Wengi tungeswekwa magerezani awamu ya tano wakati Serikali inataka IP adress za accounts zinazoikosoa, tunashukuru JamiiForums mlitusimamia

Wengi tungeswekwa magerezani awamu ya tano wakati Serikali inataka IP adress za accounts zinazoikosoa, tunashukuru JamiiForums mlitusimamia

Mimi nilishaona jina langu la ukoo humu wakijadili kile nilichoandika,asidanganywe mtu kwamba wakitaka kutujua ha
awawezi
Wanaweza but Ile Nguvu ya kufanya hivyo Kwa sasa haipo kama kipindi kile tulipona ni wazi Kwa Sasa sio ishu wamebakia kufura Kila legacy inapoguswa 😆😆
 
Hata Mimi waliowahi kuja,those days sikuwa naanzisha mada ila kuchangia tuu tofauti na Sasa..

Kuna Jamaa waliowahi kutishia Hadi kutafutiza picha yangu 😁😁😁😁 wako kule jukwa la Nairobi vs Dar huwaambii kitu kuhusu Mwendazake 😜😜

Ila wamehangaika na mimi muda mrefu sana but saizi wametuliza nyapu.
Nyapu??
 
Maxmeello angeunga Mkono Juhudi watu Wazito wazito waliomo humu wangeteketea sana
 
Wewe ni mnafiki Sana.
Kama Siasa haina Unafiki Chadema wasingechukua ruzuku ambayo asilimia kubwa kwenye ile 17% ilitoka Bunda, Tarime Mjini, Kawe, Tabora na Nkasi kwa akina Covid-19 na Aida

Tundu Lisu: Misimamo ya kisiasa siyo Sheria za Mussa zilizoandikwa kwenye Mawe!
 
Watu wengi walioingia kwenye mikono ya wasiojulikana wamekuwa kama mabubu kwa yaliyowakuta au wanatoa story ambazo haziunganiki, sijui nini kiliwapata nyuma ya pazia! Inasikitisha sana.
Abdul Nondo yupo humu! Na alimaliza kitambo tu masomo yake! Na kwa sasa analamba asali kwenye chama cha Mkigoma mwenzake Zitto, cha ACT Wazalendo, kama Kiongozi wa Jukwaa la Vijana!

Nilimuuliza anipe ukweli wa ile story yake ya kuokotwa asubuhi kwenye misitu ya Sao Hill kule Mafinga Iringa, mpaka leo ametia ngumu! Nakumbuka Mwigulu alimvalia bango, mwisho wa siku na yeye akaangukia pua! Dogo alifutiwa mashtaka na mahakama, ya kujiteka mwenyewe!! Ila enzi zile!! Mambo yalikuwa si mambo.
 
Kuna kipindi hapo awamu ya tano palikuwa na mtafutano mkali sana baina ya vyombo vya ulinzi vilivyopewa task ya kukamata wana jf hasa wa jukwaa la siasa wanaokosoa serikali.

JamiiForums ilianza kushinikizwa itoe anuani za "ip adress" za wanachama

Ili uelewe kirahisi ip daress ni kwamba tunavyopiga simu ama kutuma meseji namba zetu huwa zinarekodiwa kwenye simu za watu tuliowapigia pamoja na kwenye rekodi za mitandao ya simu, hizi namba mfano wake ni 0769xxxxx. Basi na kwenye internet hakuna utofauti sana ila huku namba za utambulisho zinaitwa ip adress mfano wake huwa ni 192.268.xxx.xxx, hizi namba hazijirudii kama ilivyo kwa namba za simu kila mtu ana yake, ukitaka kuijua ip adress yako tembelea >> hapa B]

ukitembelea tovuti yoyote mfano jamiiforums. com, mitandao ya simu itaona kwamba ip adress inayotumika kwenye simu yako imetembelea jamii forums lakini hawawezi kujua account unayotumia.

