Pre GE2025 Wazo Jipya: Sema Mambo 3 CHADEMA wafanye sasa kwa Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Wazo Jipya: Sema Mambo 3 CHADEMA wafanye sasa kwa Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukiniuliza mimi ntasema mambo yangu matatu; siyo mageni sana lakini naamini yanaweza kuisadia CHADEMA kujiandaa na uchaguzi mkuu mwakani. Na wewe kama unayakwako yaweke labda katika wastani yatapatikana mambo matatu makubwa.

1. Itangaze mapema kama msimamo wa chama kuwa wagombea wote wa ubunge na Urais mwakani watakuwa ni wale waliowahi kuwa ndani ya CHADEMA SI CHINI ya miaka 2.

2. CHADEMA ianze mchakato wa kuhakikisha sera ya mano a mano. Yaani, kila jimbo lazima liwe na mgombea kama mechi ya mpira vile. Hakuna mahali CCM isimamishe CHADEMA ISIWE NA mtu. Wasiache jimbo hata moja lisiwe na mgombea wao.

3. Waandae mawakala pia kwa kila jimbo na kuwatengenezea APP ya kukusanya matokeo (hata kutumia TELEGRAM NA WHATSAPP). Lakini watenge hela za kuwalipa mawakala na waweke mfumo wa kuwalipa. Hakuna kukopa nguvu kazi ya mashabiki.
Unaanzaga vizuri lakini huchelewi kubadili gia angani!🤣😅🤣😅.

Ukiniuliza mimi nitasema CHADEMA waungane tena na wenzao wanaojielewa kulete UKAWA II.
Na wasikubali kushiriki uchaguzi ujao bila Katiba Mpya!
 
Bila kusita kabisa, namba 2 na 3; wasipo fanya hivyo watakuwa siyo watu makini. Haya tulisha yashauri; lakini maajabu hata kwenye huu wa serikali za mitaa hawakuwa tayari kiuweka mtu kila sehemu.
Wanajigamba wanao wanachama milioni 15, au sijui milioni 8; hawa watu wote itashindikana vipi kuwapata wagombea wa nafasi zote?

CHADEMA bado wamechanganyikiwa na ule ulaghai wa "mazungumzo ya maridhiano."

Nami nitaweka mapendezo zaidi baadae, hasa kuhusiana na uchafuzi wa kura unaofanywa na CCM wakati wa uchaguzi.
Biashara kwenye ujasiriasiasa inawayumbisha sana CHADEMA.
 
Namba 1 ni muhimu sana ila sijui kama katiba ya Chama inasapoti, Maana Katiba ndio mwongozo namba 1, ila nadhani linazungumzika
Binafsi naona haina tija sana. Sema katiba ikataze mtu kuacha ubunge na kuhamia chama B kisha kugombea tena nafasi hiyo.

Kama ukiacha ubunge na kuhama chama ukae walau miaka 3 ndiyo upate sifa za kugombea ama kuteuliwa tena nafasi uliyoiacha.

Tutadhibiti zile kenge zinanzonunuliwa kisha kuahidiwa ubunge ama wa kuteuliwa ama kuwekwa tena kugombea.

Namba moja naipinga, acha watu wanaokosa fursa watafute kwingine na kuongeza upinzani zaidi.
 
Bila kusita kabisa, namba 2 na 3; wasipo fanya hivyo watakuwa siyo watu makini. Haya tulisha yashauri; lakini maajabu hata kwenye huu wa serikali za mitaa hawakuwa tayari kiuweka mtu kila sehemu.
Wanajigamba wanao wanachama milioni 15, au sijui milioni 8; hawa watu wote itashindikana vipi kuwapata wagombea wa nafasi zote?

CHADEMA bado wamechanganyikiwa na ule ulaghai wa "mazungumzo ya maridhiano."

Nami nitaweka mapendezo zaidi baadae, hasa kuhusiana na uchafuzi wa kura unaofanywa na CCM wakati wa uchaguzi.
Mbowe is tired. Kuwa mwenyekiti kwa muda wote huo ni lazima watu watakuchoka na wewe kuna mambo mengi utayafanya kama bussiness as usual. Akubali ampe mwingine kijiti na atakumbukwa sana kwa mazuri yake.
 
