Mwanahabari wa Taifa
JF-Expert Member
- May 27, 2020
- 1,588
- 956
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe David Kafulila akihojiwa na Ayo TV amekuwa na haya ya kusema juu ya kupungua kwa rushwa Tanzania kisayansi,Msikilize
Kafulila anasema,Ripoti ya kimataifa ya kupambana na rushwa inaonesha Tanzania tumetoka nafasi ya 94 mpaka 87 sawa na vietnam & Moroco kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti na taasisi ya kitaifa ya Transparency International kwa vigezo 180 na kuziacha nchi za Msumbiji 149, Uganda 142, Kenya 128, malawi110 na Zambia 117
Aidha,Taasisi inayojishughulisha na harakati za kusimamia uwazi na mapambano dhidi ya rushwa na Ufisadi duniani ya " Transparency International " tayari imetoa ripoti yake ya mwaka wa jana,
Taasisi hii iliyofanya kazi ya kuchunguza na kutafiti kiasi cha rushwa na Ufisadi kwenye nchi zipatazo 180 duniani kwa kutumia kipimo cha Corruption Perceptions Index ( CPI ) huku Tanzania nayo ikiwemo mwaka 2020'21.
Ripoti iliyotolewa na taasisi hiyo inayoheshimika zaidi duniani kwa kuwa na taarifa za kweli ya Transparency International inaonesha nchi ya Tanzania rushwa na Ufisadi vimepungua Sana wakati huu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameachia uhuru wa kujieleza kwa wananchi wake,
Mtakumbuka Tanzania ilipata alama 36 kati ya alama 100 zilizotolewa na taasisi hiyo mwaka 2019'20 huku Tanzania tukishika nafasi ya 94 kati ya nchi 180 zilizochunguzwa mwaka huo,
Kwamujibu wa ripoti iliyotolewa mapema mwaka huu Tanzania imepanda kwa nafasi saba ( 7 ) toka ile ya 94/180 mwaka 2019'20 hadi kufikia nafasi ya 87/180 huku ikijizolea alama 39 kati ya alama 100 zilizotolewa,
Hongera Tanzania, Hongera Mama Samia Suluhu Hassan kwani huu ni ushindi mkubwa kwa Taifa,