WCB na mikataba ya ajabu: Ndio maana muziki wa Tanzania hauendelei

Kwa nini unakimbilia post za magazeti kwenye internet usisome makaratsi ya mahakamni yenyewe? Yanaanza hivi


Ni karatsi 50, kwa hiyo ukitaka kutafsiriwa kwa lugha rahisi kutoka lugha za kisheria itakuwa ni vigumu kwa leo.


Halafu kama hujui malalamiko ya Kanye (niliyaandika huko nyuma) ni kuwa mkataba huo unatumia muda unaitwa "contract year" ambayo siyo miezi kumi na mbili bali ni kipindi ambacho Kanye anafikisha kutoa nyimbo kadhaa. Akifikisha idadi hiyo ndani ya miezi 12, basi mwaka inakuwa ni miezi 12, na asipotoa nyimbo zinazotakiwa kwa miaka minne, basi miaka yote minne hiyo inahesabiwa kuwa ni mwaka mmoja. Malamiko yake ni kutaka definition ya mwaka iwe wazi siyo hiyo ya kubadilikabadilika. Soma makaratasi ya kisheria ambayo nimekuwekea siyo hayo maneno ya Yahoo ambako mtu yeyote anaweza kuandika. Kwanza kesi yenyewe hata haijaamuliwa bado iko mahakamani halafu wewe unakurupuka na upupu hapa kwamba ameamuliwa na new York City wakati kesi yenyewe iko California.


Hata hiyo link ulyoweka ya Yahoo nadhani uliokoteza tu bila hata kuisoma kwani haipo. Ni tabu kweli kuelimisha graduates wa shule za kata (no offense).
 
Harmolapa ndio mfano mzuri...wali-mpromote sana na show alipiga nyingi pesa ikaingi...ilikuwa ni ptoject ya muda tu.
 
Kuna watu hapa wanaandika kwa emotions, siyo rational. Ni kazi ngumu sana kwa wanaojadili mambo kwa facts na logic kushiriki mjadala huu ambao ni wa kisheria zaidi ya Celebrities.
 
Watarudi kusema Diamond mchawi kamroga Harmonize
 
Hii comment nayo siyo rational kwani hata Diamond naye alihama hivyo hivyo kutoka label moja hadi nyingine, kubadilisha maproducers na mameneja kadhaa kabla hajawa hivyo alivyo leo; ndiyo process yenyewe. Siyo kuwa yeye ndiye atakayewamiliki wasanii wote wajao kwa vile amefikia levo hiyo; kuna watakaopita kwake na kwenda kijisimamai wenyewe na inawezekana wakaja ambao hawakupita kwake labda wakawa zaidi yake. Ndivyo nature ilivyo!
 
Biashara siku zote Hakuna Anayependa Hasara
Mambo ya Mikataba tu ni ishara tosha Ya Ubeparii
Mbona Mond Alivunja Mkataba Wake Aliokua Chini ya Papaa Misifa Na Akalipa Hela Kuuvunja
Ngoja Tuone Konde Nae
 
Kuhama kundi sio mbaya hata sehem za kazi zingine pia huwa inaruhusiwa kuacha na kwenda sehem nyingine ila ubaya unakuja pale mnapoanza kumponda diamond na kumuona Hana maana,mara kumuita mnyonyaji wakati aliwasaidia.
 
Mkuu acha upunguani!!! Usikurupuke kuandika usiyoyajua kwasababu ya chuki zako binafsi. Mof
 
Kuhama kundi sio mbaya hata sehem za kazi zingine pia huwa inaruhusiwa kuacha na kwenda sehem nyingine ila ubaya unakuja pale mnapoanza kumponda diamond na kumuona Hana maana,mara kumuita mnyonyaji wakati aliwasaidia.

labda hujawahi kusoma post zangu huko nyuma kwa sababu huwa sipost kwenye jamvi hili hap isipokuwa kwa kuwa thread hii ni ya kisheria zaid ya kiudaku. Majibu ya jumla huwa siyapendi kabisa, ukinijibu mimi, niambie mimi usiniunganishe na wengine. Mimi sijamponda Diamond popote, at the best nilisema makosa ni kwa wanasheria wao. lakini sasa hizi genralization kuwa "mnapomponda Diamond" kama vile kweli umesoma "ninapomponda" mtu yeyote hapa huwa kweli zinaniudhi sana.
 
2pac alimletea habari za kuleta CEO wa death raw record mafia mwenyewe SUGE KNIGHT, jamaa alitumia pesa nyingi kum brand 2pac halafu akamletea uhuni ikabidi ampoteze kwenye ramani...
Uongo, huyo Suge Knight alishirikiana na CIA kumuua Shakur kwa kuwa jamaa walianza kuharibu kizazi cha black upande wa West side.

Alichofanya Suge ni conspiracy tu, ni kama tunavyoona kwenye movie kama enemy within.
 
lakini tuelewe hii mikataba hii!

muda wa mkataba dont matter mleta maada, inadepend on benefit pande mbili
 
[emoji375][emoji375][emoji375]
 
Jamaa hajui kama anamharibia dogo, Harmonize anajitahdi kubalance mambo na WCB kama wanamtetea kiaina, japo Fans wa WCB wanamuona msaliti, Kibaya zaidi fans wa konde boy ndo wanachochea Moto, nyuzi kama hizi za mtoa mada ndo zinadamage Sana career ya konde boy , Mond ana fanbase kubwa Sana, kama konde boy anawaza kumwangusha Diamond nampa pole, Hawezi Kwa sasa, mwenzake yupo extra mile, ashapigwa vita na media kubwa nyingi hapa bongo but still anafight, Harmonize inabidi atumie hekima Sana Kwa mda huu, na kukaa kimya ndo best solution ikiwezekana aendelee kuwapa credit WCB kila inapowezekana hata kama akiondoka, hii itampa matokeo mazur in the long run, but not today

.
 
Tatizo lipo wapi.
Music ni biashara kila mtu analenga faida
Kwani harmonize alijua kama angefik hapo alipofika leo..??
Kwan wcb kipnd wanainvest kwa harmo waliona angefika hapo ...??
Msanii gani wa wcb amepewa promo kuliko harmo..??

Na harmo alipewa promo ili mond awaprove watu wote wrong kwamba anaweza mtengeneza mtu akawa mkubwa.

Tatizo harmo anajiona big kwasababu ni mwaka sasa mond alikua hajatoa nyimbo
Mond akawa anadeal na media
Tobo kwa harmo likaonekana
Akapita
Alaf pia wale mashabik wa kiba ndo wanaosupport huu ujinga
Wale wale waliomkataa kipind cha aiyola leo ndo wanaona anakandamizwa
 
Kwa hiyo wewe kinakuuma nini? Hukutaka aelimike? Kila mtu huwa ana pa kuanzia kabla ya kufikia mafanikio. Na yeye Harmonize pa kuanzia kwake palikuwa WCB, sasa kapata uzoefu kwa nini asisimame mwenyewe? unataka amtegemee Diamond mpaka lini? Nenda Harmonize kapambane kivyako. Jua tu kuna kushinda na kushindwa. ukishindwa basi tafuta tena pa kuanzia bila kujali maneno ya watu.
 
Drake ameshajitoa YMCMB
Lil Wayne nae alishajitoa chini ya Birdman a.k.a Baby
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…