Wema wangu ulivyoniletea kejeli na fedheha kutoka kwa mama mkwe uchwara

Wema wangu ulivyoniletea kejeli na fedheha kutoka kwa mama mkwe uchwara

Kama wewe ni mwanaume

1.usije ukajenga kwenye kiwanja cha mke, mama mkwe.

2.usije ukaruhusu mke au mchumba achangie ujenzi kwa hali yoyote, ata akipikia mafundi mlipe.

3.usije ukaruhusu mke aweke chochote ambacho hakihamishiki ndani ya nyumba.

4.usije ukaandika jina la mwanamke kwenye hati ya kiwanja au nyumba.

6.Mtunze sana mama na baba yako maana ndio waliokulea mpaka ukajua maana ya mwanamke.
Noted
 
Kuna akina sisi ambao wazazi walitulea kwa kutuhimiza kuishi na watu vizuri, kuwaheshimu wakubwa, tuwe na huruma.... Yaani kiufupi, watoto watiifu na wanyenyekevu bila mipaka (Nice guys)......


Ulimwengu unatuchapa sana tunapoanza maisha ya kujitegemea kwasababu haohao wazazi hawakutufundisha kuwa hii Dunia haina Huruma na binadamu hubadilika.


Tunajifunza kwa njia ya maumivu kuuelewa uhalisia wa maisha.

Pole sana mkuu, Shukuru Mungu somo limekuingia haswa.
[emoji848][emoji22][emoji22]
 
Nmewah kupitia story kama hii ndio maan kuna wakat nikikumbuka nilioyapitia kwa wanawake huwa nasema bora nile nishibe na kulala tu

Ipo siku nitaleta story yangu aliyonifanyia mama mkwe wangu....yaan mm niliacha nyumba yangu na mali zangu mying maana ningeedelea kubak pale kwangu segerea ingenihusu
Aiseee , mkuu ilete hiyo story haraka tujifunze kaka
 
Kuna funzo hapa, tusijiachie sana kwa wakwe, mashemeji, mawifi, hasa wakati wa amani na furaha, Mambo yakibadilika utapitia wakati mgumu Sana na utajuta, ( tusijiachie Sana)
 
Hapa kuna somo kubwa sana mwenye kuelewa na aelewe, kamwe sitokuja ata siku moja nikajenge kwenye kiwanja cha ukweni mana mwisho wake ni aibu na fedhea tu
Kwani mazoea utaanza kuyakalibisha vipi mpaka wakwe waanze kukwambia unjenge kwenye kiwanja chako? Ukiona wakwe wanakwambia ujenge kwao au kwenye kiwanja chao jua umeonekana dhaifu na hujielewi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna manzi nilimpata ana kiwanja cha urithi aisee tuliachana sababu alikuwa anakomaa sana tujengee kwenye kile kiwanja ila ukimwambia hati tuweke isome majina yetu wawili hataki kusikiaaa... haya mambo inahitaji kutumia akili sana
😆😅😅😅
 
Usikubali kupigwa 3-0 ndani ya dk 2 za mwanzo Kama umeshindwa kurudisha nifanyie sub tuchukue ushindi hapo
 
Back
Top Bottom