Wengi tungeswekwa magerezani awamu ya tano wakati Serikali inataka IP adress za accounts zinazoikosoa, tunashukuru JamiiForums mlitusimamia

Kuna wapuuzi walinifuata PM na kujifanya kunitisha, wengine kunirubuni na wengine kunitisha hadharani hapa jukwaani. Mungu mwema hatukubadilika.
Ajabu ni kuwa usiwaamini sana kuwa wahusika vingine ni vitoto vimo humu kazi ni kujiita usalama uchwara .

Vikikufuata ukavieleza kuwa uko tayari vikutafute vinaishia mitini kimoja kikasema nakupa namba tuzungumze ili nikueleweshe nikakipa namba makusudi .

Ooops , eti kananipa mikwara mara kanajua nilipo mara kanaweza kunidaka mda wowote kakiamua nikaamua nikavunjie heshima nikahack siku mbili nikaja jua hajatumwa ila kazi kutaka kujimwambafai na mwisho ni askari polisi hapo Chang'ombe .

Nilicheka sana maana hata cheo kielimu hakana kapo tu na V mbili kakadhani maisha kamemaliza .

Nikasema wacha nikatese pia nikatafuta namna nikameet nako nikakaeleza ujinga kanaoufanya kakaishia kucheka tu na kusema sorry bro ni kufurahisha genge .

Nowdays sikaoni Jf kama una ID mpya stop doing that ujinga utakuja kukukost bwana mdogo .

Pona yako ni kuwa ulikuwa ni chapombe mwenzangu ila bila hivyo ningekuchezesha kinungenunge .

Ninyi akina Chabrosy na nokwenumuya kaeni vizuri na vitoto vyenu viishi katika misingi ya kazi na ethics zenu.
 
Shujaa my .,...
 
Kuna mamluki waliingia humu ikawa ukisema kitu negative cha serikali uzi unafutwa chap kwa kasi ya radi.

Walikuwa wanakera balaa naona walitolewa hao mods maana amani imerejea. Saa hii tunaiponda serikali kwa raha zetu.

Tena nimemiss kuponda serikali ngoja niwaponde kidogo

Serikali ya Tanzania na chama chao cha mapinduzi kudadadeki zenu mbuzi nyie. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nilishaona jina langu la ukoo humu wakijadili kile nilichoandika,asidanganywe mtu kwamba wakitaka kutujua ha
awawezi
 
Naunga mkono hoja

Retired angepata tabu sana [emoji38][emoji38]
Wewe ulikua unakera sana kipindi cha Awamu Ya 5. Yani ulikua unakera kweli kweli! Pamoja na ISIS, fimboyaasali Ghosryder Edvart na Pasco.

Najiuliza hapa eti unaunga mkono hoja? Sijui unaunga hoja kwa kutumia kiungo gani, labda matarcaaal!!!
 
Hivi yule kijana aliyepicha picha nyufa za hostel alimaliza masomo chuo au walimfanyia figisu?
Abdul Nondo yupo humu! Na alimaliza kitambo tu masomo yake! Na kwa sasa analamba asali kwenye chama cha Mkigoma mwenzake Zitto, cha ACT Wazalendo, kama Kiongozi wa Jukwaa la Vijana!

Nilimuuliza anipe ukweli wa ile story yake ya kuokotwa asubuhi kwenye misitu ya Sao Hill kule Mafinga Iringa, mpaka leo ametia ngumu! Nakumbuka Mwigulu alimvalia bango, mwisho wa siku na yeye akaangukia pua! Dogo alifutiwa mashtaka na mahakama, ya kujiteka mwenyewe!! Ila enzi zile!! Mambo yalikuwa si mambo.
 
Jamaa pia lazma alikuwa anapitapita huku kama maza..sipati picha alivyokuwa anapata jazba hadi anahis kufariki
Kwani hukumsikia mwenyewe aliposema anatamani kuzima mitandao yote?

Wakati anaiba kura uchaguzi batili wa mwaka 2020 alituweka wiki nzima bila internet.

Yani yule Ibilisi asipokwenda motoni basi Mimi Nina uhakika wa kwenda peponi moja kwa moja.
 
Kabisa Mimi nilikuwa namba Moja kwa wakosoaji wa Mwendazake humu jf.
 
Kipindi kile wakosoaji walikuwa wanaitwa wapiga dili na wenye vyeti feki! Hali ilikuwa si hali. Waimba mapambio (MATAGA) walikuwa ndiyo wametamalaki humu jukwaani.

Sasa hivi, wengi wao wamejikatia tamaa baada ya kutoswa kwenye mfumo wa ulaji.
Saizi wanaomkubali mama tunaitwa walamba asali 🀣🀣🀣🀣

Ila tunasonga mbele na kuwapuuza.
 
Kuna wapuuzi walinifuata PM na kujifanya kunitisha, wengine kunirubuni na wengine kunitisha hadharani hapa jukwaani. Mungu mwema hatukubadilika.
Hata Mimi waliowahi kuja,those days sikuwa naanzisha mada ila kuchangia tuu tofauti na Sasa..

Kuna Jamaa waliowahi kutishia Hadi kutafutiza picha yangu 😁😁😁😁 wako kule jukwa la Nairobi vs Dar huwaambii kitu kuhusu Mwendazake 😜😜

Ila wamehangaika na mimi muda mrefu sana but saizi wametuliza nyapu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…