Wengi bado hawajaelewa maana ya kuunganishwa NIDA-INEC-CCM, Mwabukusi aelimishwe

Hapo ndipo INEC ilitakiwa kutolea majibu juzi kuhusu suala la Polepole.

1) Wapiga kura wanapohakiki majina yao kwenye mfumo, hiyo ni manual au digital? 🤣🤣🤣

2) Huo mfumo ukoje na umekashimiana (integrated) na mifumo ipi mingine?

3) Alisema mwenyewe anataka kumsikiliza Polepole. Maana yake hana uelewa sahihi katika hili.

4) Je anaudanganya umma au ni kweli hajui kwamba mifumo ya uchaguzi imekashimiana na ile ya CCM?

5) Anapaswa aseme ni wakati gani kura zinaweza kuibiwa - ni wakati wa kupiga kura tu au hata kabla na baada ya zoezi?

6) Kujinufaisha kwa kuingilia mifumo ya NIDA & INEC kabla ya zoezi la kupiga kura, si wizi huo?

7) Uchakataji na majumuisho ya matokeo ya mwisho pia hufanyika kidigitali (rejea kauli ya Mwabukusi jana).
 
Acha hisia, tumia logic tu ndugu,, unachokisema ndo uhalisia ila hakiwezi kufanyika na unajua kwanini..
Nani aunde kamati?
Halafu hiyo kamati ikamchunguze nani?
Halafu huyo mwalifu akashtakiwe wapi? Na nani?
Yaani unataka mtu aunde tume ije imchunguze yeye mwenyewe na yeye mwenyewe ajishtaki ...
Kwani si unafahamu hiyo show inaendeshwa na nani?
 
Rais wa TLS katika issue ya NIDA, INEC na CCM alitakiwa akae kimya awaachie wenye utambuzi wa IT na sayansi ya computer.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (Ibara ya 74–74E) inaunda Tume ya Taifa ya Uchaguzi na inataka tume iwe huru na isiyoegemea upande wowote.

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na Sheria ya Serikali za Mitaa (Uchaguzi), Sura ya 292 zinaweka masharti ya maadili na wajibu wa watendaji wa uchaguzi.

Kanuni za Maadili ya Uchaguzi (Electoral Code of Conduct) – zinawataka wasimamizi wa uchaguzi na watumishi wake kutokuwa na ushirika wa kisiasa, kutovaa nguo zenye alama/sare za chama au picha za wagombea.
 

I don't believe you.

According to Polepole, the fully integrated system of CCM+NIDA+INEC has one main goal - RIGGING the election results before hand.

Kisha hayo matokeo yaliyopikwa kwenye mifumo hiyo yanamwagwa accordingly katika vituo vya kupigia kura.

Mifumo inawanufaisha kwa kubalance voter turn out, distribution of fake votes, identifying dormant voters, non voters, etc.
 
Hapo ccm washitakiwe, je wanashitakiwa na nani? Serikali ndio ccm na ccm ndio serikali
 
kwa ufupi ni kwamba, yale makura feki yanayo kamatwa huku na kule wakati waa uchaguzi ni kura za wale waliosusa kujiandikisha. CCM inapata details za toka NIDA hivyo kuandaa idadi ya kura husika na kuzitawanya maeneo mbalimbali inchini ili ziingizwe kwenye vituo, ndo maana kuna voting posts nyingi mawakala wa upinzani hufukuzwa vituoni, na kunakua na matukio huku na kule ya kura feki
 
Lakini anachokisema Mwabukusi "kisheria" ni sahihi. Sheria ni kitu kingine, amejibu vizuri.
 
Hapo ccm washitakiwe, je wanashitakiwa na nani? Serikali ndio ccm na ccm ndio serikali
Is why reforms zinahitaji kuanzia sheria mama(katiba) na kuendelea
Else zitabaki stories
 
Is why reforms zinahitaji kuanzia sheria mama(katiba) na kuendelea
Else zitabaki stories
Watawala awataki reforms ila wananchi ndio muda wa kuamka sasa, mtu yoyote ambaye yupo pamoja na wanachi haijalishi alifanya nini huko nyuma ni wakuunga mkono.
 
Advocate Mwabukusi mwenyewe amethibitisha jana kwamba mchakato wa uchaguzi wetu ni BOTH MANUAL & DIGITAL.

INEC inawazuga Watanzania kwamba ni 100% manual. Hilo ni kosa tayari. Anaficha nini?
mwambukusi nimemwelewa kuwa unaandikishwa kielectronic, kwa maana kwamba unaweza kujiandikisha kigoma ukaja dar uka update taarifa zako na ukapiga kura dar, lakini pia networking ya inec na nida ni kuzuia watu wasiokuwa na sifa kujiandikisha mfano watoto na wasio raia. tatizo nida hawana data za wasio kuwa na akili timamu. najaribu ku map wizi wa kura nandatabase ya nida hapo sipaoni!
 
hiyo namba saba hebu dadavua
 
Hili haliwezekani bila kuongeza idadi ya maboksi ya kura feki otherwise idadi ya wapiga kura iliyoibiwa kutoka kwenye mifumo haitataly na makaratasi ya kura yanayohesabiwa manualy mbele ya mawakala. Unless kusiwe na mawakala wa kuhakiki ni karatasi ngapi za kura zimepigwa.
 
Mkuu mfumo unaonekana umeratibiwa kisawasawa - yaani hata ukiwekwa autopilot unaweza kujiendesha na kufanya kazi yake effectively & efficiently.

Kuna mdau juzi kati hapa alizungumzia uwepo wa kura feki na vituo feki.

Unadhani hivyo viko kwa lengo la kufidia nn, kama siyo kubalance sheet?🤣🤣🤣

Case Study: Advocate Mwabukusi rais wa TLS ameweka wazi jana jinsi ambavyo yeye kama mgombea ubunge alishuhudia maboksi ya kura yamejaa pomoni licha ya yeye kuwa mpiga kura wa kwanza kufika hapo kituoni.

Connect the dots by sketching the corresponding graph!😂😂😂
 
Hata sijaelewa hii kitu kwawengi NI ngumu kuelewa yaani idea hapo ikoje ilihali kila kituo kura zinahesabiwa kwa mkono na hata baadae mawakala wanaruhusiwa kujumlisha kura kila kituo zilizopatikana
za tz nzima zinajumlishiwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…