Wazoefu nipeni ABC Niko pekeangu na wife anakaribia kujifungua

Wazoefu nipeni ABC Niko pekeangu na wife anakaribia kujifungua

Pole Sana mkuu, maumivu yako ni mazito
daaah alikuwaga na tatzo la kupungukiwa damu awamu ya kwanza alitoboa bt ilipotokea mara ya pili tukampeleka muhimbili sjui ilikuaje mama ake anasema walimuwekea damu mara ghafla wakaichomoa, akavimba macho sku yalipopungua nadhan kesho yake alifariki naumia sn sn jaman mtoto wng success daaah.
 
Mkuu nilichelewa kuomba ushauri ila kwa saivi nikijifanya asafiri basi anaweza kujifungua akiwa safarini so nilidhani ni easy ila now Kuna wasiwasi unanijia
gharamia usafiri wa ndugu aidha kutoka kwenu au kwao ili aweze kuhudumiwa kwa karibu.
 
Hata usihofu mimi nlishatoboa mara 2 bila kuwa na mtu mwngn ni mimi na mwanamke wng tu thanks GOD ALITUTETEA bt nasikitika sn mtoto mmojawapo alishafariki akiwa ameshakuwa na miaka 2 mpk leo naumia sn KWAHERI SUCCESS MUNGU AZIDI KUWA NAWE HUKO ULIKO still baba yako ninakukumbuka sn nisamehe nlipowahi kukukosea kama baba yako byeeee.
Alipata changamoto gani mkuu?
 
daaah alikuwaga na tatzo la kupungukiwa damu awamu ya kwanza alitoboa bt ilipotokea mara ya pili tukampeleka muhimbili sjui ilikuaje mama ake anasema walimuwekea damu mara ghafla wakaichomoa, akavimba macho sku yalipopungua nadhan kesho yake alifariki naumia sn sn jaman mtoto wng success daaah.
Too painful to endure! Mungu pekee akupe faraja Yake ya kweli
 
Hello wanaume wenzangu na wanawake wenye uzoefu na labour naombeni ABC za kumuhudumia mke wangu muda wowote anajifungua na nipo mikoa ya mbali na mikoa ya nyumbani sina experience yoyote Wala ndugu mwingine ni mimi na wife tu

Kama Kuna dondoo nisaidieni ndugu zanguni nipate namna nzuri ya kumsaidia wife

Huu ni utakuwa uzao wa pili maana mara ya kwanza alienda kujifungulia kwao..
Majirani na marafiki au ndugu wa kike wa mkeo si wapo?

Tafuta usafiri
 
Tafuta mtu wa kukaa naye hutoweza kumhudumia peke yako mtafute ndugu wa kike yeyote mtu mzima umlete huko kwa muda mpaka akijifungua akiweza kujitegemea fanya mapema sana ndani ya wiki ya kesho uwe umempata
 
Usiogope kikubwa Andaa pesa
Usafiri wa uhakika,
Kama ni mdau wa bima na sehemu uliyopo ina hospital kubwa ya private mpeleke huko Ili kuepuka usumbufu wa leta Mara dishi,Mara kifaa Fulani na kama utampeleka government hospital hakikisha umenunua vifaa vya kujifungulia vilivyo kamili,Andaa vitenge vya Kutosha na kanga,mkifika hospital kama ni serikalini mkeo akienda wodini usiende mbali Kwa Ajili ya ufuatiliaji mwambie kabisa mkeo kuwa nitakuwa sehemu Fulani yeye ni rahisi kama anajiamini kumuomba Hata nesi kwamba aje sehemu uliyopo akuambie mawili matatu.Chupa ya chai uwe nayo uchungu ukimuanza chemsha chai ya rangi muandalie na kikombe atatakiwa anywe na hakikisha unavyomsindikiza umeshika wewe mpeleke Mpaka Kwa manesi wake
Andaa hotpot tembea nalo akijifungua ndani ya hospital baadhi Huwa wanauza mtori kamnunulie wakutosha mpeleke.baada ya hapo kimbia nyumbani Kanunue nyama au chinja kuku chemsha pamoja na ndizi bukoba Zile laini, soap ya Kutosha pamoja na nyama akila atapata nguvu lakini pia maziwa Kwa Ajili ya mtoto .mtori utamnunulia Baada ya kujifungua ndio utapeleka
 
Hello wanaume wenzangu na wanawake wenye uzoefu na labour naombeni ABC za kumuhudumia mke wangu muda wowote anajifungua na nipo mikoa ya mbali na mikoa ya nyumbani sina experience yoyote Wala ndugu mwingine ni mimi na wife tu

Kama Kuna dondoo nisaidieni ndugu zanguni nipate namna nzuri ya kumsaidia wife

Huu ni utakuwa uzao wa pili maana mara ya kwanza alienda kujifungulia kwao..