Kwa upande wa system za tovuti za mitandao unayotembelea kama jamiiforums, wao ndio wenye tocuti na wanaweza kujua ip adress inayotumika na mtu mwenye account lakini hawana uwezo wa kujua namba ya simu ya anaeitumia hio ip adress. kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba ili mtu afahamike inabidi jamiiforums na mitandao ya simu waungane, Yani mtu wa humu jamiiforums atoe ip adress inayotumika na account mwanachama kisha hio ip adress ikifika kwenye mitandao ya simu wao ndio watajua inatumika na namba ipi ya simu, na hapo utajulikana kirahisi.

Sasa kilichotokea enzi hizo ni kwamba tayari kule walikuwa na access ya kujua namba za simu zinazotembelea jf na wanauwezo wa kumjua mtu endapo jf wakitoa ushirikiano, na ndio hapo sasa jamiiforums wakawa wanafatwa kutoa ip adress zinazotumika na accounts kadhaa ili kuweza kuwatambua ni kina nani wanaikosoa serikali.

Palizuka patashika na tafrani humu ndani isiyo ya kawaida hasa ukizingatia ile awamu ya tano ilikuwa haina masihara na wakosoaji.

Ponea yetu swala hili liligonga headlines kwenye vyombo hata vya kimataifa na hili lilikuwa ni shambulizi ka privacy za watu mitandaoni, si kitu kidogo hiki na tunashukuru Jf, balozi za nchi za nje na asasi kadhaa waliweza kulipiga vita, haikuwa rahisi nakumbuka kesi zilikuwa zinapelekwa mtwarea huko na figisu kibao tu na baadhi ya viongozi wa jf walikatazwa hata kusafiri nje ya mkoa

Hii ilipelekea kuongezewa baadhi ya vipengere katika sheria ya privacy za watu mitandaoni na pia kwa sasa jamiiforums hawarekodi ip adress zetu kwa usalama wetu.

Leo hii watu wengi sana humu wameshapitia msoto mkali sana gerezani.
Hata mama alikubali kwamba Taifa lilifanya koso kubwa kumpa mtu kama huyu madaraka juu. Aliipokea hi kauli "Never never and never again" kumpa mtu mshamba kama JPM huyu Uraisi
 
Kwani Maxence Melo alikwenda jela kwa kesi gani?

Halafu ujuwe member wa JF hawapo Tanzania tu, na server za JF zipo Marekani.

Huu siyo mtandao wa kifala.
Behind the scene Bado Kuna mengi usiyo yajua...
Datc mtu kama kigogo Ali opt kutumia Tweeter why??
Tupo nyuma ya keyboard ⌨️ ⌨️
Hatarisha usalama wa nchi then uone kama hauto patikana??
Let say
Anzisha thread hapa uki utangazia uma kua utaenda kulipua let's say miondombinu yetu sehemu alaf tukio litokee then uone kama utaachwa na kulindwa?!
Najalibu kuwaza
Tunaweza kuulinda UGAIDI hata mello najua hawezi
Nacho jua hapa Jf serikali iki itaji taarifa zako zinapatikana....
najalibu kuwaza
 
Unaunga mkono hoja gani? Maana kati ya watu wanafiki na waimba mapambio kwenye hiyo awamu, wewe ulikuwa ni mmoja wao.

Na ulikuwa unakera sana pamoja na wale wenzako. Ila ilipoingia awamu ya huyu mama, akili ndiyo zimekukaa sawa. Maana unaonekana hauko kwenye kundi la walamba asali
kwan kuna awamu isiyo na mapungufu ? akil zenu ni fupi sana yaan ukimpenda mtu unamuunga mkono kwa kila kitu ndio maana unaonesha attitude yako kwa kumshambulia jamaa , kisa walitaka privacy za watu jf basi tusipongeze ubora wake kwenye nyanja nyngne ?
 
