Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Binamu mfyuuu zako., ivi unajua hata useme nini hakuna mtoto haramu?
Heshima ya ndoa haifanyi mtoto akawa haramu.
Mfyuu zako mmeacha kujadili pwanya road mmeanza kujadili uumbaji wa Maulana.Sasa kuna imani ya watu wengine wambeya wote ni haramu unakubaliana na hilo?
Kwa comment hii ni dhahiri unanilenga mimi.Na kwanini useme kwa mafumbo? Sometimes hua sipendi ugomvi na watu ila tu basi nachokozwa mie.Fumbo mfumbie mjinga ila mwerevu atang'amua hata uweke vifundo gani.Hasa mie nifah tena....aaaaarg acha masihara bwana.
Kila mtu ana msimamo wake na kikubwa tokea jana napiga kelele na wewe jamani imani zetu za kidini hazifanani!
Kiislam mtoto anayezaliwa kabla au nje ya ndoa ni kharamu haswaaa na wala katika urithi hahesabiwi ila kama mwenye mali (baba) ataamua kumrithisa, ila matumizi na huduma zote anastahili.
Na ni kweli kua katika uislam ni dhambi kubwa kusengenya, ni sawa na kula nyama ya Binaadamu mwenzio.Haya yote yameainishwa katika Qur'an tukufu sio maneno ya nifah.
Sasa ndio maana nikasema tokea jana kua kuzini tuzini kwa starehe zetu na mimba tubebe pia?
Na pia nikaendelea kusema kua kuzaa ndani ya ndoa kuna raha yake bwana.
Sasa kama nilikukwaza bibie pole sana.
Last edited by a moderator: