bullar
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 9,530
- 20,988
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa jinsi alivyoandika anaonesha hajui kitu. Kasikiliza nyimbo za lucky akapata mzuka wakuanzisha uzi.1. Paragraph ya kwanza tu unaonekana hujui mambo ya kidunia. Aliyeuwawa ni Lucky Dube (kwa risasi) Bob alikufa tu kawaida kwa kansa iliyoanzia kwenye kidole chake cha mguu.
2. Huwezi mlinganisha Lucky Dube na mkongwe Bob. Lucky anaimba na vinanda sana (huwa tunasema nyimbo zake ni kama kwaya) Bob anaimba ile "Roots Rocky Reggae" yenyewe.
3. Kasikilize nyimbo za Bob kama "Jah live" "Jump Nyabinghi" "Roots Rock Reggae" "Chant Down Babylon" "Them Belly Fully" "Bad card" "Concrete Jungle" "Kaya" najua kwa uelewa wako umeishia zile nyimbo common kama "No woman no cry" "Africa Unite" "Zimbabwe"
4. Fanya hayo hapo juu No. 3 halafu uje ufute huu uzi wako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Dunia yote inamtukuza na kumuhusudu Bob Marley (Culture?) kama mfalme wa muziki rege, sijui wanatumia vigezo gani hasa. Wanamshusha na kumchukulia poa Lucky Dube sijui kwakua Bob aliuawa ndio wanakua na sympathy naye.
Kwa upande wangu japo Dube alimuheshimu Bob ila kwangu dube ndio mfalme wa muziki wa rege duniani. Nyimbo safi zenye ujumbe mwanana, beats zilizoenda shule performance za hadhi ya nyota 15 alizofanya! Nina uhakika Bob angekuwepo wakati Dube Anatoa Album zake 3 za mwanazo (hasa Slave) angempigia magoti Dube na kumsujudu kwa nyimbo bora alizotoa.
Huyu jamaa anajua hasa sikiliza nyimbo zake zote 80% lazima uzipende tu, ukutaka ujue ukali wa huyu mtu angalia Live performance zake utadata.
Najua mtanipinga humu na kunipopoa ila kwangu huyu ndio nishampitisha kua Mfalme wa Rege Duniani, hakuna mwingine.
Ninauhakika huko alipo kapumzika kwa amani maana katimiza kile kilichomleta duniani (Kuhamasisha watu waamke) japo alikua na mapungufu yake kama mtu yoyote yule ila naamini huyu mtu mbingu ni yake na tunaweza mwita mtakatifu kwa kazi yake nzuri.
Sikiliza hizi
Ha ha haThem Belly full
Jah Live
Hizi nyimbo nilishawahi ombea mkopo
Ila kiujumla namsikiliza sana Dube kuliko Bob
Sent using Jamii Forums mobile app
Nani mkali zaidi ya mwingine mkiwa kwenu Sigimbi ndio mnaulizana hivyo,Dube anaimba nyimbo zenye hisia sana na ni rahisi kuzielewa, Bob anaimba nyimbo zenye hisia sana ila nyingi zina ugumu flani katika kueleweka( zina ufalsafa Fulani ndani yake). Nani mkali zaidi ya mwingine!? Sijui ila kila mtu anachagua flavour anayopenda!
Sent using Jamii Forums mobile app
Haitoshi lazima aelekezwe ukweli, uwezi kumfananisha Dube na Marley kila mtu aliwika kwa zama zake na kila mtu ana vibes zake Bob ni mkubwa na Lucky ni mkubwa pia wote walifanya kazi nzuri kwenye ulimwengu wa reggae,
Lucky aliinogesha reggae na vionjo vya Africa, nampenda zaidi Dube ila ukweli Bob Marley ndo Mfalme wa reggae worldwid.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kama simpendi Lucky Dube ila muziki wake nilianza kuupotezea pale alipohusishwa na kifo cha Senzo
"Cᵒᵃᶜᵏʳᵒᵃᶜʰ ⁿᵘʰ ᵇᵘˢˢⁱⁿᵉˢˢ ⁱⁿⁿᵃ ᶠᵒʷˡ ᶠⁱᵍʰT"
Mkuu umeuaSjawai ona reggae ya lucky dube ni orijino hata sku1 ,,naonaga ni kama nyimbo za kwaya,..yaan hana tofaut na waimba bongo fleva wa bongo wanaojidai wanaimba RnB..hiv RnB wanaijua,hyo waachie kina Usher,rkely na chris brown
Sasa ndo lucky dube,yaan kabisa unafananisha regae ya jamieka na ya africa...
We lazima ni mchaga tuu
Nani mkali zaidi ya mwingine mkiwa kwenu Sigimbi ndio mnaulizana hivyo,
Lakini dunia nzima inamtambua Bob Marley.
Ukiona huelewi falsafa ya Bob haikufanyi umu underrate, huyo Dube amekua influenced na kina Bob na Tosh enzi hizo anaimba kwaya kabla hajahamia kwenye Reggae.
Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Unahabari kwamba Senzo yupo hai na hiyo habari haina ukweli wowote?
Kwa mtu anae fahamu mziki wa reggae ni aibu kumllinganisha Bob Marley na Lucky Dube yaani ni sawa kumfananisha Franco na Fally Ipupa ni mlima na kichuguu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Reggae ipo ya aina tofautitofauti kama ilivyomiziki mingine.
Kwakuwa hii ni ishu ya burudani kila mmoja ana preference zake, mwingine anavutiwa na Bob mwingine anapenda kusikiliza nyimbo za Lucky Dube. Hauwezi kulazimisha kila anaesikiliza Reggae amsikilize au kuvutiwa na nyimbo za Bob.
Hauwezi kusema Lucky Dube hakuimba reggae wakati hadi mauti inamfika ulimwengu na dunia kwa ujumla inamtambua kama mwanamziki wa kimataifa wa Reggae. Ntakubaliana na wewe reggae zao zipo tofauri lakini sio kweli kwamba Lucky Dube hakuimba Reggae.
kwahiyo hoja hapa inakuwa kutangulia sio!!!Umenikumbusha kuna wajinga flan wakataka kuanzisha propaganda eti Taylor Swift ni mkali kuliko Michael Jackson hahahaha kizazi cha dotcom kina wazimu sana,
Hawajui kuheshimu michango ya waliowatangulia,
Pathetic.
Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Reggae ipo ya aina tofautitofauti kama ilivyomiziki mingine.
Kwakuwa hii ni ishu ya burudani kila mmoja ana preference zake, mwingine anavutiwa na Bob mwingine anapenda kusikiliza nyimbo za Lucky Dube. Hauwezi kulazimisha kila anaesikiliza Reggae amsikilize au kuvutiwa na nyimbo za Bob.
Hauwezi kusema Lucky Dube hakuimba reggae wakati hadi mauti inamfika ulimwengu na dunia kwa ujumla inamtambua kama mwanamziki wa kimataifa wa Reggae. Ntakubaliana na wewe reggae zao zipo tofauri lakini sio kweli kwamba Lucky Dube hakuimba Reggae.
Mkuu hii topic inadai mfalme wa Reggae Duniani ni Lucky Dube, au hujailewa?