Ilikuwa ngumu sana kwangu maana sikuambiwa:

1. Kuwa Bennet sana na mke wako, na kila kitu kinachohusu Hospital, tafuta majibu mbadala kwa watu, mfano: Mtoto ajageuka tungoje week Moja mbale - kauli kama hizi za Hospital, uliza watu wengine mawaza au Hospital 2, 3 tofauti.

2. Usiwe mbinafsi, mtoto anapozaliwa, Mama kqpambana miezi 9, akizaliwa kuwa super very supportive; usiku msaidie kumbeba mtoto na yeye alale, be there, kama hajawa tayari ku sex, msubiri mwenzako.

3. Tegemea mabadiliko kwa huyo mwanamke ya mwili wake na life style, anaweza asiwe ana meet expectations zako kama zamani, anaweza kuwa rough kidogo, mwenye harufu kidogo, analala zaidi, anadeka zaidi, mchukuliale.
 
Hello wanaume wenzangu na wanawake wenye uzoefu na labour naombeni ABC za kumuhudumia mke wangu muda wowote anajifungua na nipo mikoa ya mbali na mikoa ya nyumbani sina experience yoyote Wala ndugu mwingine ni mimi na wife tu

Kama Kuna dondoo nisaidieni ndugu zanguni nipate namna nzuri ya kumsaidia wife

Huu ni utakuwa uzao wa pili maana mara ya kwanza alienda kujifungulia kwao..
Kama una mishe za kutoka asubuhi kurudi usiku na ww ndo tegemeo kubwa hapo maskani kwa kila kitu fanya uagizie dada yako aje akae nae hapo au ndugu yake wa kike ambae ni matured...

Usaidizi na uangalizi wa mama mwenye mtoto alietoka kujifungua recently unahitaji zaidi ya mtu mmoja na reliability and availability yake iwe ya uhakika.. Sabu watoto wachanga wana heka heka sana unaweza kuta kanalia sana muda wote so kama hujazoea ww unaweza ukaona kero na kua bored muda wote lakini ni nature tu ya watoto baadhi lakini sio wote.

Kingine hakikisha mkeo unamjali kwa kununua vyakula vya lishe kwa maana mtoto anategemea lishe kutoka kwa mama yake (Maziwa) so mbogamboga za majani, samaki, matunda hakikisha havikosi maskani ukitoka mishe mishe.. Pia msimu wa mvua mvua huu wanunulie mablanket mazito baridi lisiwasumbue, na net pia nzuri imara sio zile za kuchanwa hata na kidole cha mtoto na iwe na matundu madogo sana maana mbu wengi sana, ni hayo tu baba kijacho mtalajiwa..
 
Kwangu ilikuwa uzoefu mzuri ambao kwa kweli niliufurahia. Ingawaje ilikuwa changamoto kutokana ndio mara ya Kwanza.
Nilikuwa pekeangu na Mke wangu. Kuanzia dakika ya Kwanza ya Mimba Mpaka ya mwisho. Bahati nzuri Mimba ya Mke wangu ilikuwa na masharti mengi kutoka kwa Wataalamu wa afya. Alipewa bedrest kwa miezi yote Tisa. Hivyo show zima nilikuwa naipiga mwenyewe.

