1. jipange akajifungulie private hospital.
2. Tafuta mtu/ndugu au mfanyakazi wa kukusaidia kipindi akiwa amejifungua.
3. Elimu kuhusu afya ya mtoto, kunyonyesha, kubeba, viasharia vya hatari mtapewa na nesi hivyo uzingatie sana.
4. Andaa vya kujifungulia kama sanitary pad, vitenge/Kanga, wipes, babyshoes, mpira wa kujifungulia, Pampers, nguo za mtoto, nk.
5. Andaa pesa ya dharura na kadi zake za klini ukumbuke kwenda nazo.
6. Andaa usafiri wa kumpeleka na kumtoa hospitalini iwe bajaji au gari.
7. Mfanyishe mazoezi hasa kutembea na mengine mepesi yatamsaidia sana wakati wa kujifungua.