Weka urafiki na wanajeshi (bakabaka) hutojutia

Kumtoa mtu kituoni inategemea na kosa.

Kuna dogo mmoja (Mfanyakazi wangu) alizingua huko mtaani nikaletewa kesi.

Mie nikashauri wafate utaratibu wa sheria au tuyamalize.. wale walalamikaji wakaforce kwenda polisi.

Basi dogo nikamwambia atulie hawawezi kwenda polisi wale.. khee kumbe kweli walienda kushtak na wakaja na RB.

nipo zangu ndani, naskia fujo nje Dogo wamempiga pingu wanaondoka nae wale jamaa walioshtaki polisi wana ndugu yao ni polisi ktk hicho kituo so wana backup ndio maana walikuwa wanataja taja sana neno polisi kutishia.. , basi nikawauliza jamaa ni akina nani tutambuane? Na wanampeleka wapi? Kwa kosa gani? Na je nguvu iliyotumika ni sahihi? Aligoma? Kwanini kumfunga pingu na kumdhalilisha?.. walimfungua ila kwa mbinde.

Haya.. mie nikawaacha waende nae then nitawafata kwa nyuma (nilikuw sijajiandaa).

Basi, Dogo kafika kule katiwa lockup, mixer kumtishia kwamba na mimi nikienda natiwa ndani pia maana ninajifanya najua sana Sheria... wakawa wananisubiri kwa HAMU sana nijipeleke.

Basi, kufika nikataja jina pekee na mtu niliyemfata.. wakasema anhaa wewe ndio tunakutaka sana pita huku.. mie nikagoma, nikawaambia kabisa, mkiniweka humo ndani siku/saa/dk au sekunde ninayotoka humo tunapishana siti, na nyie mtaingia humo humo.

Wakawa wanatoa macho tu.. kukata urefu wa story..

Dogo nilimtoa kwa KUFATA utaratibu na dhamana nikapeleka, wakati napeleka barua ya utambulisho ndio wakagundua kitu, basi Dogo nikarudi nae home.

Wakati tunarudi sasa wale jamaa waliompeleka polisi tukakutana nao walishangaa sana kutuona, wao waliamini Dogo yupo ndani, na mimi nipo ndani eti..

Hii kesi iliisha kibabe sana after 2 days...

Kuna muda tunatumia maneno haya " MENO ya MBWA hayaumani "
 
Naam upo sahihi kabisa lkn kwenye ground hapako hivyo. Reheat post yangu pale huu nilipo m quote ujoka, experience yangu na polisi simiyu. polisi simiyu. Wale polisi ni wezi na wametengeneza ushirika na ofisi ya mwendesha mashtaka, mahakama na baadhi ya mawakili.
 
Dah! Nidhamu ya kutishia polisi? Nidhamu ya kuvunja protokali? Subiri wakati ukifika ndio utajua hujui. Urafiki na wanausalama ndio ila uwe wa kimkakati sana.
Kabisa mkuu.
 
Hivi mbona mnaongea mambo kirahisi sana, hao polisi wenyewe ukijifanya kuzijua sheria na haki zako wanakuambia "okay wewe si unajifanya mjuaji sasa utaozea humu", sasa unafikiri hapo kama huna nguvu ya ziada kama pesa au connection unafanyaje
Wanajiongelesha hao.

Ukweli wanaujua au bado hawajawahi kuingia humo polisi wanasikia stori.
 
Bado hujatoa suluhisho, mfano kijana tu wa mtaani kakamatwa bila kosa na hana pesa wala connection anafanyaje kutoka ndani, pengine anaweza kuwa anazijua sheria na haki zake niambie anazitumiaje hapo ili wamuachie bila kumdhuru
JWTZ wavamia kituo cha FFU na kukisambaratisha | JamiiForums JWTZ wavamia kituo cha FFU na kukisambaratisha

Waambie wakae kwa kutulia.

Sisi wajasiriamali tushabebwa kuingia sana msimbazi na stakshari tunajua hao wote wanakula na kulala kwao.
 
