Wengi wanamkubali Bob Marley ila Mfalme wa Reggae duniani ni Lucky Dube

Hujui reggae muzik wewe... luck dube na sweat reggae wapi na wapi? Dube anaimba kwaya. Sweetie reggae walikuwa wanaimba UB40 kitambo hiyo sasa muziki wao wale unafanana na wa luck dube? Sweetie reggae inambwa na akina Morgan heritage family, octane,qeen ifrica etc ambawo muziki wenyewe ni tofauti kabisa na reggae aliyokuwa akiimba lucky dube.... lakini aina zote hizo za reggae zimetokana na roots ambayo alikuwa akiimba bob, so kumfanisha bob na dube ni sawa kumfananisha kwenye soka fei toto na johan cruyff
 
Kila mtu na taste yake lakini toka mwaka huu uanze sijamsikiliza Bob.
 
Hata RFA walipambanisha ila kwa ushamba wa wackilizaji wakampa ushindi luck dube, nilishangaa sana. Bob mwisho wa matatizo. Dube mtoto mdogo akalale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bob ni kiumbe chengine. yaani nikisikiliza no woman no cry ndo nahisi hasa ladha ya bob
 
mziki wa bob unahitaji akili kubwa sana kuuelewa, ukiona mtu atambui bob n nan co kosa lake kosa ni low IQ iliyoshindwa kuelewa mafumbo na vitendawili vilivyopo kwny mziki wake
bob kaimba mziki ambao hata ipite karne ukiusikiliza unaona kabisa unareflect the real situation in a society
bob was a prophet asee
rip legend


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeenda vizuri

Lakini lukcy dune kumfananisha na senzo is not right

Lucky dube anakimbizana na akina alpha blondy
 
mziki wa dube una nafasi ya kuishi miaka 100 mbele kuliko wa bob.

leo hii hata ukikamata kijana wa miaka 18,hamjui bob ila dube anamjua,unajua kwanini!!!,mwamba aliimba nyimbo zinazoeleweka na watu wote.

hata baadae kuna uwezekano akaja kutambulika kama muasisi wa reggae kwa vizazi vijavyo,haitakuwa bahati mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sipendi nyumbo za bob ila nampenda sana dube yaan ni mfuasi wake wa kufa na kufurukutwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu sijui wanafikiriaje, huwezi kumfananisha mwanamuziki aliyewika worldwide na mwanamuziki anayefahamika kusini mwa jangwa la Sahara pekee.
sasa unadhani kosa lilikuwa anachoimba au anaimba akiwa wapi???hivi unadhani dube angezaliwa marekani hali ingekuwaje!!!!!

na vile alikuwa na muonekano a ajabu ajabu ndio kabisaa,wengi wenu mkanuna mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa unadhani kosa lilikuwa anachoimba au anaimba akiwa wapi???hivi unadhani dube angezaliwa marekani hali ingekuwaje!!!!!

na vile alikuwa na muonekano a ajabu ajabu ndio kabisaa,wengi wenu mkanuna mazima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lucky Dube alishindwa kumfunika Alpha Blondie, ndio umpambanishe na muasisi wa reggae. Mkuu hebu kuwa serious basi.
 


Wasiomfahamu Bob Marley ni watu wa wapi? Tuanze hapo kwanza. Maana sio uko tu Mbagala, unakuja kuleta madai kwamba watu Duniani hawamfahamu Robert Nesta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…