Wazo la kufungua barabara ya Makambako to Mlimba

Huyo ni mbunge wao akielezea mafanikio hapo tumechukulia reference ya upembuzi wa Barabara ya makambako hadi MGOLOLO
 
Ile Barabara imejengwa na mradi Agri connect km 40 hadi lulanda na Ile itaenda hadi mlimba kwa Sasa wamepewa km 40 kutoka nyororo hadi mtwango zitaenda kuungana na hiyo na bado ya ifwagi nayo inawekwa lami kupitia mradi wa RISE
 
Ile Barabara imejengwa na mradi Agri connect km 40 hadi lulanda na Ile itaenda hadi mlimbaView attachment 2972436View attachment 2972439
Sasa barabara za aina hii zinashindwa vipi kujengwa kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara? Mfano kutoka Ifakara kwenda Mlimba, Ifakara kwenda Mahenge na Malinyi, Nyololo Mgololo, nk!!

Washauri viongozi wako waache mambo ya hovyo. Hii mifumuko ya bei ya vyakuka na bidhaa nyingine, wakati mwingine wanajitakia tu wenyewe.
 
kweli aisee ifakara mlimba,ifakara mahenge,mlimba malinyi,mlimba njombe,mahenge lindi,mlimba mafinga na malinyi songea ni barabara muhimu sana ila viongozi wanakomaa na kujenga vitu vya ajabu ili wapige madili
 

Wazo zuri ila mradi wa Agri connect wamejenga maeneo ya uzalishaji wa mazao ya biashara hasa chai ,kahawa
 
Wakina JAH PEOPLE nao wamezubaa, barabara na reli ya Makambako ni ya kwanza (T001) nchi hii lakini sioni maendeleo ya maana.
 
MALORI 25 YAKWAMA BARABARA YA MGOLOLO-MAKAMBAKO

Zaidi ya magari ya mizigo 25 ambayo yanasafirisha bidhaa mbalimbali kutoka kiwanda cha karatasi Mgololo wilaya Mufindi mkoani Iringa yamekwamba kwa zaidi ya siku tano katikati ya vijiji vya Nyamande na Kitandiliko halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe kutokana na ubovu wa barabara katika eneo hilo.

Wakizungumza na radio one madereva wa magari hayo akiwemo Godwin Ngajilo na Jumanne Hussen wamesema changamoto kubwa katika eneo hilo inatokana na aina ya kifusikisicho na changarawe kilichowekwa na mkandarasi ambacho kimesababisha Barabara hiyo kutopitika kutokana na uwingi wa matope kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Wakizungumzia umhimu wa Barabara hiyo wamesema barabara hiyo inatumiwa na nchi zaidi ya tano ikiwemo Kenye,Uganda ,Burundi na Zambia ambazo zinategemea karatasi kutoka kiwanda cha Mgogolo na kwamba kwamba jitihada za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa.

Aidha madereva hao wamesema kutokana na adha hiyo kumesababisha watumie gharama kubwa kwaajili ya kupata chakula na kueleza kuwa mpaka sasa hakuna hakuna jitihada zinazoendelea kwaajili ya kunusuru hali hiyo .

Nao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kitandililo akiwemo Obedi Msingwa na diwani wa kata hiyo bwana Imani fute wamesema kutokana na barabara hiyo kutopitaka kwa zaidi ya siku tano kumesababisha abiria wanaotoka vijiji vya wilaya ya mufindi kuishia kitandililo na kutafuta usafiri mwingine ili kufika mjini mkambako huku wengine wanalazimika kutembea miguu

Kwa njia ya simu meneja wa Tanroad mkoa wa Iringa Yudas Msangi amekiri kupokea changamoto hiyo na kuahidi kutaftia ufumbuzi haraka na kueleza kuwa barabara hiyo itafanywia marekebisho pindi mvua zitakapo bada ya kufanyiwa usanifu

mwandishi Njombe
0766880828
 
Nimetumwa na nani Hilo ni wazo Sasa kutumika kunakujaje tatizo mnaingiza siasa kwenye mambo ambayo haya husiani
Wewe ndiyo umeingiza Siasa kwa kuanza kumsifia Rais Samia unayemwita mama.

Au Samia siyo mwanasiasa toka CCM??
 
Wakina JAH PEOPLE nao wamezubaa, barabara na reli ya Makambako ni ya kwanza (T001) nchi hii lakini sioni maendeleo ya maana.
HApo ndo inatakiwa upeleke wazo ila wenzio kama mkoa wamefikiria haya kuwa na dry Port viwanda na biasharaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema mji wa Makambako ni lango la biashara na anaufananisha mji huo kama ulivyo mji wa Mkuranga mkoani Pwani ambao una viwanda vingi.

Mtaka amesema hayo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makambako mkoani Njombe.

Mtaka ameongeza kuwa, wao kama mkoa wana mipango ya kuifanya Makambako kuwa mji wa viwanda na tayari wameanza ujenzi wa kiwanda cha chuma na hivyo wananchi mkoani humo hawatapata tena adha ya kufuata chuma mkoani Dar es Salaam.

Pia wana mpango wa kuongeza thamani ya zao la Parachichi ambalo linalimwa sana mkoani humo.

Aidha, Mtaka ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kuwaelekeza wananchi namna nzuri ya ulipaji kodi bila bughudha na hivyo kuwataka wafanyabiashara mkoani humo kufanya shughuli zao kwa utulivu.
 

Attachments

  • 1713453839758.jpg
    166.4 KB · Views: 3
Mimi binafsi nakubaliana na mleta mada kabisa tunapashwa kuzitengeneza njia nyingi zinazoiunganisha Nchi pande zote hiyo ndio njia mojawapo nzuri ya kuleta maendeleo ya ndani ya Nchi. Kuto kuzijenga itakuwa sawa sawa na kile wanachokipata DRC maana upande mmoja hakutani na mwingine kwa urahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…