Wengi wanamkubali Bob Marley ila Mfalme wa Reggae duniani ni Lucky Dube

Kwa jinsi alivyoandika anaonesha hajui kitu. Kasikiliza nyimbo za lucky akapata mzuka wakuanzisha uzi.
 



Wewe vipi, huoni kwamba huo wimbo wa pili "Buffalo soldiers" ni wimbo wa Bob marley ambao Lucky Dube karudia kuimba??!!.

Hapo inaonyesha Bob Marley ndiye King of Reggae.
 
Baada ya kukaa Ujerumani kwa miezi akipewa matibabu kwa ajili ya Cancer, iligundulika kuwa hawezi kupona tena na ana muda mfupi tu wa kuishi. Kwahiyo Bob Marley aliamua arudi nyumbani, japo aione Jamaica 🇯🇲 kwa mara ya mwisho. Kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufika. Akiwa njiani, siku kama ya leo, tarehe 11,mwezi wa 5,mwaka 1981, Bob aliaga Dunia, Miami, Florida.

Muda mfupi kabla ya kifo chake, Bob Marley alipokea Order of Merit by the government of Jamaica. He had also been awarded Medal of Peace from United Nations 1980.

Mazishi ya Bob Marley yalikuwa ya kihistoria. Alizikwa na umati wa watu 30,000 kutoka pande zote za Dunia.
 
Nani mkali zaidi ya mwingine mkiwa kwenu Sigimbi ndio mnaulizana hivyo,
Lakini dunia nzima inamtambua Bob Marley.

Ukiona huelewi falsafa ya Bob haikufanyi umu underrate, huyo Dube amekua influenced na kina Bob na Tosh enzi hizo anaimba kwaya kabla hajahamia kwenye Reggae.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 

We ndio unajua. Lucky Dube mwenyewe alimheshimu na kuwathamini Bob na Toshi, niliwahi kumsikiliza akifanya mahojiano akasema Peter Tosh ndio alumpa hamasa ya kuima Reggae wakati huo alikua akiimba Mbakanfa yenye asili ya ki afrika kusini.

Bob anabaki kuwa mfalme kwa vile ni kama muasis wa reggae, hiyo haitafutika hata atokee mwingine hawezipata hiyo heshima ila atathaminiwa na kutambuliwa kazi yake.

Binafsi, namwelewa sana Dube.
 

Unahabari kwamba Senzo yupo hai na hiyo habari haina ukweli wowote?
 
Kwa mtu anae fahamu mziki wa reggae ni aibu kumllinganisha Bob Marley na Lucky Dube yaani ni sawa kumfananisha Franco na Fally Ipupa ni mlima na kichuguu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hapo nimemu underrate Bob au siyo!?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu anae fahamu mziki wa reggae ni aibu kumllinganisha Bob Marley na Lucky Dube yaani ni sawa kumfananisha Franco na Fally Ipupa ni mlima na kichuguu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Reggae ipo ya aina tofautitofauti kama ilivyomiziki mingine.

Kwakuwa hii ni ishu ya burudani kila mmoja ana preference zake, mwingine anavutiwa na Bob mwingine anapenda kusikiliza nyimbo za Lucky Dube. Hauwezi kulazimisha kila anaesikiliza Reggae amsikilize au kuvutiwa na nyimbo za Bob.

Hauwezi kusema Lucky Dube hakuimba reggae wakati hadi mauti inamfika ulimwengu na dunia kwa ujumla inamtambua kama mwanamziki wa kimataifa wa Reggae. Ntakubaliana na wewe reggae zao zipo tofauri lakini sio kweli kwamba Lucky Dube hakuimba Reggae.
 
Umenikumbusha kuna wajinga flan wakataka kuanzisha propaganda eti Taylor Swift ni mkali kuliko Michael Jackson hahahaha kizazi cha dotcom kina wazimu sana,

Hawajui kuheshimu michango ya waliowatangulia,
Pathetic.

Boost your Immune System to fight a Covid-19.
 
Wabongo wajuaji sana!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwahiyo hoja hapa inakuwa kutangulia sio!!!
 


Mkuu hii topic inadai mfalme wa Reggae Duniani ni Lucky Dube, au hujailewa?
 
Mkuu hii topic inadai mfalme wa Reggae Duniani ni Lucky Dube, au hujailewa?

Nimeielewa sana, nilikua namjibu mhusika niliyemnukuu.

Kuhusu Luck Dube kuwa mfalme wa reggae ngumu. Ni sawa na mchezaji aibuke leo mcheza soka useme huyo ndio mfalme wa soka kumpiku Pelle. Yaani kuna ile heshima anapewa mtu kwa kazi aliyoifanya.

Lucky Dube alikua vizuri sana tu kwa eneo lake ila mfalme wa reggae anabaki kuwa Bob.

Unafikiri akitokea kiongozi wa kutolewa mfano leo akafanya maajabu ataitwa Baba wa taifa? Hiyo ni heshima ya Mwl. Nyerere tu, haitafutika kamwe.

Naamini umenielewa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…