Wengi hatuna utamaduni wa kula matunda na kunywa maji.

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Salamu.Watanzania wengi wanaishi vijijini. Nahuko matunda ni mengi lakini husafirishwa kwenda mijini.
Matunda kama embe zinaonekana ni kwa watoto.
Ndizi mbivu wengi huzidharau kwamba chakula cha nyani.
Watu wa mijini wanajitahidi kula matunda sana.
Watu wa vijijini hasa wanaume wakienda mijini wao huona kuchoma nyama ndio muhimu zaidi
Mtu anabanwa na kiu badala anywe maji ananunua soda au juice.
Wen zetu mbele naona wao wanajali matunda na mboga mboga.
Kwetu huku mtu kununua mboga za majani hataki anaona ataonekana hana hela ya nyama au samaki.
Siwapangii watu namna ya kuishi ila ni ushauri.
Matunda huimarisha kinga na afya zetu .Yanapoibuka maradhi ya kuambukiza kwa kasi mfano Corona huenda ukaokoa maisha yako dhidi ya mashambulizi
 
Hamna bwana...matunda yapo, yanaweza kuwa usiyoyazoea. Huwezi kutegemea kukuta parachichi na mapeasi dodoma/singida. Unatakutana na zambarau, sasati nk. Mbona wanakula sana tu
 
Wababa wengi huenda hawali. Zaidi watoto
 
Juzi nilishangaa mwanamke mmoja kaja kijiwe cha kula matunda naye kaagiza sahani akala huku wanawake wenzake wakipita kana kwamba hawaoni kuna matunda yanauzwa yakiwa yameandiliwa tayari kuliwa
 
Yaani mi niache kunywa bia ninywe maji? We jamaa vipi? Na leo simba ikishinda mtaniokota mtaroni ntalewa mbaya mbovu..¡¡¡
Lakini kumbuka ipo kiu ya maji. Bia kwani si starehe ya muda tu?
 
Tatizo watu wengi hawana elimu ya lishe bora, wengi wanakula ili washibe, kutimiza hamu, hawana ratiba ya chakula

40%+ ya watoto wa Tz wamedumaa haijarishi mtoto wa geti kali au wa uswahilini
 
Ulaji wa matunda kwa kweli unasaidia mwili kufanya kazi yake ipasavyo. Matunda kama ndizi mbivu, machungwa, ndizi, embe, nanasi, tikiti, parachichi yana matokeo mazuri mwilini
 
Tatizo watu wengi hawana elimu ya lishe bora, wengi wanakula ili washibe, kutimiza hamu, hawana ratiba ya chakula

40%+ ya watoto wa Tz wamedumaa haijarishi mtoto wa geti kali au wa uswahilini
 
Kuna hawa watu wanauza matunda mchanganyiko sahani 2000 ila mara nyingi nawaonaga na kuwapuuza. Ila ni watu muhimu sana
wengine wanauza sahani ya matunda buku tu unakula matunda mchanganyiko mpaka unashiba. Ila kuna madaktari wanaona kula matunda mchanganyiko kwa wakati mmoja si vizuri, wanataka ule tunda aina moja tu kwa wakati mmoja na sio uchanganye matitkiti, maembe, mapapai, maparachichi, mananasii na machungwa kwa wakati mmoja
 
Mkuu una hoja nzuri saana ila lengo lako lilikuwa ni kuwadharau watu wa kijijini kuwa wakifika mjini wanashobokea soda badala ya maji, nyama badala ya matunda ila mimi nimekaa kijiji na hata hapa nipo kijijini naomba nikupe maisha yetu ya kila siku kwa ufupi saana.
1. Sisi huku kijijin kula mboga za majani ni sehemu yetu ya maisha nyama ni kwa wale wenye uwezo tu.
2. Kuna vijijini matunda hayanunuliwi tunaanza na msimu wa maembe kisha mapera, parachichi, huwa hatununui unajichumia tu kwa matunda kama ndizi ndio utanunua kama hujalima.
3.kuku kwetu huku tunawala wale ambao hata chanjo ya ndui hawaijui

Sasa sijajua kwanini umeamua kutunanga sisi wa VILLA
 
Huenda wakawa na mantiki kubwa hasa kwenye mfumo wa umen'

Sijawananga. Chunguza hapo kijijini kama wababa wanapenda matunda?
 
Back
Top Bottom