Wengi hawajui siri zilizopo ndani ya vitabu hivi vya dini, yaani Biblia, Quran na Tanakh

Zipo kwa wisemen illuminated people nyie wa level ya kwanza ya ufahamu inatakiwa muishie kwenye kuhudhuria tu ibada na kufukuza mapepo tu.
Hizi level zingine za ufahamu ya pili na ya tatu kwa wanaozama kwenye theory ndo wanazivunja vunja hizo codes
Siri nyingi ni siri kweli kweli.. hata ukizijua huwezi simulia mtu.. maana zinakua above normal understanding.. vinginevyo utazua taharuki mtaani
 
" imeandikwa jino kwa jino" nami nakuambieni akupigae shavu la kushoto mgeuzie na kulia" " watendeeni mema wote wanaokuudhi, usilipe wema kwa ubaya" kisasi ni juu ya Bwana".
Haya ni mafundisho na yamebeba maana nzima ya siri ya mafanikio kuanzia uponyaji nk
 
Mtume Paulo alishauri kuwa mtu akitaka kuishi bila matatizo yoyote basi asioe au asiolewe. Soma{ 1wakorintho 7:28 Lakini,kama ukioa,huna hatia;wala mwanamwali akiolewa,hana hatia; lakini watu hao watakuwa na dhiki katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo}.

Maandiko hayo 👆👆inaonyesha wazi mtume Paulo alifahamu wazi kuwa ndoa siyo chanzo halisi cha furaha wala amani.Hivyo kuoa au kuolewa japo ni jambo la baraka;lakini siyo chanzo cha furaha, upendo wala amani ya kweli.

Ndiyo maana wanandoa wengi wana maumivu makubwa sana na hawana furaha,upendo wala amani ya kweli.Wanaishi kama wako tu kwenye gereza la mahusiano kwa sababu wana watoto na wakati mwingine utegemezi wa kiuchumi.Wengine ktk ndoa wamepata magonjwa na misongo ya mawazo na ulemavu uliotokana na vipigo kutoka kwa wenza wao wa ndoa.

Kwa hiyo siyo sawa kuingia kwenye ndoa kutafuta furaha,upendo wala amani. Ndoa haina vitu hivi vyenye thamani sana maishani. Mke au mume hawezi kukupa vitu hivi;ila anaweza kujitahidi kwa namna fulani tu.
 
Mtoa mada , kwanini usisimamie unachoamini? Acha kila mtu ajae na Imani yake. Dini zitafarakanisha watu sana humu.
 
Biblia inaruhusu talaka lakini andiko hili hatuwafundishi watu watalitumia vibaya kuwaacha wake zao.
Maandiko yapo " mwanamke mpumbavu anastahili talaka" Hizi ni siri laiti wanawake wa Kikristo wangejua siri hii wasingewasumbua waume zao kwa kigezo cha Hakuna kuachana my foot.
Kama MUNGU alishindwana na shetani akamtimua sembuse wewe mwanadamu kuweza kuishi na ajent.
Mpumbavu aombewi labda uwe Yesu.
 
Mzee wa Code Nakupa Challenge moja The redemeer
Kama Utaiweza Nitajua Kweli Wewe Code Umeishika na Unajua Code Vizuri sana zilizopo kwenye Bible..

Niambie hii code inamaana Gani..
The coount down Starts Now..

Kutoka 20:4-5

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,


Masharti hakuna Tumia Lugha au Tumia Maarifa Yoyote UjibU hii code
 
Miswahili bwana,badala ya kusoma mambo ya maana mnapoteza muda kwenye hekaya za abundantly!!!
 
Hakuna kitabu cha dini kinachoitwa Biblia leta andiko linalotambua kuwa kuna kitabu kinaitwa biblia
Ubishi mwingine hauna maana yoyote. Kwa uelewa wako Biblia ni nini?
Nini kinakupa uhalali wa kusema hakuna kitbu kinachoitwa Biblia wakati kinaonekana na kusomwa na watu?
 
