Wengi hawajui siri zilizopo ndani ya vitabu hivi vya dini, yaani Biblia, Quran na Tanakh

.Ukiwa na imani kama punje ya haladali unaweza ukauambia mlima huu ng'oka na unang'oka.
Haya nenda kauambie mlima Kilimanjaro ng'oka kama utang'oka.

"Nami nitakuonya mali zilizofichwa gizani" ni hazina zipi hizo?

"Akupigae shavu la kushoto mgeuzie na la kulia " Haya we tega shavu lako uumuke manundu.

Vyote ving'aavyo fedha na dhahabu ni mali ya Bwana" still bado wengi ni masikini.

Hizi ni baadhi tu
 
Hiyo mbn code nyepesi sana

Maaana ake shtuka mwanateolojia utapigwa kweupeee kama kitambaa Cha sanda,😆😆
 
Uyahudi sio dini kubwa duniani, dini ya tatu kwa ukubwa baada Ukristo na Uislamu ni Ubudha na Uhindu.

Uyahudi ndio Dini kubwa au foundation ya Dini ya ukristo na uislam

Kutokuwa na waumini wengi hakuifanyo uyahudi isiwe Dini Kubwa.

Kuna tofauti ya wingi wa watu na ukubwa.

Hizo Dini ambazo ni ukristo na uislam ukitoa maudhui ya kiyahud hazina Ziada yoyote Ile.
Na huo ndio ukubwa wa Dini ya kiyahudi

Ila uyahudi hautegemei Dini zingine.

Ni kama ubudha na uhindu.
 
Zipo kwa wisemen illuminated people nyie wa level ya kwanza ya ufahamu inatakiwa muishie kwenye kuhudhuria tu ibada na kufukuza mapepo tu.
Hizi level zingine za ufahamu ya pili na ya tatu kwa wanaozama kwenye theory ndo wanazivunja vunja hizo codes
Nimewahi kuingia pale Masonic Lodge,posta , mule ndani Kuna Biblia, Quran,na kitabu Cha Seleman
 
Hizo siri unaanza kuchambua muda gani mkuu
 
Kuna muda ni bora ubaki uamini kile unachokiamini.
Kuna watu waliopitia matatizo makubwa na wakapona kupitia biblia na Quran hawa huwambii kitu kuhusu imani.
Lakin wale ambao hawajapitia matatizo na kukimbilia huko wana imani ndogo sana.
Lakini swali la kujiuliza kwanini wale waliosoma mpka elimu ya juu kuhusu imani (theolojia) kwanini washindwe kung'amua hizo codes ili waweze kusema ukweli?
 
Kiukweli Mimi sijasoma theolojia Ni muumini wa kawaida kabisa lkn wakushika sheria za Mungu. Ni mmoja wa watu ambao wameona mambo makubwa Sana na ya ajabu. Ni mtu ambaye kiukweli huniambii kitu kuhusu dini yangu kutokana na Mambo ambayo nimeyashuhudia na huwa nawashangaa watu wanaoponda biblia eti Ni hadithi za watu. Sielewi Sasa hii imekaaje.
Na bahati mbaya Sana watu Hawa huwa hawaelezi kwaundani kujiridhisha juu ya madai yao. Najaribu kuendelea kupeleleza kuona Kama kunamtu atakuja na hoja itakayopenya kupasua ngome ya imani yangu lkn wapi, zaidi tu utasikia ooh! Mmeshikiwa akili. Ooh! Mungu hayupo. Duh!
 
Una
Una hoja ndugu, usikilizwe..!
 
Binti yangu kwanini una chuki mno na wakristo walikufanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…