Mkuu 'Joka', hili la pesa tulisha lizungumzia sana. Sote tunajuwa CHADEMA haiwezi kuwafikia CCM kwa kiasi cha pesa kilichopo...Ccm wana ruzuku ya bilioni 3.2 kila mwezi.
..mkiwaona Ccm wamenawiri na kutakata na wako kila mtaa mjue chanzo chake ni mabilioni wanayopata ktk ruzuku.
Lakini hii kamwe haiwezi kuwa sababu ya kutofanya hata yanayo wezekana kwa kiasi hicho kidogo kilichopo.
Kuna mambo ambayo pesa haiwezi kuyanunua toka kwa wananchi kwa kiasi chochote cha pesa CCM walicho nacho. Hiyo ni fursa nzuri kwa CHADEMA kuitumia.
Tatizo kubwa linalo wakabili CHADEMA ni hivi vyombo vya dola vinavyo tumiwa na CCM. Hili linaweza kukomeshwa na wananchi walio pania kukataa upumbavu huo. Hawa wananchi wanahitaji uongozi, na kuunganisha nguvu zao kufanya kazi hiyo.