Ukiniuliza mimi ntasema mambo yangu matatu; siyo mageni sana lakini naamini yanaweza kuisadia CHADEMA kujiandaa na uchaguzi mkuu mwakani. Na wewe kama unayakwako yaweke labda katika wastani yatapatikana mambo matatu makubwa.
Asante, nimefurahi kukuona Mkuu Mzee Mwanakijiji
1. Itangaze mapema kama msimamo wa chama kuwa wagombea wote wa ubunge na Urais mwakani watakuwa ni wale waliowahi kuwa ndani ya CHADEMA SI CHINI ya miaka 2.
Huu ni ubaguzi, kama ubaguzi mwingine wowote
Kunaweza kutokea fresh blood ambao ni serious, loyal and committed, kuliko old guards ambao ni virusi!.
2. CHADEMA ianze mchakato wa kuhakikisha sera ya mano a mano. Yaani, kila jimbo lazima liwe na mgombea kama mechi ya mpira vile. Hakuna mahali CCM isimamishe CHADEMA ISIWE NA mtu. Wasiache jimbo hata moja lisiwe na mgombea wao.
Naunga mkono hoja
3. Waandae mawakala pia kwa kila jimbo na kuwatengenezea APP ya kukusanya matokeo (hata kutumia TELEGRAM NA WHATSAPP).
Naunga mkono hoja
Lakini watenge hela za kuwalipa mawakala na waweke mfumo wa kuwalipa. Hakuna kukopa nguvu kazi ya mashabiki.
Not necessarily kuwalipa, wapenzi wa Chadema at heart wanaweza kujitolea.

Mimi ushauri wangu kwa chadema ni ule ule wa siku zote
1. Changing mindset
2. Reaching out strategies
3. Investing on people
4. Doing real politics
Transformation from chama cha kiharakati into chama tawala in waiting.
P.
 
Asante, nimefurahi kukuona Mkuu Mzee Mwanakijiji

Huu ni ubaguzi, kama ubaguzi mwingine wowote
Kunaweza kutokea fresh blood ambao ni serious, loyal and committed, kuliko old guards ambao ni virusi!.

Naunga mkono hoja

Naunga mkono hoja

Not necessarily kuwalipa, wapenzi wa Chadema at heart wanaweza kujitolea.

Mimi ushauri wangu kwa chadema ni ule ule wa siku zote
1. Changing mindset
2. Reaching out strategies
3. Investing on people
4. Doing real politics
Transformation from chama cha kiharakati into chama tawala in waiting.
P.
Sasa hivi hayo yote ya kusambaza nguvu bila manufaa ni ya nini. Kazi ya kwanza na ya pili hadi ya tatu ni kuwaondoa CCM kwenye madaraka wanayo shikilia kwa mabavu.

Kwa hiyo 'strategy'/mkakati namba moja, namba mbili na namba tatu ni kuhusu ajenda hiyo kabla ya mengine yote

Wakisha waondoa CCM, waanze hizo kazi zingine ambazo wakionekana hawana uwezo nazo, na wao waondolewe mara moja.

Lakini kazi ya kuwadhibiti 'watekaji' (CCM) hiyo ni ajenda tosha kabisa inayo eleweka kwa wananchi sasa hivi.
 
Nilivyosoma hapo juu nimejiuliza swali moja; CHADEMA bila migongano na mivutano ya ndani inawezekana? Ni kama kila wanapoelekea uchaguzi wa ndani au uchaguzi mkuu kunakuwa na hii mivutano.
 
..changamoto nadhani iko ktk uwezo wao wa fedha, na vifaa, kufanya kampeni ya nguvu nchi nzima.

..pia kuwa na chombo cha habari ambacho kiko loyal kwao na kitawatangaza kwa nguvu zilezile zinazotumika kutangaza Ccm.

..jambo lingine wabadilishe ujumbe wao kwa vyombo vya dola. Waache kuvizomea, badala yake wavielimishe, na kuvinasihi, ktk kutenda haki.

..ndani ya vyombo vya dola kuna watu wanapenda haki. Sasa Chadema ielekeze ujumbe kwa kundi hilo.
Hili suala la uwezo nalo linafikiriksha; ni kweli hadi leo CHADEMA hawana kitega uchumi? Yaani, kama ruzuku zikisimamishwa CHADEMA haiwezi kusimama? Mbona wanawezaga kuchangisha wanachama wao kwa mambo mengine mengi tu. Chama kinachoongozwa na mfanyabiashara si kingejipanga kibiashara? Hili linahusishsa hata vyombo vya habari. Nakumbuka kuna wakati walikuwa na tovuti yao sijui kama bado ipo au ilipotelea wapi.
 
