Wengi Amboa Pesa Zao Hazirudi baada ya "Kuisha" chanzo kikubwa huwa ni hiki.

Wengi Amboa Pesa Zao Hazirudi baada ya "Kuisha" chanzo kikubwa huwa ni hiki.

Joined
Jul 8, 2024
Posts
24
Reaction score
47
Nilijawa na furaha sana siku ambapo niliokota elfu nane barabarani,

Na katika utoto wangu nikaenda na kumpa mama,

Tangu hapo nikaanza kupambana sana kuwa makini barabarani ili "niokote hela nyingine 😁"

Lakini mpaka leo sijawahi bahatika kuokota hela kama hiyo,

Sidhan kwa sababu sina bahati ila ni kwa sababu "mambo yamebadilika"

Hili limenikumbusha kuhusu changamoto ambayo wengi wanaipata,

Walikuwa na pesa huko kabla,

Na kwa bahati mbaya labda hasara, kutapeliwa na mengine mengi,

Hela zikaisha na kwenye harakati za kupambania kurudisha pesa kama mwanzo,

Inakuwa ngumu kwa sababu "wanashindwa kuenenda na uhalisia wa mambo sasa"

Ni sawa na kusema leo hii unamwambia mtu awashe moto kwa kufikicha vijiti,

Ni kweli jana waliweza kupata pesa za kutosha ni kwa sababu fulani,

Labda ni bidhaa mpya sokoni,

Au ni ujuzi fulani ambao ni wewe pekwe ulikuwa nao,

Au ni ukaribu ambao ulikuwa nao na viongozi fulani na hivyo ukapata pesa hizo,

Lakini kutaka kutafuta pesa kwa namna hiyo hiyo na bila kujua "uhalisia wa mambo upoje sasa"

Na uhalisia wa mambo ulikuwaje kipindi kile mpaka ukawa tajiri?

Maana huwa wanasema "mi mbaya sana kuwa na mafanikio na usijue kwa nini umefanikiwa"

Maana siku nyingine unaweza filisika na ukadhani ulijua siri na kumbe hukuwa unaijua,

Hivyo,

Ni ngumu kwa wengi kutoka kwa sababu ya ile hali ya "kukariri maisha"

Yaani kukariri njia yao ni ile ile na haibadiliki hata wakifilisika bado watainuka,

Mwisho ni kuishia kuteka na kusota sana bila maendeleo yoyote ya maana.

Kama unajua unapitia hali kama hii yani kurudisha pesa zako,

Au ni kwamba siku za mbele unatamani hata ukifilisika ujue unainukaje

Zingatia hili;

Nenda na uhalisia wa mambo kwa sasa na kqamba unatumiaje rasilimali zako kwa ubora kulingana na "uhalisia ulioupata".

Mpaka wakati mwingine kwa heri.
 
Pesa haina fundi, ikiamua kukusaliti inakusaliti tuu. Ikiamua kuja inakuja tuu.
Umemaliza kila kitu.
Leo unaweza kulima ukaivisha ukakuta bei nzuri sokoni na ukapiga pesa hatare. Ukirudia kinakulamba hadi unajutia.

Unaweza kufanya biashara ikakupa faida ukajiona mwamba. Unaenda badaye unakula hasara ya mwaka..

Kwenye uvuvi , migodini, ufugaji.

Tusiwe washauri sana wakati Mwingine ni mapenzi ya Mungu tu
 
Umemaliza kila kitu.
Leo unaweza kulima ukaivisha ukakuta bei nzuri sokoni na ukapiga pesa hatare. Ukirudia kinakulamba hadi unajutia.

Unaweza kufanya biashara ikakupa faida ukajiona mwamba. Unaenda badaye unakula hasara ya mwaka..

Kwenye uvuvi , migodini, ufugaji.

Tusiwe washauri sana wakati Mwingine ni mapenzi ya Mungu tu

Ndio hivyo mkuu.
 
Back
Top Bottom