Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi

Wema Sepetu, Mr. Blue, TID, Recho wahusishwa na Dawa za Kulevya. Watakiwa kuripoti kituo cha Polisi

Hii vita ya madawa ya kulevya sio vita ndogo ,mataifa mengi makubwa bado wanahangaika nayo mpaka leo,hivyo hatua anazochukua Mh Makonda sio za kubeza hata kidogo.hatuna budi kumuunga mkono kwa kutoa ushirikiano kwani wasambazaji wamo humu humu mitaani kwetu na wanajulikana kabisa.
 
Naamini hawakutajwa kwa chuki,haki itatendeka KWAO! Ukituhumiwa kuwa mpole,subiri ,onyesha USHIRIKIANO na vyombo vya usalama,MATOKEO yake ndio ukweli halisi unaotakiwa!
 
Paulo anakuwaga mawazo yenye tija kwa kizazi hiki na kijacho kuna muda anajitoa ujinga kabisaaa mpk mi nywele znanisisimkaga inakuwa vigumu hata kuamin km ni drama Angeondoa na mabuibui ya siasa kichwani angekua mashuhuri kuliko hata bwana huyu anyway huyu ndio wakumeongezea dozi ya maombi this time ili adhma hii ya kulinusuru taifa na vijana lifanikiwe
 
Mgombea ubunge wema yumo daaah kweli huyu nae eti alikua anataka awakilishe watu kupitia viti maalum! Daahh nakupenda burr makonda kuanzia Leo! Ukiwin hili utaandikwa ktk vitabu vya historian ya nchi hii watoto wetu wake wakusome habari zako
Kabla ya kusubuiria ku win kwake, anaonekana keshaanza kwa kufeli, mkuu wa ulinzi na usalama wa mkoa, anaanzaje kuwataja watuhumiwa kwa majina ya kihuni huni! Tena wengine ni waajiriwa wa serekali!

Yaani japo mi si mwelewa sana wa sheria lakini najua akifikia kwenye mashtaka mtuhumiwa atakataa kila kitu mpaka jina na akipeleka mahakamani ushahidi kwamba yeye ( mtuhumiwa) jina lililoshtakiwa sio lake, hana kesi"

Hata hao alioagiza kukamatwa kwa majina ya kihuni, watakamatwaje wakati sio wenye majina hayo!

Hao aloagiza waende central, kama ni mimi siendi" eti chid benz! T.i.d....! Ndo nani!?

Wauza madawa wakubwa raia wanawajua, sembuse vyombo vya ulunzi!? Wamuulize kikwete awaoneshe"

Mkoa wake unaongoza kwa vilaza" sijui kama analijua hili? Na labda sio mhimu kwake:
 
Huo ndio mnyororo tunataka, hata akiwa anapata kwa mtu wa nne, akionyeshwa kazi huyo mtu wa nne atataja mtu wa tatu, akionyeshwa kazi mtu wa tatu atataja mtu wa pili kwa vyovyote vile.. Katika hili lazima ukatili wa hali ya juu utumike kama itakavyohitajika!
akikamatwa mtu wa pili akiaambia amtaje mtu wa kwanza unakuta anamtaja bosi wa maconder..... na hapo ndo mwisho wa movie
 
View attachment 466457



Akitoa taarifa katika kipindi cha infomer cha clouds FM kufuatia msako wa kukamata wahusika wa madawa ya kulevya alichofanya mkuu wa mkoa Paul makonda.

Askari 9 wamekamatwa wakishirikia na wauza madawa ya kulevya Huku wasanii watumiaji wa madawa hayo wakitajwa na kutakiwa kuripoti polisi wenyewe mapema ,

wasanii waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi ni
1. Wema sepetu
2. Petiman wakuache
3. TID
4. Mr. Blue
5. Recho(kizunguzungu)

SOURCE; Clouds FM (Informer)

NB: Suala la Dawa za Kulevya limikuwa likizungumziwa na kupewa kipaombele kwa muda mrefu hapa JamiiForums. Kwa taarifa zaidi tembelea mada hii, kupata orodha ya mada nyingine nyingi zinazojadili suala hili - Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Kule Uphilipino kazi ya kumaliza madawa hayo karibu wanaihitimisha hivi karibuni
 
Hii vita ya madawa ya kulevya sio vita ndogo ,mataifa mengi makubwa bado wanahangaika nayo mpaka leo,hivyo hatua anazochukua Mh Makonda sio za kubeza hata kidogo.hatuna budi kumuunga mkono kwa kutoa ushirikiano kwani wasambazaji wamo humu humu mitaani kwetu na wanajulikana kabisa.
Kwani wewe unafikiria wauzaji serekali haiwajui!? Tatizo wananguvu sana, yaani hawakamatiki.
Na kama huamini muulize kikwete.
Yeye alikuwa na list nzima ya wauzaji lakini aliishia kusema tu! Wakamfunga mdomo hata kuiweka hadharani tu iliimshinda"

Hushangai huyu aliewataja kwa nn awataje vidagaa tena kwa majina feki!?
 
Back
Top Bottom