Wazungu wapewe maua yao na si lawama, Utumwa ulikuwepo Dunia nzima, Wao ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha harakati za kuufuta

Wazungu wapewe maua yao na si lawama, Utumwa ulikuwepo Dunia nzima, Wao ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha harakati za kuufuta

hebu na wewe wacha huo ukenge unaoita wenzakp, hivi hiyo heligoland treaty inahusu nini wakati ilikuwa ni issue ya kubadilishana visiwa ili waweze kutawala vizuri zaidi? Au umeona ukitaja hiyo treaty ndiyo wengine hatujawahi kusikia? Unadhani hatujui kama hizo treaties ni mbinu tu za watawala kumiliki nchi nyingine?

Na vile vile tunajua kuwa hasa Waingereza walianza kupiga vita utumwa baada ya kuona hauna faida kwao na hasa baada ya kuanza kutengeneza mashine za kufanyia kazi mbali mbali.

Nenda kaangalie clips za Thomas Sowell kuhusu biashara ya utumwa kwenye youtube utapata maelezo ya kutosha.
helgoland, mkataba wa uingereza na ujerumani kuhusu kisiwa cha helgoland-zanzibar
 
Maslahi ya watumwa yalimalizwa na maendeleo ya science na teknolojia. Weupe wote wanaishi na sisi kimaslahi tu. Sasa wewe jione unapendwa.
 
Tunaanza na hapa kwetu Afrika, utumwa ulikuwepo hata kabla ya waarabu na wazungu kuja, hapo badae soko la watumwa wa kiafrika lilikuwa kubwa na kutufanya sisi kwa sisi waafrika tuanze kuuzana kwa wageni, hivyo nasi tulishiriki kwa kiasi kikubwa sana kwenye utumwa

Warabu walikuwa na watumwa na hapo badae kuanza kununua watumwa huku Afrika, hawa walipinga sana harakati za mzungu kupiga stop utumwa, ilibidi kuwe na jitihada za ziada, mpaka leo nchi za kiarabu kama Libya na Mauritania bado kuna biashara ya utumwa kwa waafrika wanaowakamata wakijaribu kuvuka nchi hizo kwenda ulaya.

India kulikuwa na watumwa ila mpaka leo wana matabaka ya kuamini flani yupo chini ya flani, makampuni ya wahindi hapa kwetu yamekuwa yakilalamikiwa baadhi ya mambo kufanyika kitumwa

Wazungu wao kwa wao walitumikishana, waingereza waliwahi kuwa na makoloni mengi hapa duniani kuanzia india, nchi za kiarabu, china, n.k.

China kulikuwa na watumwa

Israel kulikuwa na watumwa

Walatini walikuwa na wafltumwa, mfano mzuri muvi ya apocalypse

Kwenye vitabu vya dini kulikuwa na watumwa

..................

Lakini licha ya wazungu kupiga stop utumwa bado walikuwa na nafuu kwa mbali, walitupa elimu, waliruhusu watumwa tuweze kujiongoza kwa kiwango flani, waliruhusu kuzaliana leo hii kuna wamarekani babu zao walikuwa watumwa, ikafikia hatua wazungu wao wenyewe wakaona utumwa sio sawa wakaupiga ban.

Na kumbuka mwenye mamlaka makubwa ya kuchukua hatua hii ni yule anaetumikisha sio watumwa wanaotumikishwa,

Si kuharamisha tu utumwa kwa binadamu lakini wazungu wapo mbele zaidi wameweza kutokomeza kwa kiasi kikubwa unyanyasaji wa wanyama.
Nashangaa watu wanawaskama wenzao kwa kuwatolea hoja warab wakat wao wanashinda kuwafagilia wazungu. Kweli nyani haoni kundule
 
Lakini waarabu wana petrol, diesel za kutosha majamaa haya yamegundua mafuta jangwani
 
Back
Top Bottom