Wazo: WanaJF naomba tufanye shukrani kwa Mungu ya kufunga na kufungia mwaka kwa kutoa msaada kwa wahitaji

Raynavero

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
38,378
Reaction score
56,047
Hey brothers and sisters nilikua na wazo kwa kua tuko mwishoni mwa mwaka na tunaanza 2020 naomba tutoe shukrani kwa Mungu kwa kurudisha tulichokipata hata km kidogo kwa mwaka mzima na huku tukiwa mbioni kuanza mwaka mwingine.

Kuna mengi tumepitia makubwa na madogo, shida na raha lakini Mungu hakutuacha. Kuna tuliopitia mitihani miingi mizito na wapo waliopitia tambarare mwaka wote lakini Mungu wetu mwema tumeweza kuwa na afya na hata wagonjwa pia Mungu awaponye, na wale wenye mitihani pia Mungu awavushe salama.

Nilikuwa na wazo kuwa tutoe msaada kwenye vituo au tuchague kimoja tupeleke misaaada yetu hasa mwanzo wa mwaka hapa mahitaji yao makubwa ni uniform mabegi na madaftari ya shule n.k

Kwa yoyote ambaye ataguswa tunaweza tuma pesa halafu vikanunuliwa kwa jumla au mtu kama anavyo akagaia au akannua hayo mahitaji then tukayapeleka sehemu husika siku tutakayopanga.

Mniwie radhi I know watu wana magroup mengi ya familia n.k, na wamepeleka misaada mingi sehemu nyingi lakini sisi wanaJF pia kama familia moja tunaweza tukafanya pia kama tulivofanya huko kwingine.

Anaweza chagulia mtu au hata mods ambaye anaaminika kufanya hyo kazi ya kukusanya pesa n.k Niko tayari kushirikiana 100% maana Mungu ametutendea miujiza mingi mnoo hatuna cha kumlipa zaidi ya kurudisha shukrani kwake. Jf Ni ndugu sote ingawa si wa kuzaliwa na Mungu anasema toa ili nikuruzuku.

Tafadhali naomba wale wenye mawazo mgando hapa wapite tu.
Tukikubaliana tutaweka utaratibu mzuri wa kutoa sadaka zetu.

Ahsanteni na mnisamehe ntakaowaboa pia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilisemaga humu ndani tungekuwa na utaratibu kwa mwaka mara 2 au 3 kuwasaidia wahitaji.

Wengine tunao humu humu wala hakuna hata haja ya kwenda nje Mshanajr embu njoo hapa.

Mtu amepooza, anaishi kijijini kwao yeye ndo alikuwa tegemeo asome amalize udaktari awaokoe wazazi wake lakini ndoto zikaishia njiani yeye sasa hivi ndo anasaidiwa na wazazi tena hali duni inapelekea hata matibabu akose.

Huyu ni wa humu humu ndani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aaseehhh!nani huyo daahhh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni huzuni sana yarrabi daah
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma hii hapa Mpwa ikutie nguvu, hao anti--social walikuepo Ever since kwahio piga kazi twende tena
Thank you barikiwa kwa hilo twaweza Fanya tena

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana bro we can do it again ngoja wadau waje tujadili tunalifanyaje
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…