Yote uliyopendekeza hapa, kasora hilo la kwanza yalifanywa na CHADEMA kuelekea 2015. Waliunda UKAWA na kila jimbo likawa na mgombea, walitumia wataalamu wa TEHAMA kutoka nje kusaidia mawakala, ila serikali ya CCM ikatumia mabavu.​
Umesahau kuwa UKAWA iligeuka UKIWA? Ulikuwa ni muungano mbovu zaidi wa vyama vya upinzani kuwahi kutokea Afrika kama siyo duniani.
 
Bila kusita kabisa, namba 2 na 3; wasipo fanya hivyo watakuwa siyo watu makini. Haya tulisha yashauri; lakini maajabu hata kwenye huu wa serikali za mitaa hawakuwa tayari kiuweka mtu kila sehemu.
Wanajigamba wanao wanachama milioni 15, au sijui milioni 8; hawa watu wote itashindikana vipi kuwapata wagombea wa nafasi zote?

CHADEMA bado wamechanganyikiwa na ule ulaghai wa "mazungumzo ya maridhiano."

Nami nitaweka mapendezo zaidi baadae, hasa kuhusiana na uchafuzi wa kura unaofanywa na CCM wakati wa uchaguzi.
Kalamu, haya ni marudio tu huwa tunarudia rudia lakini ni kwa sababu binafsi sioni kama kweli wanataka kujipanga kushinda; wao wanapenda kushiriki uchaguzi siyo kushinda uchaguzi.
 
Maoni yangu katika kuwashauri CHADEMA wakati tukielekea kwenye chaguzi zifuatazo siyo mageni, kwani yamerudiwa rudiwa mara kadhaa humu humu JF tokea 2020.

Baada ya kutofanya lolote la maana tokea wakati ule, kwa sababu walilazwa akili kwa hadaa na ulaghai wa "mazungumzo ya maridhiano", sasa wamejikuta CCM ndio inakaza kamba zaidi kuvuruga uchaguzi ili waendelee kubaki madarakani.
Mazingaombwe ya "Tume Huru", wakati haiko huru kwa lolote isipokuwa jina; sheria ya uchaguzi iliyo wekwa na mengi mengine yaliyofanywa na serikali ya CCM yanalengo moja tu ya kuibakisha CCM madarakani kwa njia yoyote iwezekanayo; hata kwa kuondoa roho za watu.

Huu uchafuzi wa Serikali za Mitaa unaonyesha wazi, bila kificho, kwamba ni maandalizi ya CCM kuvuruga ule wa 2025.

Kwa hiyo, ushauri ninao wapa CHADEMA ni wao pia kufanya kila watakalo weza katika hali iliyopo sasa hivi kujiandaa kwa uchafuzi wa 2025.
Wakati ni sasa, kuweka mipango ya kuzuia "UHALIFU" unaopangwa na CCM kwenye uchaguzi huo.

Kujiandaa ni kujua mbinu zinazo tegemewa kufanywa ili kuvuruga uchaguzi. Wakisha juwa mbinu hizo, kazi inageukia kutafuta njia za kuzuia uhalifu.

Kazi kubwa ya uhalifu inaanzia huko huko mitaani; kwenye vituo vya kupigia kura na kuhesabu kura hizo. Huku ni lazima CHADEMA wajipange vizuri kukabili hali hiyo; na iwe hivyo hivyo katika ngazi zinazo fuata sehemu zote kunakopitia kura hizo.

Sasa basi, kazi hii inahitaji watu walio andaliwa vizuri na watu ambao imani yao kwa chama chao haiteteleki.
Watu hawa ni lazima, muhimu kabisa wapatikane kuanzia sasa. Lisiwe tena jambo la kubahatisha dakika za mwisho mwisho wakati uchaguzi umeingia.

Hawa watu ni lazima wawe ni wana chama waaminifu, walio funzwa vizuri na chama chao mbinu za kuhadaiwa kwa fedha, au vitisho visivyo zingatia sheria.

Udhaifu mkubwa wa CHADEMA upo kwenye kutojuwa kutumia raslimali yao muhimu kabisa ya wanachama wao, na wapenzi wa chama hicho. Hili linatakiwa kufanyiwa kazi haraka. Chama ni lazima kitumie raslimali yao muhimu wakati huu. Kama chama kina wanachama hai milioni 5; hawa ni lazima wawe ni wanachama wanaoiona CHADEMA kuwa na maana katika maisha yao na wawe tayari kukipigania chama chao kwa dhati kabisa. Isibakie tu, kuwaona kwenye nyomi za mikutano ya hadhara ya chama, na baada ya hapo hata kura hawapigi. Ni lazima viongozi wa CHADEMA wajiulize maswali magumu kuhusu wana chama wao hawa.
 
