resentment' inayojengeka ni mbaya na kwamba ipo siku CCM itashindwa kuzuia na nchi kulipuka. Akakubali minority wasikilizwe kutokana nyakati
Nyerere hakumaanisha kujenga mazingira kwa Wapinzani, alilenga kuepusha balaa

Hawa wapinzani ni representative wa sehemu kubwa ya jamii ambayo ina chuki na hali ilivyo.

Dalili za chuki hiyo tumeziona wiki kadhaa pale watu wanaposubiri kwa shauku kuhusu tangazo baya. Hii ni dalili kwamba hali siyo njema kama wanavyodanganyana

Yule kijana wa Tunisia aliyejichoma moto alisababisha middle east ikawaka moto.

Si kwamba watu walisikitishwa na kujichoma moto bali walikuwa wanatafuta sababu ya kueleza resentment zao zilizojengeka muda mrefu. Mibuyu, mikuyu na mipingo ikaanguka!

Matatizo ya 2007 Kenya yanasemwa kama ukabila. Ukiangalia kwa undani kilichochoe ni resentment za hao hao ndani ya ukabila. Sababu ilipopatikana Kenya ikawakama moto

Hoja ni kuwa kama tunaweza kuzuia maafa basi na iwe kuliko kusubiri kuona nyongo zinatumbuka. Siyo CCM wala Wapinzani watakaokuwa salama, ni sote na maafa

Haya yanayoendelea yanapalilia mazingira mazuri si CCM kushinda 100% bali Taifa kutumbukia katika hali tusiotarajia. Tumekuwa na vyama vingi miaka 25! nini kimebadilika leo?
 
Nimependa swali namba 5. Bila kuwa na vijana wenye jeuri hiyo ya "hatutoki mpaka kieleweke" hakuna kitakachobadilika

Nadhani wanakumbukumbu ya yaliyotokea kinondoni 2015. Huyo aliyeunga mkono huenda hata asingetangazwa 2015
 
Kwa aina ya majibu yaliyojaa humu juu ya maswali yaliyoulizwa, ni dhahiri kabisa bado tuna safari ndefu sana

Vijana wasioipenda CCM na wanachama wa vyama pinzani ni kama wanadhani eti CCM haijui kama haipendwi! Yaani wanataka CCM iweke mazingira sawa ya kupimana ubavu! Hiyo HAITOKAA ITOKEE!!

Mleta mada nimependa swali lake la 5, kulikosekana vijana wabishi watakao lianzisha kwa yeyeto atakayekataa kupokea fomu au kuleta mizengwe? Badala yake watu wameporomosha matusi

Ndugu zangu, huu ni uchaguzi wa serikali sio wa viongozi wa serikali ya wanafunzi mashuleni!!!

Mbinu na mikakati ni lazima ipangwe mapema na sio kutegemea kanuni na taratibu tuu!

Kwa hali ilivyo, haiingii akilini chama kubwa kama chadema waingie kwenye battle na CCM bila kuweka plan B!

Lazima wawe na plan B, kwamba kanuni zikikiukwa kiholela na sisi tutafanya haya kiholela! Kama serikali na chama chake wanakiuka taratibu kihuni, lazima wapinzani nao wapange mikakati ya kukabiliana nao kihuni! Hapa mahakama na rufaa zinawekwa kando, mambo yanaendeshwa kihuni!

Haiingii akilini mtaani vijana kibao halafu mpokea fomu au mgawa fomu haonekani ofisini siku ya kwanza, ya pili, ya tatu halafu anaangaliwa tuu! Kwani anaishi mbinguni?

Haiingii akilini kabisa kutegemea Jafo atawatetea wapinzani eti kisa wasimamizi wa uchaguzi walikiuka taratibu!

Anyway, hongera kwa wanabutiama kwa walichofanya angalau wamepoza hasira zao
 
Hivi unadhani babu zetu wangefuata utaratibu kwa kila jambo, wakoloni wangeondoka Afrika? Zimbabwe, Angola, Mozambique vyama vya siasa vilizuiliwa, je wapigania Uhuru walikibali kukaa kimya eti kisa wamezuiliwa kudai Uhuru?
 
..huu uhasama, uadui, na chuki, inayopandikizwa na ccm, watoto wetu watakuja kuishi namna gani?
Just a matter of time , it's not why but when
Yaani chuki imetamalaki nchini , uadui umekuwa sehemu ya utamaduni wetu, tunahasimiana kuliko wakati wowote ule.
 
Sio chadema tu.Ata ACT wamekatwa.Wagambea laki moja naishirini elfu wa ACT wamekatwa wakati wa CCM wamepita wote.
 
Heshima sana mkuu. Hili ndilo ninalosema hapa JF siku zote, na watu hawataki kulisikia, sijui kwa nini.

Sasa hivi hakuna "Chama Cha Mapinduzi,". Hiki alikichukua Mwenyekiti anayefanya maamuzi yote, na hata huko ndani ya chama hakuna tena anayeweza kuhoji.

Ni kama ilivyo serikalini - taasisi zote zinasikiliza Rais anataka nini. Sio Mahakama, sio Bunge, sio Tme ya Uchaguzi , sio Polisi, sio Uhamiaji, n.k., n.k..

Matakwa ya Mweyekiti ni kuua upinzani. Sasa hata huko ndani ya CCM kuna watu wanaoona jambo hilo halifai, hakuna mwenye uthubutu wa kuweka mawazo yake yanayopingana na mawazo ya Mwenyekiti. Hakuna.

Na mbaya zaidi, hata kama wapo humo ndani ya CCM wasiokubali na mambo yanavyokwenda sasa, hakuna mwenye uthubutu wa kusema ajiondoe, akapambanie nje. Wote (wengi) watanung'unikia pembeni tu, huku wakihofia manung'uniko yao yasije yakadukuliwa na kumfikia Mwenyekiti. Wote wanalinda kula yao. Si uliwaona Nape na Makamba, na Mzee Ngoyaye?

Akheri ya Kinana aliyejinyamazia kimya.

Akina Kikwete wanaruka Kimanga, wasifichuliwe madudu yao. Mwinyi ni kama hakuwahi kabisa kuwa Kiongozi wa nchi hii. Huenda akilinda matumaini ya kijana wake.

Nasikitika sana, hata yule Mzee milima viazi, Makamu Mwenyekiti kudhalilika kiasi hiki! Warioba atafanya nini, Butiku atafanya nini ndani ya CCM ya sasa?
 
Yawezekana mzee mwanakijiji uko sawa au la!. najiuliza kama ni kweli Watanzania wanaogombea uongozi serikali za mitaa hawana weledi wa kujaza fomu hizo kwa kiwango kikubwa hivo naingiwa na woga wa elimu itolewayo Tz. Hebu fikiria wagombea hawa wengi ni wahitimu wa elimu ya msingi darasa la 7 na wengine sekondari sasa iweje haya makosa? na si ajabu kuna watumishi wasitaafu ambao pengine ni diploma na degree holders nao wanakosea teh teh teh. waziri wa elimu jitafakari na wizara kwa ujumla.
 
JokaKuu, sijui kama unanipta ninachokisema ambacho sijakisema. CCM haina sababu, lengo, maslahi au hata nia ya kutengeneza mazingira ya kuinua au kuimarisha upinzani ili baadaye upinzani uje kuingia madarakani. Msimamo huu haujaja na Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…