Wazungu wana uchawi wa "small scale"?

Wazungu wana uchawi wa "small scale"?

Mfano wako hau relate na hoja yangu kiufupi uko irrelevant

Definition ya computer umeijulia wapi?..
Hoja yangu ni kwamba huwezi kutaka kuthibitishiwa kitu ambacho hukijui,huijui computer huwezi kuanza kutaka kuthibitishiwa uwepo wa computer hali ya kuwa hata hujui computer ni nini hivyo lazima ujue computer ni kitu gani.

Maana uthibitisho ni hatua ya kuhakiki sasa huwezi kukurupuka kutaka kuhakiki usichokifahamu hata kinafananaje.
 
Hoja yangu ni kwamba huwezi kutaka kuthibitishiwa kitu ambacho hukijui,
Sio kweli kwamba ili uthibitishiwe kitu ni lazima ukijue, unaweza usikijue kitu halafu uthibitisho ulioomba ukakupa elimu ya kukijua

huijui computer huwezi kuanza kutaka kuthibitishiwa uwepo wa computer hali ya kuwa hata hujui computer ni nini hivyo lazima ujue computer ni kitu gani. Maana uthibitisho ni hatua ya kuhakiki sasa huwezi kukurupuka kutaka kuhakiki usichokifahamu hata kinafananaje.

Unaweza kuthibitisha uchawi upo au hauwezi?
 
Sio kweli kwamba ili uthibitishiwe kitu ni lazima ukijue, unaweza usikijue kitu halafu uthibitisho ulioomba ukakupa elimu ya kukijua...
Nimekwambia unapotaka kuthibitishiwa maana yake unataka kuhakiki,sasa unahakiki vp ambacho hukijui?

Kujua kitu ni jambo moja na kuthibitisha ni jambo lengine.
 
Magonjwa kama yapi?
Nikupe mfano wa ndugu yangu alikuwa na rafiki yake walienda Tanga,kufika kule yule ndugu yangu ziwa lake moja likavimba na kuwa kuwa kubwa na yule rafiki yake macho yakawa yanawasha sana kama mtu anayasugulia na mchanga. Hawakwenda hospitali walikwenda kwa mganga na kutibiwa huko na kuambiwa ilikuwa ni uchawi aina zongo.
 
Vp kama walipatwa na allergy au maradhi mengine?

Ukiambiwa kitu fulani ni uchawi na kupewa dawa ukapona hiyo inahalalisha kwamba ni uchawi?

Unaweza kuumwa malaria tukasema umelogwa ila ukapewa mseto na kupona, does that make malaria kuwa uchawi?

Story za uchawi zote huwa zipo hivi; kwanza zote ni story za hearsay kama yako ambayo inaondoa credibility yake kwa kiasi kikubwa maana pengine hata wao waliokupa story wamejitungia au kuongeza chumvi, pili huwa hazi add up kama yako.
 
Vp kama walipatwa na allergy au maradhi mengine?

Ukiambiwa kitu fulani ni uchawi na kupewa dawa ukapona hiyo inahalalisha kwamba ni uchawi?...
Kwa mganga sio hospitali ambako kuna vipimo vya kujua tatizo lanalo msumbua mtu,ndio maana hata wewe unajaribu tu kuotea kuwa labda ilikuwa Allergy au maradhi mengine ila walipoenda kwa mganga na mganga alijua tatizo ni nini na akawatibu.

Halafu kwani nikitaka kuelezea corona au ukimwi ni kwamba lazima niwe mimi mwenyewe nimeumwa huo ugonjwa? Ukitaka nieleze matukio ya yenye kuhusu uchawi ambayo mwenyewe nimeshuhudia yapo naweza kukutajia.
 
Kwa mganga sio hospitali ambako kuna vipimo vya kujua tatizo lanalo msumbua mtu,ndio maana hata wewe unajaribu tu kuotea kuwa labda ilikuwa Allergy au maradhi mengine ila walipoenda kwa mganga na mganga alijua tatizo ni nini na akawatibu...

Watu wengi tu wanatibiwa kwa njia za jadi bila kwenda hospital na wanapona. Kipi cha ajabu hapo hadi useme uchawi?
 
Biashara zao ni ubora wa bidhaa na huduma. Tz biashara haziendi kwa kuwa umasikini umezidi, watu hawana pesa za kutumia. Nchi zilizoendelea kuna ajira na kupelekea watu wengi kuwa na uwezo wa kufanya manunuzi, hivyo biashara zinashamiri.
Words
 
Nimekwambia unapotaka kuthibitishiwa maana yake unataka kuhakiki,sasa unahakiki vp ambacho hukijui?
This is fallacy.

