Wema Sepetu amwokoa Kajala, atoa milioni 13 kumnusuru

Wema Sepetu amwokoa Kajala, atoa milioni 13 kumnusuru

HUKUMU ya kesi iliyokuwa
inamkabili staa wa filamu za
Kibongo, Kajala Masanja na
mumewe imetolewa leo na
Hakimu Sundi Fimbo katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar.

Katika hukumu hiyo Kajala
amehukumiwa kwenda jela
miaka mitano au kulipa faini
ya shilingi milioni 13 na
mumewe kwenda jela miaka
saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.

Kajala alikuwa anakabiliwa na
kesi ya kuuza nyumba
iliyowekwa kizuizini na Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) baada ya
mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa
kutakatisha fedha haramu.
 
Steve Nyerere ametoa au amechukua ngapi?
 
Jamani Kajala pole sana na karibu tena uraiani!
 
Habari Njema Hii,kiukweli Kabisa Kajala Ni Muigizaji Mzuri! Sasa Mbona Hamtuambii Mumewe Nae Kalipa Hiyo Fain Ya Mil Miambili Au?yaani Hawa Waume Zetu Hawa,kwa Kweli Unaweza Kujikuta Matatizoni Bila Kujua! Ni Kuomba Tu Mungu,vyanzo Vya Mapato Ya Waume Zetu Ni ZAIDI YA TUJUAVYO!
 
attachment.php

Hawa hapa!!!!!!!!!!!!
 
Attachments

  • Wema and Kajala.jpg
    Wema and Kajala.jpg
    18.9 KB · Views: 5,795
Habari Njema Hii,kiukweli Kabisa Kajala Ni Muigizaji Mzuri! Sasa Mbona Hamtuambii Mumewe Nae Kalipa Hiyo Fain Ya Mil Miambili Au?yaani Hawa Waume Zetu Hawa,kwa Kweli Unaweza Kujikuta Matatizoni Bila Kujua! Ni Kuomba Tu Mungu,vyanzo Vya Mapato Ya Waume Zetu Ni ZAIDI YA TUJUAVYO!

Ni ngumu mwanaume au mume wako kukuambia source zake zote anazoingizia hela coz akikuambia lazima utamchukia na kumkataza ndio maana mengine atuwashirikishi wanawake/wake zetu maana utafanikiwa.kwa ufupi nyinyi ni waoga sana kutake risk kuliko wanaume.
 
Hakimu Sundi.... mshtakiwa Kajala

watoto wa kisukuma hao
 
Hongera wema, ulichofanya kitabaki katika moyo wa kajala daima na washabiki wako kwa ujumla.......
 
Ngoja uone magazeti ya kesho..!
sasa wewe ulishapata hizi taarifa zote magezeti ni ya nini tena!?? Au u miongoni mwa wale ambao hata akishuhudia tukio linatokea hayaamini macho yako mpaka uone 'imeandikwa gazetini'.

Siwezi kujua Wema hiyo pesa kaitoa kwenye hazina gani lakini kihuhakika kaonyesha picha tofauti kwa jamii maana katika maeneo ambayo mtu asingependa yeye au ndugu yake kuishi ni gerezani. Kwa hili kaonyesha uungwana halisi.
...na inaweza kuwa 'reminder' kwa wale waliokuwa wakibishia kauli ya jk kuwa 'atatengeneza mamilioneaire'
 
Hongera Sana Wema Sepetu! Wenye Moyo Wa Kutoa Km Wewe Ni Wachache Sana! Kajala Mshukuru Wema Sepetu,ni Rafiki Wa Kweli!
 
Sasa mbona hamsemi mumewe naye imekuaje mnamsema kajala tu wakati wote kesi yao ilikuwa moja.
 
sasa wewe ulishapata hizi taarifa zote magezeti ni ya nini tena!?? Au u miongoni mwa wale ambao hata akishuhudia tukio linatokea hayaamini macho yako mpaka uone 'imeandikwa gazetini'.

Siwezi kujua Wema hiyo pesa kaitoa kwenye hazina gani lakini kihuhakika kaonyesha picha tofauti kwa jamii maana katika maeneo ambayo mtu asingependa yeye au ndugu yake kuishi ni gerezani. Kwa hili kaonyesha uungwana halisi.
...na inaweza kuwa 'reminder'
kwa wale waliokuwa wakibishia kauli ya jk kuwa 'atatengeneza mamilioneaire'

mmhuuu!!!! ndo nini hapo? kama kuna kitu tofauti kinazungumziwa hapo
 
Back
Top Bottom