Jambo jema, lakini ni tiba? Inapaswa tujifunze toka huko zilipoanzia, wao wamefanyaje? Wanawalindaje watoto? Maana wao wanazo miaka na miaka. Na ukilinganisha, sidhani kama watoto wao ndo watu washenzi kihivyoooo. Ninadhani kuna mahali tunakosea , tujifunze namna bora ya kukabiliana na hili tatizo. Kufungia si tiba mujarabu saana, maana kwa utandawazi huu, siku watoto wakipata upenyo na kuanza kuziona, tutajuta.
Sisi bado tunaishi zama zileee,kudhani kuficha na ubabe ni tiba. Kama tunaweza kuuenzi utamaduni huu wa kizamani , sawa tuufanye. Lakini, kama hatuuwezi, tutafute mbinu mbadala.