Wazoefu wa hii njia: Nina safari ya Dar - Kahama, sasa Nina Maswali hapa Msaada

Ufike manyoni uende itigi alafu uende tabora then urudi nzega ili uitafute kahama? Mzunguko utakua mkubwa kuliko kunyooka moja Kwa moja kutoka manyoni kwenda kahama
Mtu anataka kutalii siyo kuwahi kufika Kahama Chief.

NB:Tabora-Nzega hakuna kabisa magari unaweza kusinzia kwenye usukani japo hiyo lami siyo smooth ila hakuna hata shimo njia nzima.
 
Mimi naanzia kahama
Kahama➡️Masumbwe➡️Ushirombo➡️Runzewe➡️Bwanga➡️Chato

Ukifika chato ndiyo unarudi tena
Bwanga➡️Katoro➡️Geita➡️ Sengerema ➡️Mwanza

Hapo hautagusa vumbi hata kidogo
Ukifika Geita nicheki mzee
 
Poa masta, Geita nadhani nitalala maana kazi ni vituo viwili.
 
 
Naomba kupata maelezo kuhusu gari hilo Honda Fit. Uzuri na changamoto zake.
 
Pale Manyoni njia panda wewe nyoosha Singida, Igunga, Nzega, Tinde, Kahama. Achana na kupita Tabora vinginevyo uwe unaenda Kigoma.
Pale Nzega kuna Nzega=>Kagongwa=>Kahama ni vumbi achana nayo piga Nzega-Tinde.

Kahama, Masumbwe, Ushirombo, Katoro ni mwake mwake. unaweza pitia Kahama Kakola pia.
 
Chukua ramani hii! Ukifika Manyoni chepuka kushoto utafute Tabora, Nzega, Tinde, Isaka, Simba Kagongwa tena halafu Kahama. Ukimaliza kazi zako hapo Kahama nyooka kwenda Chato kupitia Biharamulo zuga zuga hapo kidogo halafu pitia pori la Burigi kula utalii hapo njiani. Nenda mpaka Kyamyorwa kunja kulia kuitafuta Chato. Lala hapo, au kama huna issue hapo nenda ukalale Katoro. Kesho yake shika barabara kwenda Geita fanya mambo yako hapo baadaye nyooka kwenda Sengerema - Busisi ukaone daraja la Magufuli, ukifika Usagara chepuka kushoto uitafute Mwanza, lala hapo ili kesho yake uanze safari ya Dar kupitia Shinyanga, Nzega, Igunga, Shelui, Singida, Manyoni, n.k
 
Hiyo budget ya mafuta hiyo chuma ni Hybrid!? If not i assume kwa makadirio ya juu kabisa (cc1300 hiyo si ndio?) itakuwa inakula 21 km per 1 litre, jumla una km 2,700÷21=128.6km kwa hiyo jumla itakupa 128.6km× 3900sh (makadirio ya bei kwa lita)=504,128.6 sh (kuna issue za elevation, barabara mbovu na na bei ya mafuta mkoani huwa inaongezeka kidogo) hapo ongeza akiba ya 100,000 sh just incase (kama ni hybrid utatoboa)

Lala Singida.. kama utatoka mapema asubuhi ukitembea kistaarabu)/kama babu na kwa kuzingatia 50 kph, Singida unaingia kwenye saa 11-12 jioni kilometa 700 hizo
 
Shukrani mkuu. Ni hybrid ndio. Highway uwa inacheza 30 km/L kwenda juu.

Hii ndio latest trip. Ngoja tuone.
 
Hii nzuri sana. Njia nzima si mkeka hamna vumbi?
 
Naomba kupata maelezo kuhusu gari hilo Honda Fit. Uzuri na changamoto zake.
Mi naenda nacho nautafuta mwaka wa pili, Hakina shida. Pia, Kuna wadau watatu wamenunua baada ya kukiona hiki na kukitest, nao wamesema Hakina shida hadi leo.
 
Aende runzewe akunje kulis mpaka bwanga akunje kushoto to chato,wakati wa kurudi aeleker katoro ,Geita,sengerema mwanza misungwi ,tinde,nzega singida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…