Kwa kifupi

1. Andaa pesa ya uzazi. Itakayoenda zaidi ya siku 30-40. Ikiwa kuanzia Laki tano upo kwenye Nafasi nzuri.

2. Andaa pesa ya dharura za uzazi hata kama Una Bima. Mambo ya uzazi kuna emergency nyingi.

3. Kama unafriji na majiko ya kisasa kama ya gesi na pressure cooker. Hautapata shida Sana.

4. Kama hauna Mfanyakazi, ANDAA elfu Saba kila siku kwa Mfanyakazi WA kuja na kuondoka kwa hizo siku 40.
Akusaidie kupika, kuosha vyombo, KUFUA n.k.
Ila kama Kazi zako ni nyumbani kama Mimi unapiga Mzigo mwenyewe tuu. Sio tatizo.
Ni Kazi rahisi Sana hasa kama Mkeo unampenda na ulijiandaa

5. Anza Kufuatilia lishe ya Mama mzazi ambayo itamfanya maziwa yatoke Mengi na Mkeo akila awe na afya nzuri
Sio akondeane kana kwamba kuzaa ni ugonjwa

6. Jiandae kuvaa nguo za Ubaba zenye heshima ya Ubaba.
Pia mkeo mnunulie nguo nzuri ili mkitoka wote kwenda Kliniki mambo yawe mazuri. Ufurahie maisha.

7. Ratiba yenu jaribu kuipanga upya. Sasa Mnaenda kuanzisha familia. Mambo ya kuishi kisela kama ghetto yanaenda Kukoma.
Sasa wewe ni Baba, Mkeo ni mama na mtoto anakuja. Sheria, ratiba na miongozo lazima ibadilike.

8. Hakikisha mazingira yanakuwa Safi kumsapoti mtoto. Mtoto mchanga hataki eneo lenye vumbi, baridi na lenye Mbu.
Muda wote mtoto kama hujambeba akae ndani ya neti .

9. Mkeo awe Safi hasa wakati anamnyonyesha mtoto.
Kabla hajamnyonyesha aoshe maziwa yake na maji Safi yaliyo chemshwa.
Hii itamuepusha mtoto Kula uchafu iwe ni jasho au uchafu mwingine katika nyonyo la Mama.

10. Mtoto akinyonya lazima mhakikishe ameshiba. Na akishiba lazima mum-bump, abeue kwa kumbeba begani au kumlaza mapajani.
Hii itamuondolea gesi tumboni na hatakuwa analialia hovyo.
Yaani malezi yanaenda smooth mtoto hataumwa.

11. Mtoto anyonyeshwe kila baada ya saa moja unusu au saa Mbili.

12. Mtoto anyonye maziwa tuu usimpe kitu chochote hata Kwa miezi yote sita.

14. Mkeo mlishe vyakula vyenye virutubisho na vyenye kuongeza damu.

15. Mtoto akifikisha miezi sita Anza kumkorogea Uji mwepesi, supu, na maziwa mengine kama ha Ng'ombe.

16. Mtoto asikae na uchafu hata kwa dakika kumi. Akikojoa au kunya mbadilishe mara Moja.

17. Muogeshe mtoto kwa sabuni maalumu isiyo na kemikali. Maji yawe vuguvugu.

18. Nguo za mtoto zifuliwe kwa Dettol au sabuni yoyote maalumu ya kuulia bacteria

19. Usianike nguo za watoto kwenye kamba za watu wazima wengine.
Mtoto anaweza Kupata Magonjwa ya ngozi. Hii itamaanisha pia uwe na begi la kuwekea nguo za mtoto

20. Nguo za mtoto zipigwe Pasi.

21. Mtoto akifikisha siku 36 Mpaka 40 umtoe Nje kila asubuhi apigwe na Jua na asubuhi na azoea hali ya hewa ya Nje.

22. Muda wote mtoto mvalishe kofia kichwani na soksi miguuni.

23. Usigombane gombane na Mkeo. Mood yenu inaathiri mood ya mtoto.
Mkiwa na Amani na utulivu kwenye familia yenu mtoto hata Magonjwa hukimbia.
Kumbuka mtoto husikia na kuhisi mood zenu. Na Magonjwa Mengi hutokana na mambo ya kisaikolojia zaidi kuliko mazingira.

24. Usimpe Dawa zozote za kienyeji mtoto Nje ya maelekezo ya madaktari WA watoto.

25. Usilete Mila na kijinga kwa Mtoto wako.

Ukifanya hivyo malezi utaona kama anakunywa UJI. Utatamani uzae kama hao Kumi.
 
Back
Top Bottom