Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #221
Haya yanayoendelea yanapalilia mazingira mazuri si CCM kushinda 100% bali Taifa kutumbukia katika hali tusiotarajia. Tumekuwa na vyama vingi miaka 25! nini kimebadilika leo?
Sasa unakaribia niliko; upinzani ukiendelea kusubiria CCM iwasafishie shamba, iwalimie, iwapandie, halafu iwamwigilie na kuwapililia halafu wao waje na matenga yao kuvuna basi watasubiri sana. Hii hofu ambayo unaisema ni hofu isiyo na msingi. Hakuna mtawala ambaye anapenda kutoka madarakani au atatoka madarakani. Hosni Mubarak, Bin Ali, na wengine wengi waliweza kutawala tu kwa muda mrefu kwa sababu watu walikuwa na hizi hisia za kuogopa kuingiza nchi katika machafuko. Nchi si lazima iingie kwenye machafuko; lakini ikishachafuka kinachofanyika ni kuitoa kwenye machafuko. Nisome unielewe. Kama wapinzani wanaombea sana CCM iwasaidie haya wasubirie; na tutazeeka na watoto wetu watazeeka wote wakisubiria... kumbuka CCM imeshaanza kupitisha uongozi kwa vijana wake (wale ambao miaka 15 nyuma walikuwa chipukizi!).