Wazoefu wa mambo ya familia nipeni ushauri

Kwanza huyo mwanamke hakufai. Pili narudia kwako nilishatoa ushauri huu kwa mtu mwingine humu. Kabla ya kuoa fanya uchunguzi wa kina (ule upelelezi haswa) kuhusu mke mtarajiwa, ndugu zake na maisha yake ya nyuma.

Navyoona humjui huyo mwanamke na mambo hayo anayoyafanya yanakujia kama surprise wakati ulitakiwa kuyajua kabla.

Hata hao watoto anaosema ni wa dada yake nahisi ni wa kwake. Wewe unaona kama haya mambo ni simple tu sijui watoto wa dada yake wamehamia kwako, elewa sio simple hivyo. Kuna watu wanaratibu hayo mambo nje na wanakaa vikao kabisa na kukujaribu hawajakurupuka.

Hapo hauna mke ndugu yangu mie mtu mzima nakwambia shtuka na kimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…