Pre GE2025 Wazo Jipya: Sema Mambo 3 CHADEMA wafanye sasa kwa Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata kama utaielimisha Polisi lakini kila Askari atakayeitendea haki Chadema atafukuzwa kazi au atauawa, chukua haya maneno yangu.

Hivi Wambura au Kingai wasikie Askari anaitendea haki Chadema unadhani itakuwaje?
 
Kuna moja (wengine wanaweza kuona ni dogo) lakini siyo. i.e. Imefika muda wa mwenyekiti kuachia kiti kwa mtu mwingine. Hili litafanya watanzania wengi kupata morali kwa kuwa na kiongozi mpya ambaye hata kina Msigwa hawawezi kumzushia mambo ya kuzusha. Mbowe ni kiongozi mzuri sana na amefanya mengi mazuri ila sasa hivi amechokwa (hili ni jambo la kawaida kwa kiongozi yoyote anayekaa muda mrefu hata awe mzuri namna gani).
 
Ushauri wako ungekuwa na maana iwapo kungekuwa na uchaguzi wa kweli, sio haya maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
1.chadema wakae pembeni kwa kuwa ccm haitegemei kura za wananchi ili kuingia madarakani,huo ndio uhalisia ata nape aliropoka wazi.
 
🤣 🤣 🤣
 
🤣 🤣 🤣
 
Nimemuambia hataki kuelewa. Ayatollah akishafanya maamuzi kila jambo linawezekana. Mbona Lowassa aliruhusiwa kugombea 2015 bila hata kamati kuu ya chama kufahamu.

Mbowe is the party, and his words are the law.​
🤣 🤣 🤣
 
Unataka tiss waanza kuunsa sheria ya kuzuia app ya whatsapp nchini?
 
Namba 1 ni muhimu sana ila sijui kama katiba ya Chama inasapoti, Maana Katiba ndio mwongozo namba 1, ila nadhani linazungumzika
Still inawezekana kwa sababu sidhani kama kwenye katiba kuna sehemu inayosema kwa mfano "Mgombea wa urais ni Mtanzania yeyote bila kujali amekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa muda gani!" Kukiwa na kifungu kinachosema "bila kujali amekaa CHADEMA kwa muda gani, basi mwongozo wa kuweka muda utakuwa batili lakini kama hawajataja muda, chama kinaweza kuweka mwongozo wa uchaguzi.
 
Bila kusita kabisa, namba 2 na 3; wasipo fanya hivyo watakuwa siyo watu makini. Haya tulisha yashauri; lakini maajabu hata kwenye huu wa serikali za mitaa hawakuwa tayari kiuweka mtu kila sehemu.
Wanajigamba wanao wanachama milioni 15, au sijui milioni 8; hawa watu wote itashindikana vipi kuwapata wagombea wa nafasi zote?

CHADEMA bado wamechanganyikiwa na ule ulaghai wa "mazungumzo ya maridhiano."

Nami nitaweka mapendezo zaidi baadae, hasa kuhusiana na uchafuzi wa kura unaofanywa na CCM wakati wa uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…