funzadume
JF-Expert Member
- Jan 28, 2010
- 13,624
- 21,362
Kwanza huyo mwanamke hakufai. Pili narudia kwako nilishatoa ushauri huu kwa mtu mwingine humu. Kabla ya kuoa fanya uchunguzi wa kina (ule upelelezi haswa) kuhusu mke mtarajiwa, ndugu zake na maisha yake ya nyuma.Huyu mwanamke tumekua kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwaka. Katika kipindi hicho alikuwa anaishi kwao. Wakati tunaanza mahusiano alinieleza kuwa tayari ana mtoto wa kiume. Na kwasababu pia Mimi nilishapata Mtoto huko nyuma sikuona tatizo. Huyo mwanaye baba yake yupo na maisha yake mengine safi tu.
Baada ya kungoja sana mambo yake sawa, tukafikia kuamua kuishi pamoja angalau kwa kuwahusisha wazazi hasa upande wake. Binti ikabidi aje tuishinaye vkwangu. Hapo awali tulikubaliana kuwa huyo mwanaye atabaki kuishi kwa bibiyake na tutamuhudumia akiwa huko.Mimi mwanangu Yuko shuleni na akiwa likizo anakuja kusalimia na kurudi kwa mama, maana yeye ni wa kike.
Sasa baada ya miezi mitatu ya kuishi naye, huyu mwanamke alisubiri nikiwa safari akaenda kumleta huyo mwanaye aje aishi hapo. Pia hakuishia hapo akabeba na watoto wawili wa dada yake nao kaleta hapo na Sasa Kuna watoto watatu.
Nimesafiri tena na kurudi na bado nawakuta na hawana mpango wa kuondoka. Tayari anawaweja kwenye mipango na bajeti zetu kama wangu vile.
Binafsi napenda kuishi na Mtoto ambaye nakuwa huru naye. Yaani hata nikimuonya asichukulie kama namtesa. Kuna mambo yanafanyika nakaa kimya lakini nimegundua hiyo inanitesa Mimi.
Tafadhali nipe USHAURI wako. Hapo nifanyeje ili nipatie amani bila kuonekana Nina roho mbaya?
Navyoona humjui huyo mwanamke na mambo hayo anayoyafanya yanakujia kama surprise wakati ulitakiwa kuyajua kabla.
Hata hao watoto anaosema ni wa dada yake nahisi ni wa kwake. Wewe unaona kama haya mambo ni simple tu sijui watoto wa dada yake wamehamia kwako, elewa sio simple hivyo. Kuna watu wanaratibu hayo mambo nje na wanakaa vikao kabisa na kukujaribu hawajakurupuka.
Hapo hauna mke ndugu yangu mie mtu mzima nakwambia shtuka na kimbia