Hata kama utaielimisha Polisi lakini kila Askari atakayeitendea haki Chadema atafukuzwa kazi au atauawa, chukua haya maneno yangu.

Hivi Wambura au Kingai wasikie Askari anaitendea haki Chadema unadhani itakuwaje?
PoliCCM

IMG_0200-4234671364.jpg
 
Kalamu, haya ni marudio tu huwa tunarudia rudia lakini ni kwa sababu binafsi sioni kama kweli wanataka kujipanga kushinda; wao wanapenda kushiriki uchaguzi siyo kushinda uchaguzi.

Kilicho nishangaza hivi karibuni ni kumsikia Tundu Lissu akikiri kwamba chama hakina uwezo wa kuweka wagombea kila mtaa; kwa vile hawana pesa za kufanya hivyo!
Tuliwashauri tokea zamani kabisa kwamba kuiga muundo wa CCM ilivyo tapakaa pote huko mitaani siyo kosa, na sidhani kwamba CCM hutumia hela nyingi kwa kazi hiyo. Na hasa ukichukulia urahisi wa mawasiliano ulivyo siku hizi.

Kama wanaweza kukodisha chopa wiki nzima, kweli chama kitashindwa kufanya mawasiliano na viongozi wake wa ngazi za chini kabisa, angalau mara moja kwa mwezi? Hizi simu zipo kwa kazi zipi hasa!
Hapana. Ingekuwa hivyo, wasinge endelea kuwemo kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa wakati wakijuwa watu wao wengi wameondolewa. Bila shaka wanazo sababu za kuwafanya waendelee kuwemo kwenye mchakato, pamoja na kwamba hawana njia ya kushinda viti vingi. Nami nawaunga mkono kwa hilo; kwa sababu moja kuu, kwamba uchaguzi huu wa serikali za mitaa uwe ni mazoezi muhimu yatakayo waa elimu ya kutosha na mbinu za kuzuia uonevu hao 2025.
 
Hili suala la uwezo nalo linafikiriksha; ni kweli hadi leo CHADEMA hawana kitega uchumi? Yaani, kama ruzuku zikisimamishwa CHADEMA haiwezi kusimama? Mbona wanawezaga kuchangisha wanachama wao kwa mambo mengine mengi tu. Chama kinachoongozwa na mfanyabiashara si kingejipanga kibiashara? Hili linahusishsa hata vyombo vya habari. Nakumbuka kuna wakati walikuwa na tovuti yao sijui kama bado ipo au ilipotelea wapi.

..wangekuwa na kitega uchumi Magufuli angekiharibu.

..upinzani ni kama wameanza upya kutokana na unyama na ukatili uliotokea kati ya 2016 na 2020.
 
Kilicho nishangaza hivi karibuni ni kumsikia Tundu Lissu akikiri kwamba chama hakina uwezo wa kuweka wagombea kila mtaa; kwa vile hawana pesa za kufanya hivyo!
Tuliwashauri tokea zamani kabisa kwamba kuiga muundo wa CCM ilivyo tapakaa pote huko mitaani siyo kosa, na sidhani kwamba CCM hutumia hela nyingi kwa kazi hiyo. Na hasa ukichukulia urahisi wa mawasiliano ulivyo siku hizi.

Kama wanaweza kukodisha chopa wiki nzima, kweli chama kitashindwa kufanya mawasiliano na viongozi wake wa ngazi za chini kabisa, angalau mara moja kwa mwezi? Hizi simu zipo kwa kazi zipi hasa!
Hapana. Ingekuwa hivyo, wasinge endelea kuwemo kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa wakati wakijuwa watu wao wengi wameondolewa. Bila shaka wanazo sababu za kuwafanya waendelee kuwemo kwenye mchakato, pamoja na kwamba hawana njia ya kushinda viti vingi. Nami nawaunga mkono kwa hilo; kwa sababu moja kuu, kwamba uchaguzi huu wa serikali za mitaa uwe ni mazoezi muhimu yatakayo waa elimu ya kutosha na mbinu za kuzuia uonevu hao 2025.

..Ccm wana ruzuku ya bilioni 3.2 kila mwezi.

..mkiwaona Ccm wamenawiri na kutakata na wako kila mtaa mjue chanzo chake ni mabilioni wanayopata ktk ruzuku.
 
Back
Top Bottom