Wengi wenye vitambi walipata utapiamlo utotoni

Wengi wenye vitambi walipata utapiamlo utotoni

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habarini wakuu sana.

Ipo namna hivyo. Watu ambao hawakupata lishe ya kutosha utotoni huwa wanapoteza uwezo wa kuchakata msosi. Yaani mwili wake unavyotumia chakula ni tofauti na mtu ambaye alipata lishe ya kutosha.

Sasa mtu huyu akipata pesa au uhakika wa msosi ukubwani, anajikuta anakula kuliko uwezo wa mwili wake kuchakata msosi. Jambo hili linapelekea tatizo la obesity, kitambi, kisukari na magonjwa mengine yatokanayo na ulaji mbaya.

Ni vema tujitahidi wapate mlo kamili utotoni, maziwa na nyama ni muhimu sana. Na kama hukupata chakula kamili utotoni na ukapata udumavu, punguza ulaji usio na afya.
 
Habarini wakuu sana. Ipo namna hivyo. Watu ambao hawakupata lishe ya kutosha utotoni huwa wanapoteza uwezo wa kuchakata msosi. Yaani mwili wake unavyotumia chakula ni tofauti na mtu ambaye alipata lishe ya kutosha. Sasa mtu huyu akipata pesa au uhakika wa msosi ukubwani, anajikuta anakula kuliko uwezo wa mwili wake kuchakata msosi. Jambo hili linapelekea tatizo la obesity, kitambi, kisukari na magonjwa mengine yatokanayo na ulaji mbaya.

Ni vema tujitahidi wapate mlo kamili utotoni, maziwa na nyama ni muhimu sana. Na kama hukupata chakula kamili utotoni na ukapata udumavu, punguza ulaji usio na afya.
Kinyume chake ni kweli.
Watoto waliokula kupita kiasi hasa vyakula vya sukari mfano maziwa ya ng'ombe wako kwenye hatari kubwa ya kupata unene ukubwani.
Unene ni dalili ya ugonjwa unaoitwa insulin resistance. Na huu ni ugonjwa huanza wakati wa utoto ila unaweza usijitokeze hadi ukubwani.

Unene uliopita kiasi hausababishwi na kula sana,mtu anaweza kula kidogo tu na bado akanenepa kama ana ugonjwa huu wa insulin resistance.
Hata magonjwa kama kisukari hayasababishwi na unene kama tunavyoambiwa.Kisukari pia ni dalili ya ugonjwa wa insulin resistance.
 
Hapana. Watoto wanaokula kupita kiasi wako kwenye hatari ya kupata obesity ya utotoni. Watu ambao hawakupata mlo kamili utotoni wapo katika hatari ya kupata obesity ukubwani.

Na unene ndiyo husababisha insulin resistance, siyo insulin resistance kusababisha unene.
 
Unda group la watakaochangia au ignore me....la sivyo nitachangia chochote mkuu
Karibu mkuu kuchangia. Nilikuwa tu nakupa tu mawili matatu. Kama huna cha kuchangia, na hasa kama huna cha maana unatulia.
 
Back
Top Bottom