Kaka nisaidie kujua code kaka
 
Siri kubwa kwenye vitabu tajwa ni ukoloni na unyonyaji wa jamii zilizoandika vitabu husika kuzinyonya na kuzitawala jamii zilizovipokea na kuviamini wakati ni ngano za utamaduni wa jamii zenye vitabu hivi. Hamna jambo kubwa la maana kwa watawaliwa na walioaminishwa zaidi ya kuwafanya wasijitambue na kujikomboa. So simple.
 
Kaka nisaidie kujua code kaka
Code Nzima Inahusika na DNA and Genetic make up na Sio kitu kingine..yaani Kwa Kifupi ni Jinsi Tabia au Character zinavyoweza kurithishwa Kutoa Kizazi kimoja mpaka Kingine..

Natamani Kueleza Mengi ila Ngoja Nieleze Vichache ili Kama Utakuwa una swali uniulize Nieleze Zaidi..Natamani Tuende kwa maswali zaidi

DNA Hurithisha Tabia au Effects Mpaka Kizazi cha Tatu na Cha nne Baada ya Hapo DNA Halisi ya Mwanzo yaani ancestral DNA huwa haiathiri chochote Kwenye Kizazi kuanzia cha Tano na Kuendelea..

Lets Break vizuri Ulinielewe..
Ukisoma Kitanu cha David Reich's kinachoitwa "Who we are and how we got here" kuna graph Inaeleza Hivi "The more we go back in our ancestors generations, the least we have chances to have any DNA inherited from one of these ancestors"

unajua kwanini "because the number of ancestors is doubling every generation while the number of stretches of DNA is only increasing by 71."

Najua Nikisema Hivyo Nitakuwa naweka Ugumu zaidi au..

LEts make it easy sasa..


Au Ngoja Niweke Hii Kabisa..

Kuna Kitu Kinaitwa centimorgan (cM) ni genetic measurement ya estimation ya distance between genes or markers on a chromosome..

Sasa Hii inasema Kwamba Ubora wa Genes Huweza Kulindwa Kwenye Vizazi Vitatu mpaka Vinne zaidi ya Hapo Haiwezekani..

Natamani Unielewe zaidi..


Umeona Hapo Yaani Babu yako Kuanzia kizazi cha Tano anachangia Kiadsi cha 3.12 tu ambacho ni sawa na Hakuna Mchango wowote..

Sasa Lets Break down..



Sasa Lets go Kwenye Fungu Husika..

Kutoka 20:5
[5]Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

Thou shalt not bow down thyself to them, nor serve them: for I the LORD thy God am a jealous God, visiting the iniquity of the fathers upon the children unto the third and fourth generation of them that hate me;

Imagine umeanza Kuvuta Sigara Sasa Hivi Nakuapia Kuwa Effects za Sigara zitaanza na wewe Mpaka kizazj chako cha Nne kitakapofika Ila tu kama Mwanao naye hatavuta ila mwanao baye akivuta mpaka Kizazi cha nne Pia..


Hiyo ndo Ilikuwa na Maana Ya Amri Hiyo hata amri kumi haimaanishi eti ni amri kama zinavyosemwa..

Sasa Nakaribisha Maswali ili nieleze Kupitia maswali.zaidi
 
Hata wao wanatumia vitabu hivyo huko wanamkoloni nani
 
J
Hata mimi the great genius sina uwezo wa kufumbua mafumbo magumu? Ninao uwezo huo kwa dini zote za ukweli na za uongo nitafumbua fumbo zake.
 
Hata wao wanatumia vitabu hivyo huko wanamkoloni nani
Wanawakoloni wasiomilki hivyo vitabu ambavyo vinaongelea mambo yao na si ya hawa wanaowakoloni. Mfano mdogo, inakuwaje Waswahili wapewe majina ya kigeni au kwenda kupoteza fedha ugenini kwa kisingizio cha kuhiji wakati ardhi na dunia yote viliumbwa na Mungu baada ya kupendezwa navyo? Mbona hili jambo ni rahisi kuliona na kulielewa usipofungia akili yako kwenye imani kibubusa?
 
Asante sana kaka, kwakweli mimi sina swali kwa sasa zaidi ya kuitaka hii elimu zaidi. Kama hutojali ningependa kupata ufahamu zaidi kupitia wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…