Wema Sepetu akutwa na hatia ya kukutwa na Madawa ya kulevya! Alipa faini na kuachiwa huru

Wema Sepetu akutwa na hatia ya kukutwa na Madawa ya kulevya! Alipa faini na kuachiwa huru


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Ijumaa, Julai 20, 2018 inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu na wenzake wawili.



Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu tayari amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili.



Hukumu ya kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Mrembo na mwigizaji Wema Sepetu imeanza kusomwa na Hakimu Thomas Simba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam muda huu.

=======

View attachment 813906
Msanii wa filamu ambae pia alikuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu amekutwa na hatia ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya.

Ahukumiwa jela mwaka mmoja au kulipa faini ya milioni 2.

Washtakiwa wawili kwenye kesi hiyo ambao ni wafanyakazi wake wa ndani wameachiwa huru baada ya kukutwa hawana hatia

Habari zaidi, soma=>Sakata la Madawa ya Kulevya: Wema Sepetu afikishwa Mahakamani, apata dhamana

Mkemia Mkuu: Mkojo wa Wema Sepetu ulikuwa na bangi


Wema amelipa faini, wakili wake, Msando amezungumza

Huyu martin kadinda anaweka nini wema. Maana si mchezo hiyo kufuli ya mikono
 
Hata akifungwa kesho yake atatoka kwa msamaha wa nanihii. Maana yeye hataki wasanii wakae jela wanakula sana na kutia hasara serikali yake.
 
tuliambiwa sheria za kupambana na madawa ya kulevya zimekuwa Kali kumbe hamna kitu !!!! kwa wenye mifedha watapeta tu!!! kwa style hii wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya kamwe hawato acha
 
Heading:...... Miaka miwili,Content........ Mwaka mmoja.Epukeni upotoshaji wa makusudi.
 
Ni kweli wakikosa kuvuta bangi, kuwa mateja basi wanakuwa MASHOGA,au VYOTE KWA PAMOJA, MUNGU APISHIE MBALI, yote inatokana na kuiga mambo ya wazungu
 
Mwana ccm huyo hii sheria ingakuwa inatumika hadi kwa wakina chid benz tungepunguza mateja mitaani.
 
ila wajamaica wakijua kuna watu wanafungwa kwa ajili ya marijuana.watafungua kesi mahakama za juu.
 
Back
Top Bottom