Ukisha pata uthibitisho wa kitu fulani unakua umepata ujuzi (kujua). Uthibitisho hutangulia kabla ya ujuzi, uthibitisho ni njia ya kuufikia ujuzi. Sasa inakuaje utake uthibitisho wa kitu ambacho umekijua?
Kujua kitu ni jambo moja na kuthibitisha ni jambo lengine.
Sasa hapo ni tatizo lako kutoweza kuthibitisha jambo ambalo unalijua. Na kwa pointi hiyo umekosa vigezo vya kumfanya mwingine ajue

Nataka kujua unaweza kuthibitisha uchawi upo au hujui kuthibitisha?
 
Mmmhh! Nimeipenda comment yako.
Ila kwenye ujenzi ni shule tu ndio hutumika ndugu. Tupo kwenye hiyo industry ya ujenzi ndio maana nasema hivyo.
Japo kuna mazingira mengine hutokea ugumu wa asili(mazindiko ya wakaazi wa eneo husika. Kama waliweka zindiko au hapana). Mfano, Kabiri la ukoo wa Kiyeyeu huko Iringa.
ukitaka amini wazungu ni wachawi ujenzi wa madaraja haya ya kawaida. bwana weee! Wana sarakasi si kawaida. Hapo mweusi huitwi. Unasubiri nje Kama lile la kirumi. TARIME/ musoma jamani wee! walikuwa wanajenga usiku tu. Hapo ni baada ya company kibao kushindwa.
 
This is fallacy.

Ukisha pata uthibitisho wa kitu fulani unakua umepata ujuzi (kujua). Uthibitisho hutangulia kabla ya ujuzi, uthibitisho ni njia ya kuufikia ujuzi. Sasa inakuaje utake uthibitisho wa kitu ambacho umekijua?

Sasa hapo ni tatizo lako kutoweza kuthibitisha jambo ambalo unalijua. Na kwa pointi hiyo umekosa vigezo vya kumfanya mwingine ajue

Nataka kujua unaweza kuthibitisha uchawi upo au hujui kuthibitisha?
Sasa inakuaje utake uthibitisho wa kitu ambacho umekijua?

Nimeshasema hili kuwa kwa kifupi uthibitisho ni kuhakiki na hauwezi kuhakiki usichokifahamu. Kujua hakuna maana ya kwamba unachokijua ndio ukweli na si vinginevyo,ndio maana kuhakiki(kuthibitisha)
 
Watu wengi tu wanatibiwa kwa njia za jadi bila kwenda hospital na wanapona. Kipi cha ajabu hapo hadi useme uchawi?
Kwani wewe unaelewa vp neno "jadi"? Unavyojua wewe ni kwamba hakuna tiba za jadi ambazo zinahusu ushirikina? Issue hapa ni aina ya tatizo kama tatizo ni limesababishwa na uchawi basi litatatuliwa kama tatizo la kichawi,iwe kwa kutumia njia jadi ama si ya jadi.
 
Sasa inakuaje utake uthibitisho wa kitu ambacho umekijua?

Nimeshasema hili kuwa kwa kifupi uthibitisho ni kuhakiki na hauwezi kuhakiki usichokifahamu. Kujua hakuna maana ya kwamba unachokijua ndio ukweli na si vinginevyo,ndio maana kuhakiki(kuthibitisha)
Kuhakiki na kuthibitisha ni mambo mawili yanayoonekana kufanana lakini kiutendaji yanautofautiana

Kuhakiki (verify) ni kuangalia maelezo kujua kama hoja ni ya kweli, ambayo maelezo hayo ni uthibitisho uliopewa kuhusiana na kitu usichokijua

Kuthibitisha ni kuonesha kitu fulani ni kweli kwa kutafuta maelezo mwenyewe tofauti na kuhakiki ambapo unachukua taarifa ulizopewa ambazo ni uthibitisho

Kwa hiyo mimi ukinithibitishia uchawi upo utakua umefanya attempt moja ya kutoa uthibitisho kisha baada ya hapo tutaingia zoezi la pili la kuhakiki huo uthibitisho ili tuone kama kweli ni uthibitisho wa kweli na kuanzia hapo nitakua nishajua

Unaweza kuthibitisha uchawi upo?

Thibitisha
 
"Kuthibitisha ni kuonesha kitu fulani ni kweli kwa kutafuta maelezo mwenyewe"

Unaweza ukafafanua ulichokieleza hapo?
 
Back
Top Bottom