Wengi hatuna utamaduni wa kula matunda na kunywa maji.

Mi huwa nashangaa wauza matunda mchanganyiko wanaoweka kwenye sahani kwa nini huwa hawaweki epo na zabibu wakati zipo hapo hapo kijiweni kwao sambamba na matunda mengine? Epo na zabibu hawachanganyi
 
Mi huwa nashangaa wauza matunda mchanganyiko wanaoweka kwenye sahani kwa nini huwa hawaweki epo na zabibu wakati zipo hapo hapo kijiweni kwao sambamba na matunda mengine? Epo na zabibu hawachanganyi
Bei huenda na pia huangalia customers preferences
 
Matunda kama embe zinaonekana ni kwa watoto.
Enzi hizo tulikua na ligi za maembe hasa msimu wa maembe unakuta kila mtoto na kitoto ndoo chake kimejaa maembe, nilikua nakula maembe vibaya mno. Ila utoto raha sana 🙌
 
Mijini kuna familia zina utamaduni wa kula matunda katika milo yao mikuu kama mlo wa mchana na mlo wa usiku lazima matunda yawepo yaliwe sambamba na ugali au wali hata kama ni kipande cha tunda. Ndizi moja inaliwa na watu wawili au chungwa moja mnakula wawili. Huwezi kula tunda zima peke yako ndani ya familia hiyo labda ukale mitaani
 
Hata mimi nilipata kusikia ila inafikirisha...
 
Familia nyingi hazina utamaduni wa kula matunda sambamba na milo mikuu miwili ya mchana na usiku. Matunda yanaliwa kiholela mtu akijisikia kula embe, chungwa, ndizi anakula hukohuko mitaani, habebi akale nyumbani sambamba na ugali|wali wake. Bora wale wanaenda kijiweni kula sahani nzima unashiba kama mlo mkuu
 
Juzi nilishangaa mwanamke mmoja kaja kijiwe cha kula matunda naye kaagiza sahani akala huku wanawake wenzake wakipita kana kwamba hawaoni kuna matunda yanauzwa yakiwa yameandiliwa tayari kuliwa
Huyo amekula sababu ya njaa wala si kwa umuhimu wake
 
Kuna hawa watu wanauza matunda mchanganyiko sahani 2000 ila mara nyingi nawaonaga na kuwapuuza. Ila ni watu muhimu sana
janabi akikutana nao hao anawafunga jela.

haishauriwi kuchanganya matunda yenye sifa tofauti kwa mlo mmoja,au juice mtu katia parachichi,passion na embe humo humo.
 
wanasema kila tunda lina virutubisho yake, wanasema ukila matunda mengi tofauti kwa wakati mmoja hayatameng'enywa yote, tumbo litashindwa lianze kumeng'enya tunda lipi
Hapa nimejifunza kitu
 
Mi huwa nashangaa wauza matunda mchanganyiko wanaoweka kwenye sahani kwa nini huwa hawaweki epo na zabibu wakati zipo hapo hapo kijiweni kwao sambamba na matunda mengine? Epo na zabibu hawachanganyi
zipe pacel huwa ni 1000/1500/2000

ukitia zabibu au apple tayari inabidi isome 3000 kuendelea,naonaga hawa wa 2000 huwa wanatia kipande cha apple.
 
Pamoja na madaktari kuona ulaji matunda mengi kwa wakati mmoja si mzuri, inabidi tule tu. Ni kupunguza bajeti ya kununua matunda mazima mengi, ubebe tikiti, embe, chungwa, nanasi, papai, tango, parachichi, ndizi ongeza zabibu na epo ni bajeti kubwa wakati buku au buku jero unakula yote hayo kwa gharama ndogo,japo ni vipande vidovidogo sahani moja inatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…