Na wale waliokuwa wanashabikia mambo hayo tuko nao humu wanatoa povu lao kwa nguvu sana kulinda legasi!
Unafiki mtupu.
hakuna serikali timilifu , akili zenu ndo zinafanya siasa kuwa vita , hata Putin au Biden wana mazur na mapungufu , ni kituko kisa matukio mawili au matatu bas usiangalie mazuri mengi ya mtu , huu ukichaa wanao wasomi wa afrika
 
Nafahamu vizuri hata serikali za kina Hitler, Iddi Amin, Mobutu, Makuburu n.k hazikuwa timilifu na zilikuwa na mazuri yake pia.
hakuna serikali timilifu , akili zenu ndo zinafanya siasa kuwa vita , hata Putin au Biden wana mazur na mapungufu , ni kituko kisa matukio mawili au matatu bas usiangalie mazuri mengi ya mtu , huu ukichaa wanao wasomi wa afrika
 
Kuna kipindi hapo awamu ya tano palikuwa na hali ya hatari kwa mtandao wa jamii forums kushinikizwa kutoa kutoa namba za utambulishi za internet IP ADRESS za wanachama wanaokosoa serikali.

Ili uzielelewe kirahisi ip adress ni kwamba tunavyopiga simu ama kutuma meseji namba zetu huwa zinarekodiwa kwenye simu za watu tuliowapigia pamoja na kwenye rekodi za mitandao ya simu, hizi namba mfano wake ni 0769xxxxx. Basi na kwenye internet hakuna utofauti sana ila huku namba za utambulisho zinaitwa ip adress mfano wake huwa ni 192.268.xxx.xxx, hizi namba hazijirudii kama ilivyo kwa namba za simu kila mtu ana yake, ukitaka kuijua ip adress yako tembelea >> hapa <<

ukitembelea tovuti yoyote mfano jamiiforums. com, mitandao ya simu itaona kwamba ip adress inayotumika kwenye simu yako imetembelea jamii forums lakini hawawezi kujua account unayotumia.

Kwa upande wa system za tovuti za mitandao unayotembelea kama jamiiforums, wao ndio wenye tocuti na wanaweza kujua ip adress inayotumika na mtu mwenye account lakini hawana uwezo wa kujua namba ya simu ya anaeitumia hio ip adress. kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba ili mtu afahamike inabidi jamiiforums na mitandao ya simu waungane, Yani mtu wa humu jamiiforums atoe ip adress inayotumika na account mwanachama kisha hio ip adress ikifika kwenye mitandao ya simu wao ndio watajua inatumika na namba ipi ya simu, na hapo utajulikana kirahisi.

Sasa kilichotokea enzi hizo ni kwamba tayari kule walikuwa na access ya kujua namba za simu zinazotembelea jf na wanauwezo wa kumjua mtu endapo jf wakitoa ushirikiano, na ndio hapo sasa jamiiforums wakawa wanafatwa kutoa ip adress zinazotumika na accounts kadhaa ili kuweza kuwatambua ni kina nani wanaikosoa serikali.

Palizuka patashika na tafrani humu ndani isiyo ya kawaida hasa ukizingatia ile awamu ya tano ilikuwa haina masihara na wakosoaji.

Ponea yetu swala hili liligonga headlines kwenye vyombo hata vya kimataifa na hili lilikuwa ni shambulizi ka privacy za watu mitandaoni, si kitu kidogo hiki na tunashukuru Jf, balozi za nchi za nje na asasi kadhaa waliweza kulipiga vita, haikuwa rahisi nakumbuka kesi zilikuwa zinapelekwa mtwarea huko na figisu kibao tu na baadhi ya viongozi wa jf walikatazwa hata kusafiri nje ya mkoa

Hii ilipelekea kuongezewa baadhi ya vipengere katika sheria ya privacy za watu mitandaoni na pia kwa sasa jamiiforums hawarekodi ip adress zetu kwa usalama wetu.

Leo hii watu wengi sana humu wanaokosoa serikali wangekua wameshapitia msoto mkali sana gerezani, hasa ikizingatiwa maafande walishapewa ruhusa na rais wa awamu hio kuwashushia vipigo vizito wafungwa na namnukuu "Wafungwa wafanyishwe kazi usiku na mchana", "wapigwe mateke"
Kwa Asali ya awamu hii. Usishangae IP address zikatolewa kimyakimya
 
Back
Top Bottom