Pale stakshari kulala corridor ni uwe mbabe🤣

Wote ndani tena unalala mchongoma umenyooka kiupande pande.

Mbu plus taa kuwaka aseee na harufu ya chooni. Acheni stori mnazodanganyana.

Aliletwa jamaa alikuwa ni dereva katika taasisi Fulani. sasa jamaa kagomea kutoka pale mlangoni, sababu ukingia lazima uitwe mwisho kule vyoo vilipo wanakukagua.

Baada ya hapo, wakaja wale watukutu, wakamwambia afande jamaa hataki kutoka hapa.

Afande alitamka neno moja mfinyeni, asee ndani ya dakika1 yule jamaa macho yameumuka.

Afande huyo anatoa go ahead watuhumiwa wampige mtuhumiwa mwenzao.


Hapa tunadanganyana tu eti Sheria sijui nn.

Kutoka polisi
1. Uwe na mwanasheria.
2. Uwe na connection ya mtu mwenye nguvu zaidi.

3. Uwe na pesa za kuhonga.

FULL STOP

kuna vijana wamesingiziwa wapo wana miezi 2 anakuambia hajui afanye nini.

Mnadanganyana tu hapa Sheria
 
JWTZ wavamia kituo cha FFU na kukisambaratisha
 
Primitive & Uncivilized Society always don't fall order & Law.
Si kosa letu ndo mana mkoloni alituona bara la watu wajinga,manyani. Kwa hiyo Bado tuko era of uncivilized society.
 
Primitive & Uncivilized Society always don't fall order & Law.
Si kosa letu ndo mana mkoloni alituona bara la watu wajinga,manyani. Kwa sisi Bado tuko era of uncivilized society.
Mkuu ushawahi ingia stakshari au kituo chochote?

Kama ulishawahi kuingia niambie kuna haki na Sheria humo ndani?

Mimi nishakutana na misala ya kuwepo humo ndani marafiki zangu bakabaka wananisaidia au natoa rushwa tena kwa kuambiwa weka kitu tukutoe.

Hivi nyinyi mnazungumzia Tanzania gani kwani??
 
wale jamaa ni Bora hata uingie mikononi mwa majambazi unajua ukiyabahatisha unaweza ukayaotea ukayaua sasa haya mapimbi ukiyaua ujue umekwisha 😁
 
wale jamaa ni Bora hata uingie mikononi mwa majambazi unajua ukiyabahatisha unaweza ukayaotea ukayaua sasa haya mapimbi ukiyaua ujue umekwisha 😁
Kwakweli kuna majambazi wenye uniform na wanaolipwa mishahara. Reffer Simiyu. Kabla ya kuingia kwenye changamoto ya kunikutanisha nao, niliamini sana jeshi la polisi. Niliwaambia nikawapa kila taarifa Ili wafanye kazi yao vizuri na kwa urahisi lkn wao sasa kumbe ni watafuta pesa.
Majizi makubwa yale.
 
Usihangaike na huyo boya hajatembea huyo
 
tulia we pongo mjeshi akitoa boko akiingia selo anaakua mpole ila akiuziwa kesi ya kifala kama tunazouziwa sisi sijui uzururaji jua akipiga simu Moja tu tu kwa wanae vipongo lazima vijinyee

Kuna ex polis alinipa mkasa wake , kipind wapo doria za usiku wanaokota mandezi wakamzoa ba mwamba mmoja yuko na bag lake wakamtia pingu bag wakakata nalo wenyewe wakazaurura naye usiku kucha maana yeye alikua hawongei wengine wanatoa mpunga wanashushwa unapewa simu yako upigiwe ndugu zako waliweka marundo unashushwa alfajir kabak jamaa na walevi kadhaa wakapelekwa kituoni sasa kufungua bag la jamaa anakutana na gwanda zina nyota apo ndio walijua wamejipakata mkuu wa kituo ndio alikuja kuomba radhi kwa niaba ya wahuni wake, katika scenario kama hii usitegemee luten ataanza process za dhamana serikali ya mtaa akipiga simu kikosin kitakachofatia hapo ni west bank
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…