Kaka mbona huelewi?, Africa tunabaki kuwa masikini kwasababu ya kuendelea kuuza bidhaa za mashambani moja kwa moja (raw materials). Hivi dunia inapopiga kelele kuhusu " value addition" wewe hata huelewi maana yake nini?. Tunapozingumzia uchumi wa viwanda lengo ni hilo kaka yangu, ukiruhusu nchi au watu kununua Mali ghafi eti kwasababu ndiyo wanayohitaji, hakuna hata mmoja atakayenunua bidhaa zetu za viwandani.
Bahati nzuri umeekeza faida za mahindi. Tukisaga unga hapa nchini, tutatengeneza ajira katika viwanda vya Kusaga, na katika viwanda vya chakula cha mifugo, pia viwanda vya chakula cha mifugo vitaweza kuuza kwa watanzania kwa bei nafuu kuliko wakiagiza hicho chakula cha mifugo kutoka nje. Tutauza Unga ambao bei yake ni Mara mbili ya bei ya mahindi, tutapata pesa nyingi zaidi.
Kama unasema wanaweza kukataa kwenda kununua nchi zingine, kwani wao ndio wanunuzi pekee?. Kwa taarifa yako, Azam anauza Unga mwingi sana katika nchi za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Msumbiji, kuliko anavyouza ktk soko la East Africa, lazima tuendeleze viwanda vya ndani, na viwanda vyetu lazima vitumie Mali ghafi ya ndani ili wakulime wapate bei nzuri ya mazao yao.